Kwa wenye madishi sijui itakuwaje?
itv wako zuku..hivi karibuni
Kaka nadhani utakuwa umechanganya mambo,hizi local channels ndizo zinatakiwa ziwalipe hawa service provaida(startimes na ting)ili chaneli zao ziwe kwenye package zao.mi kuna semina nilihudhuria iliyotolewa na tcra,kwa wamiliki wa station za tv,waliambiwa watatakiwa kuwa wanalipa kama tsh.milioni mia sita kwa mwaka!kwa kila mwenye station ya tv kulipa hayo makampuni(startimes,ting na mengine)ikaleta malalamiko sana, wadau wakasema ni kiwango kikubwa sana hawatakimudu,tcra wakasema ngoja watarijadili,sijui kama wameshalitolea ufafanusi tena.Hadi sasa ni Startimes, Ting na Zuku ndio wanatoa service ya kurusha matangazo kwa njia ya TERRESTRIAL DIGITAL VIDEO BROADCAST (T-DVB) ambayo ni digital ambayo haitumuu satellite wala madishi(ingawa wanayo pia).
Swala la akina ITV na Star Tv ni la kibiashara zaidi, hawa akina Startimes na Ting na Zuku kazi yao ni kukusanya station mbali mbali za bure na za kulipia na kuziweka kwenye package zao kwaajili ya kuziuza kwa malipo ya mwezi.
Sasa kama akina ITV wakipeleka chaneli zao Startimes au Ting maana yake wao watakuwa wanalipwa sehemu ya mapato,
Wao wanachotaka ni wao pia kutafuta chaneli zingine na wao kuja na kampuni zao ambapo kibiashara inalipa zaidi
Na ndio maana TCRA imesema italazimisha kampuni zote kuhakikisha zinakuwa na chaneli zote local na ziwe free kama ilivyokuwa kwa Startimes na TBC, hata muda wa package yako unapokwisha unaendelea kuiona TBC
Kwa wanaotumia madish wao wataendelea kupeta kama kawaida
Kiukweli TCRA wanatakiwa kuandaa lots of public information programs kutuelewesha jambo hili.
Ninavyo fahamu mimi, tangu tarehe 1/1/2013, vituo vyote vya TV vinageuka content provider tuu yaani waandaaji vipindi tuu na warushaji ndio hayo makampuni 4 ya multiplex providers. Hii inamaanisha hata sisi jf tunaweza kufungua JF TV na kupewa channel yetu 24/7 wakati kwa sasa ili kutangaza ni lazima ama upeleke ITV, TBC au TV zilizopo!.
Ujio wa Digital ni ukombozi mkubwa.
Amoeba, vituo vya TV ndio vinageuka vinageuka content provider na kulipia tx kwa hao multiplex wanne! Gharama bado sijajua ila hitaji la kupewa kibali cha kuwa content provider ni ama kuwa na production studio, au kuingia mkataba na production house.Hapohapo Pasco, hili suala kila nayeongea nae ananipa majibu tofauti! Content provider anamuuzia vipindi mwenye kituo cha TV, au anakuwa na TV yake ambayo kurusha anakodi nafasi kwa wenye transmitter za digital na leseni? Na gharama kwa mwaka ndy M600?!!!...yaani 50M kwa mwezi?..hahahaa Na je TV za kikanda hazitakuwepo?...kama mimi nataka kurusha matangazo katika zone flani tu inaweza? Maswali mengi bila majibu!
Amoeba, vituo vya TV ndio vinageuka vinageuka content provider na kulipia tx kwa hao multiplex wanne! Gharama bado sijajua ila hitaji la kupewa kibali cha kuwa content provider ni ama kuwa na production studio, au kuingia mkataba na production house.
Providers wote wanne watalazimika kurusha bure channel zote za free to air, yaani hata kingamuzi cha star time lazima kionyeshe bure tv zote za bure!.
Nimekuelewa mkuu, je unaweza kunisaidia kupata hizo gharama,au mawasiliano ya wahusika! Natanguliza shukrani!
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
|
itv wako zuku..