Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,103
- 43,350
Jamii yoyote ambayo inategemea mawazo na ushauri wa jamii zingine ili kujiletea maendeleo yake haiwezi kuwa na viongozi bora kwa sababu viongozi hao watatokana na matakwa ya wale wale ambao walitunga na kuendesha mawazo hayo
sasa kwa afrika na nchi nyingi zinazoendelea utaona inategemea viongozi wanaoenda kufundishwa na wengine kupewa misaada na mambo mengi na wengine ili waje kuendeleza kwao ila wao wanachofanya sio kuendeleza ni kunyanganya kile kilichopo na kukirudishwa walioleta ushauri
Wenzetu Kiongozi ni mtu anayeandaliwa kwa muda mrefu na watu wanaendelea kumpima kabla hajawa kiongozi. Hapa kwetu loooool mtu anatokea from nowhere anapigania anakuwa kiongozi taabu kwelikweli
Wenzetu Kiongozi ni mtu anayeandaliwa kwa muda mrefu na watu wanaendelea kumpima kabla hajawa kiongozi. Hapa kwetu loooool mtu anatokea from nowhere anapigania anakuwa kiongozi taabu kwelikweli
Hata kama atokee ghafla from no where, as long as anafata kanuni, masharti ya kazi, kiapo chake na ni mwenye kupenda maendeleo yake na yale ya jamii yake, haijalishi; huyo atakuwa ni mwenye sifa ya kiongozi bora.
Sawa, lakini ni muhimu kurejea na kuona utendaji wake wa kazi huko nyuma na misimamo aliyokwisha chukua na maamuzi aliyoyafanya. Sasa mtu anayetokea ghafla from nowhere mtajuaje hayo yote? Ndio maana mimi nilimpinga Kikwete tokea 1995 kwa sababu sikuona chochote alichowahi kufanya kumfanya akwolifai kuwa raisi ukiacha kwolifikesheni zilizotajwa kwenye katiba. The guy has no track record of achievement and accomplishments...none...nada!!!!!!
Nyani, swali limeuliza 'kiongozi bora ni yupi basi' halijaongelea kiongozi bora na mwenye experience ni wa aina gani... au?!
Track record na experience katika kitu fulani ni nyongeza ambazo zinaweza kujumuishwa katika huo uongozi bora. Kama track record ni mbaya, then huyo siyo kiongozi bora mpaka hapo mnapom-judge hivyo. Kama ni nzuri, basi ni kiongozi bora mpaka hapo pia. Kama alikuwa na track record mbaya kisha akafata misingi yote ya kazi yake kama nilivyotaka kuelezea hapo juu bila kubadilika, then huyo atakuwa kiongozi bora - ambaye huko nyuma alikuwa na track record mbaya lakini akaamua kubadilika for better. And vice versa.
Kwa hiyo mtu kama Andrew Chenge akigombea uraisi na kushinda (pamoja na maskendo yake yote) halafu akafanya kazi kufuata misingi yote ya kazi kama "ulivyoelezea", atakuwa kiongozi bora na wala maskendo yake hayatakusumbua?
Ni kweli, yatanisumbua. Kwa sababu nitakuwa nimeangalia matendo yake ya zamani, ila sitokuwa nimepima future ya uongozi wake ambao nimekubali kuwa ni bora. Which is which....
Nyani, haya mambo ya hypothesis sasa.... je akija mpya mpya bila ya mimi kujua hayo maskendo, kisha akaonyesha sifa zote kama nilivyoelezea?
Basi wewe utakuwa uninformed voter na mimi nitakuwa informed voter..... nitakuwa skeptical...nitajua ni geresha tu
.... kwani kiongozi bora ni lazima awe voted in?
Asilimia 80 ya wapiga kura mwaka 2005 walimuona JK ni kiongozi "bora".... walikosea wapi?
Asilimia 80 ya wapiga kura mwaka 2005 walimuona JK ni kiongozi "bora".... walikosea wapi?