Kinana ameua kabisa upinzani

Kinana ameua kabisa upinzani

Huuniujinga sana anajifanya yupo pamoja na watu wachini hakuna kitu watu tumelima mahindi mnafungua soko mnanunua tani elfu20 na kituo kina tani lakimoja afu mnaongea blabla tu! mkivishwa nahizo kofia,kanga na tshirt kwisha!
 
Atakufa yeye kabla upinzani haujafa!
 
Nilijua unasema kaua TEMBO kumbe Upinzani!!!!! Ooohh, my left Foot....

BACK TANGANYIKA
 
huyu kanali mstaafu wa jeshi hapana chezea kabisa. Pamoja na cheo kikubwa sana alichonacho lakini hajali hali.. Anashiriki kazi za mikono na jamii anayoikuta. Si kulima, kujenga, kuendesha baskeli, bodaboda, kula kwa mama ntilie na hata kuvaa kiatu cha tairi maarufu sendeu kule kwetu.

Tabia hii ya kinana ni janga kuu kwa upinzani uliobaki na sera ya maandamano haram ya kuvizia, ya kuhamasisha vurugu,matusi na lugha za kuudhi...

Nawashauri wapinzani waige nyendo za huyu jamaa.

we kweli chizi unadai kaua upinzani halafu unawashauri wapinzani wamuige.je maiti zinaweza kuiga?
 
Naona buku saba zimeshaingia mifukoni mbona tutakoma!
 
Watanzania hawahitaji watu wanafiki kama kinana, watanzania hatuhitaji watu kama hawa wanaojifanya eti wanawasaidia kulima na kujenga, tunahitaji huduma nzuri kwa wajawazito,watoto, wazee,na watanzania kwa ujumla

watanzania tunataka elimu bora kwa wote sio unafiki wa kinana kuendesha baiskeli kuwalaghai watanzania bali tunataka wezi na mafisadi wafilisiwe,wanyongwe

Kinana ni mnafiki kwa sababu anajifanya eti aonekane anawajali watanzania kumbe ni wale wale wanaofaidika na wizi,ufisadi. tunataka sement ishushwe bei, mabati,nondo na misumali ishuke bei kila mtanzania aweze kujenga nyumba ya kisasa. ETI KINANA ANAWALAGHAI WATANZANIA KWA KUWASAIDIA KUJENGA NYUMBA ZA MATOPE badala ya kushauri mafisadi washushe bei ya cement ili hawa anaowalaghai wajenge nyumba za kisasa
Pia hawahitaji wazinzi na wapora wake za watu kama dr slaa
 
Watu wengine bana! Sijui huwa wanakosa cha kuandika?
Mtakuja kubebwa mzega mzega kupelekwa Milembe kupimwa wakidhani mnaumwa. (Akili).
Siku nzima unakaa unafikiria cha kuandika hatimaye unaibuka na uoza kama huu?
Au unapenda kuona wangapi wanachangia hoja yako?
 
CCM kimebaki ni chama cha maigizo sawa na Kingwendu na Masanja mkandamizaji.Kushika tope lililoandaliwa na wananchi na kuliweka juu ya ukuta uliojengwa na wananchi wote bila kujali itikadi zao nako ni kuuwa upinzani?Kupanda miti iliyoandaliwa na wananchi tena akiwa amepiga magoti juu ya kapeti alilotandikiwa na wananchi ili asichafuke nako ni kuuwa upinzani au ni maendeleo?kuvaa makurubasi nako mnaita maendeleo au ni maigizo?nenda nyumbani kwa Kinana uone kama utayakuta makurubasi yake hata ya familia yake hutayakuta pia kama utakuta Kinana na familia yake wanakula chakula kama kinachopikwa na mama nitilie.CCM ni sawa na muigizaji yeyote yule anaye fanya maigizo ili mkono uende kinywani.
 
kuna ule wimbo wa kitoto unasema, danganya toto tule, halafu unamaliziaje vile?.................
 
Sababu kubwa ya Kinana kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi ni kukagua sehemu yenye tembo wengi awashughulikie
 
Watanzania wanapenda sana maigizo,kwa hiyo hilo igizo la kinana lishakumaliza kabisa? Lol!.
 
Wapinzani wenyewe wote majuha kinana kamalizia kwisha habari yao.

Ukubwa wa Upinzani ndio uliomfanya Kinana apite kila mtaa ,hivi kuna kumbukumbu zozote kwa mkuu wa CCM kufanya ziara kubwa ya kutumia hela za chama kiasi anavyozitafuna Kinana ,usifikiri yeye na Nape wanazunguka bure ? Kuna ulaji hapo wenzao wanakula BMK wao wanatafuna vijijini ,akushindae kea tonge mshinde kwa kutowea ,upo ?

Weka kando hayo ya ulaji ni yao ! Kinana anachokifanya ni kuwalewesha wananchi kwa mtindo uleule wa kiccm kuwadanganya wananchi kwa ahadi ,unafikiri wananchi hawalielewi hilo ? tumewasikia wananchi wakimlalamikia Kinana malalamiko lukuki ,anachokifanya Kinana kama umeangalia ni kuwa mkali sana kwa watekelezaji wa serikalini na huwabebesha mzigo wenziwe ,mambo ambay walikuwa walaumiane ndani ya baraza lao la ya CCM ,Kinana anawatwisha wenziwe kuwa ndio sababu ya kucheleweshwa miradi na maendeleo mbalimbali huko vijijini. Anashindwa kuwaeleza kuwa Chama chake hakifuatilii mambo hayo ila unapokaribia uchaguzi.

Anachokifanya kinana ni kurahisisha wizi wa kura na ubadilishaji wa matokeo ya uchaguzi ,itakubidi uwe mwelewa sana hapo ili upaone.

Hivi ni kweli kinana anakula kwa mama ntilie ,hivi ni kweli kinana anaendesha baiskeli ,hivi ni kweli kinana analima ,Kinana kwa kuyafanya yote hayo ni kujivisha ngozi ya kondoo ili aonekane na yeye ni katika hao.

Wananchi hawataki kiongozi wao ashike jembe wala apande baiskeli mbele ya macho yao ,ninachokiona ni kwa wananchi hao kukilalamikia Serikali ya CCM kuwa imewatupa vibaya sana na suluhisho ni kuwa haiwajali ,sasa Kinana amekuja kuwambia nini wakati huu unapokaribia uchaguzi,hilo ndilo wanalokwenda kulisikia kwa Kinana na sikumuona akilima au kupanda baiskeli ,au hufuatilii mikutano yake ni malalamiko tu kutoka kwa wananchi ,hakuna sehemu ambayo wananchi wanaishukuru serikali kupitia Kinana ,hakuna !

Jawabu analolitoa Kinana ni kuwajibu ,nitalifuatilia ,nani mwenyekiti wa Kijiji nani mbunge ,nani mkuu wa mkoa ,nitataka kujua kabla sijaondoka hapa ,yuko wapi mwite na viambatanisho kibao vya ubabaishaji ,akiondoka anawaachia mzigo watawala wa maeneo ,anakuwa ameshajenga chuki ,kwa kweli anawavuruga na kujenga makundi.
 
ukubwa wa pua si wingi wa kamasi...ukubwa wa upinzani si ukubwa wala uzito wa hoja...wale ni wahuni tu
 
Kinana kaua Ndovu sio kau upinzani, ngoja mgombea Huru Lowasa apite uone kama jel ataikwepa.
 
Eti anatoka kipara kwa kuzifikiria shida na matatizo ya watanzania
 
Back
Top Bottom