Hizo ni Qualities za a good leader kwa mujibu wa wazungu, kama ilivyo demokrasia yao, kuwa ni serikali ya watu, inayoongozwa na watu kwa ajili ya watu, but not in Africa. Kule leaders are selfless, viongozi ni watu waliojitosheleza na wanagombea uongozi ili kutumikia watu, kuwa watumishi wa watu, huku Africa, watu wanagombea uongozi ili kuukwa, kukamata madaraka, ukubwa na ulaji, sio ili kutumikia watu bali uabudiwe, unyenyekewe, usifiwe.
Africa hatuhitaji leaders kutuongoza, we just need rulers to rule, yaani tunahitaji watawala tutawaliwe. Rais Magufuli ni mtawala anatutawala.
Demokrasia yetu ni serekali yangu, inayoongozwa na mimi kwa ajili yangu, na watu wangu na chama changu na walionichagua!.
Ni kufuatia haya mambo ya kuendekeza good leadership na good governance ndio yametufikisha hapa, sasa tuko kwenye Tanzania ya Magufuli na Dar es Salaam ni jiji la Makonda,
hatuhitaji hizo qualities, tunataka maendeleo, mambo yaende hata ikibidi kwa mijeledi, mambo ya kubembelezana hakuna tena, siasa hakuna, hapa ni kazi tuu!. Hii ndio Tanzania ya Magufuli.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
P