Kiongozi bora ni yupi basi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi bora ni yupi basi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 23, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tutaweza vipi kumtambua kiongozi bora, atakuwa na sifa zipi? Je kiongozi bora anaweza kutokea katika Tanzania?

  Je kiongozi ambaye hataki mzaha, hachelewi kuchukua hatua na anayejua anaongozwa na falsafa ya aina gani ndiye Tanzania inamhitaji au inahitaji kiongozi ambaye anatawala kwa amri yake.

  Kati ya wanasiasa tulio nao hivi kweli kuna yeyote ambaye tunaweza kusema ni kiongozi bora?
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jamii yoyote ambayo inategemea mawazo na ushauri wa jamii zingine ili kujiletea maendeleo yake haiwezi kuwa na viongozi bora kwa sababu viongozi hao watatokana na matakwa ya wale wale ambao walitunga na kuendesha mawazo hayo

  sasa kwa afrika na nchi nyingi zinazoendelea utaona inategemea viongozi wanaoenda kufundishwa na wengine kupewa misaada na mambo mengi na wengine ili waje kuendeleza kwao ila wao wanachofanya sio kuendeleza ni kunyanganya kile kilichopo na kukirudishwa walioleta ushauri
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Kheheheheheheheeeee.....wewe karibu utadata sasa.....
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Shy, una point nzuri hapa... lakini naona umevurugavuruga katika kuilezea. Tafadhali iandike tena, itajileta tuu...
   
 6. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wenzetu Kiongozi ni mtu anayeandaliwa kwa muda mrefu na watu wanaendelea kumpima kabla hajawa kiongozi. Hapa kwetu loooool mtu anatokea from nowhere anapigania anakuwa kiongozi taabu kwelikweli
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Hmmmmm....sounds like presidential wannabe (who won't be) Obama.....
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hata kama atokee ghafla from no where, as long as anafata kanuni, masharti ya kazi, kiapo chake na ni mwenye kupenda maendeleo yake na yale ya jamii yake, haijalishi; huyo atakuwa ni mwenye sifa ya kiongozi bora.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Sawa, lakini ni muhimu kurejea na kuona utendaji wake wa kazi huko nyuma na misimamo aliyokwisha chukua na maamuzi aliyoyafanya. Sasa mtu anayetokea ghafla from nowhere mtajuaje hayo yote? Ndio maana mimi nilimpinga Kikwete tokea 1995 kwa sababu sikuona chochote alichowahi kufanya kumfanya akwolifai kuwa raisi ukiacha kwolifikesheni zilizotajwa kwenye katiba. The guy has no track record of achievement and accomplishments...none...nada!!!!!!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mnataka kusema kuwa kiongozi bora kabla ya kuwa kiongozi anakuwa na rekodi inayopimika? Sasa mtu hawezi kuanzia 0 na kuwa kiongozi bora au hadi awe na rekodi inayopimika? Na katika rekodi hiyo ni vitu gani vitakuashiria kuwa huyo mtu ni kiongozi bora?
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nyani, swali limeuliza 'kiongozi bora ni yupi basi' halijaongelea kiongozi bora na mwenye experience ni wa aina gani... au?!

  Track record na experience katika kitu fulani ni nyongeza ambazo zinaweza kujumuishwa katika huo uongozi bora. Kama track record ni mbaya, then huyo siyo kiongozi bora mpaka hapo mnapom-judge hivyo. Kama ni nzuri, basi ni kiongozi bora mpaka hapo pia. Kama alikuwa na track record mbaya kisha akafata misingi yote ya kazi yake kama nilivyotaka kuelezea hapo juu bila kubadilika, then huyo atakuwa kiongozi bora - ambaye huko nyuma alikuwa na track record mbaya lakini akaamua kubadilika for better. And vice versa.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mtu kama Andrew Chenge akigombea uraisi na kushinda (pamoja na maskendo yake yote) halafu akafanya kazi kufuata misingi yote ya kazi kama "ulivyoelezea", atakuwa kiongozi bora na wala maskendo yake hayatakusumbua?
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni kweli, yatanisumbua. Kwa sababu nitakuwa nimeangalia matendo yake ya zamani, ila sitokuwa nimepima future ya uongozi wake ambao nimekubali kuwa ni bora. Which is which....

  Nyani, haya mambo ya hypothesis sasa.... je akija mpya mpya bila ya mimi kujua hayo maskendo, kisha akaonyesha sifa zote kama nilivyoelezea?
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Basi wewe utakuwa uninformed voter na mimi nitakuwa informed voter..... nitakuwa skeptical...nitajua ni geresha tu
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .... kwani kiongozi bora ni lazima awe voted in?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  sio lazima.......
   
 17. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #17
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kama gadafi wa libya si ndio?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Asilimia 80 ya wapiga kura mwaka 2005 walimuona JK ni kiongozi "bora".... walikosea wapi?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Oct 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Hawakuangalia ni wapi/ lini na kwenye nini alionyesha uongozi. Walikunywa kool-aid ya ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya (kinda like hope and change)......
   
 20. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Unasema "walimuona"???!
  .
   
Loading...