MWENYEKITI wa kampeni ya mgombea urais wa CCM, Abdulrahman Kinana juzi alisema kwamba wapinzani hawana jipya.
Alitoa kauli hiyo wakati akimnadi kwa wananchi wa Arusha mgombea ubunge wa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.
Alisema,Dk Batilda ni lulu kwa wananchi wa jimbo hilo na hivyo wanapaswa kumpa kura zote ili awe Mbunge.
Kinana alisema,wapinzani wanazungumzia tatizo la ufisadi na ubadhirifu ambayo yameshashughulikiwa na serikali ya CCM na wao wanayarudia tu.
Kinana alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mgombea huyo wa CCM na kuwasihi wananchi wa Arusha kutofanya kosa kuiachia lulu na hazina hiyo.
Alisema, kuna watu watapita huko na kule kueleza ubaya wa mgombea wa CCM lakini nyie msidanganyike kwa maneno yao kwani kila kukicha wanazua mapya yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Wapinzani hawana jipya kwa sasa wasikilizeni na muwaache hapo hapo wala msiwafikirie kwani mtaumiza vichwa bure, alisema.
Dk. Buriani aliwaomba wananchi wa Arusha wamchague yeye awe Mbunge wa jimbo la Arusha kwa sababu wana uhakika wa kuweka Jiji la Arusha katika hadhi ya kimataifa zaidi.