Kipi heri? Kuamini kuwa Mungu yupo na kwamba huwapa thawabu watu wote wanaomwamini na kumwabudu AU Kuamini kuamini kinyume chake? Bwana Yesu kristo anatushauri : HERI KUAMINI MUNGU LAKINI BAADA YA KUFA USIMKUTE KULIKO KUTOAMINI HALAFU UKIFA UNAMKUTA! adhabu unayopata huko kwa KUTOAMINI kwako ni MBAYA SANA. Hatuhukumiani lakini pia Tusifarijiane bure. Tusiendekeze na kudanganywa na kiburi cha uzima pamoja na fahari ya Dunia hii inayopita. Sisi ni wasafiri na wapitaji tu hapa. Tusidangangwe na elimu tulizonazo. Elimu ya Dunia hii humjengea mwanadamu moyo wa kiburi. Mambo ya BWANA Mungu mtu huyajua kwa msaada wa Roho Mtakatifu. TUOKOKE wandugu ili tujazwe na Roho Mtakatifu kinyume chake ni vigumu sana kuurithi Ufalme wa BWANA Mungu ambao Bwana Yesu kristo ndiye haswa MFALME wa WAFALME na BWANA wa MABWANA!