Uchaguzi 2020 Ushauri kunusuru upinzani ‘kidharura’: CHADEMA msimamisheni Membe, ACT msiweke mgombea bara; Haitawapa ushindi ila itawasaidia kuendelea ku 'savaivu'

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Disclaimer;

Mtoa ushauri huu ni mwana CCM anayeamini katika demokrasia. Anaamini CCM imara itatokana na uwepo wa upinzani bora kwa kuwa CCM itapata kioo cha kujitazama, na kufa kwa upinzani kutasababisha CCM isiwe na pa kujipimia na hivyo ubora wake kuyumba.Kama Simba ikipotea kabisa, hatuwezi kuwa na Yanga tunayoijua leo, bali tutakuwa na kitu kingine kabisa.

Hivyo ushauri huu haulengi kusaidia vyama vya upinzani kushinda kiti cha urais Tanzania bara kwa kuwa hilo kwa sasa haliwezekani (kutokana na sababu mbalimbali) lakini angalau kusaida vyama hivyo kubaki kwenye ramani baada ya uchaguzi wa oktoba.

================
‘Facts nne (4) za wazi sana (Hizi ukiona mtu anabisha ni kwa kuwa tu anatumia uhuru wake wa kidemokrasia. Ni kama mtu anavyoweza kubisha kuwa dunia sio duara)

Kwanza, kwa hali ilivyo kuna dalili za wazi sana kwa CHADEMA kupoteza karibu viti vyote vya ubunge bara, na Zbar hawana dalili ya kupata kiti hata kimoja.(ili kuepuka kutanua sana mjadala hatutajadili sababu moja moja kwa kuwa zipo wazi sana tayari)

Pili, ACT wana dalili ya kutopata kiti hata kimoja bara lakini kupata viti kadhaa Zbar

Tatu, kwa upande wa urais bara, Rais Magufuli ana uhakika wa kishinda kwa 99%. Kwa sababu ambazo pia ziko wazi sana. na

Nne, Vyama vya upinzani vyenye ushawishi kiasi kwa bara kwa sasa ni CHADEMA na ACT, wengine ushawishi wao uko chini sana.

Kwa nini CHADEMA wamsimamishe Membe na ACT wasisimamishe mgombea?

Kwanza, Lissu ndie mpinzani pekee anayeweza kum challenge rais Magufuli kwa kiasi fulani, japo pia hawezi kumshinda kwa sababu mbalimbali. Kwa bahati mbaya lisu yuko ulaya na ndege haziruki kutoka ulaya kwa sasa. Kwa hiyo upo uwezekano ukafika wakati wa kuchukua fomu na Lissu kakwama ulaya.

Pili, kuhusu mbowe; kwa tukio lililotokea Dodoma, iwe maelezo yaliyotolewa kwa upande wa polisi ndio kweli au maelezo yaliyotolewa upande wa Mbowe ndio kweli; tukio kama lile kutokea kwenye kipindi hiki linamfanya Mbowe kuonekana hayuko serious vyakutosha na hivyo sio ‘presidential material’.

Tatu , kuhusu Msigwa; Kwa tukio la kumsingizia mzee Kinana kuwa anaua tembo (huku akijua ametunga tu kichwani kwake kwa hila) na asiombe msamaha kwa miaka na miaka hadi ahukumiwe mahakamani huku akijua anasababisha usumbufu usio wa lazima, linamfanya asiwe ‘presidential material’.

Nne, kuhusu Nyalandu; huyu kalelewa na CCM, kawa waziri wa muda mrefu na hana ushawishi wa kutosha kwenye level ya urais Tanzania bara.

Tano, Kuhusu Zitto; kwa sababu mbalimbali kiwango chake cha kuaminika kimepungua kwa sababu mbalimbali. Hivyo, akigombea urais hawezi kupata hata 10% ya kura. Aidha, hataungwa mkono na CHADEMA, na ndani ya ACT hakuna mtu mwingine ambaye ni ‘presidential material’ kwa Tanzania bara anayeweza kuwa na ushawishi zaidi ya Zitto.

Kwa nini Membe?

Kwa sababu ukimuacha Lisu, upande wa vyama vya upinzani hakuna mtu mwingine Tanzania bara mwenye haiba ya urais inayomkaribia Membe. Kwa mantiki hiyo, ijapokuwa Membe hatamshinda Rais Magufuli; angalau atasaidia CHADEMA kujipatia % fulani la kura ambayo itasaidia waendelee kupata ruzuku japo kidogo na uwepo wao uendelee kuonekana.Ikombukwe hapo tayari watakuwa washapoteza viti karibu vyote vya ubunge!

Ingawa ni kweli kwamba Membe bado anaiwazia CCM, lakini ni kweli pia kwamba kwa sasa hana uwezekano tena wa kugombea kupitia CCM. Sasa kwa kuwa tatizo la Tanzania sio CCM kama chama bali mtu mmoja mmoja, CHADEMA wakimtumia Membe ili awabusti sio jambo baya kwa kuwa ana haiba chanya zaidi ukilinganisha na wengine wengi waliotajwa hapo juu.

Kwa upande wa ACT, viti kadhaa watakavyopata Zbar, vitawasaidia kuendelea kuonekana na kupata ka - ruzuku kidogo katakako wasaidia ku ‘savaivu’.

Najua wapo watakaobisha, kutukana, na kubeza ushauri huu, ila ushauri huu unazingatia zaidi ‘facts’ ziwe za kuvutia au za kuudhi. Ni hiari ya wahusika kuufuata na wapate namna yenye uafadhali ya kuendelea ku ‘savaivu’ kwenye kipindi cha 2021 -2025, au wapuuze halafu wawe kama TLP, NLD n.k Kama watapuuza na kufikia hatua hiyo, CCM itakosa pakujitizama hiyo nayo utendaji wake unaweza kuathirika kwa namna hasi na kwa kuwa kitakuwa ndicho chama kinachounda serikali, taifa nalo linaweza kukabiliwa na changamoto kadha wa kadha ambazo pengine zingeepukika kwa kufuata ushauri huu.

Kuna wazo kwamba CCM inaweza ikaamua kuwaachia vyama vya upinzani viti kadhaa kwa makusudi ili viendelee kuwepo. Hiyo ni kweli lakini sishauri vyama vya upinzani kutegemea favor kutoka CCM. Wanaweza wasipewe hiyo favor na ikawagharimu sana.

Mtu anaweza kusema kwa nini vyama vya upinzani visipewe ushauri utakaowawezesha kushinda? Jibu ni kwamba ushauri huo walishapewa sana na kuelezwa kwamba pamoja na changamoto za nje zinazowakabili, changamoto kubwa zinazowakwamisha ziko ndani ya vyama vyao wenyewe. Kwa bahati mbaya hilo hawajaliamini hadi sasa na kwa kuwa hawajaliamini na wanadhani changamoto zinazowakabili ni ‘100% external’; hawajachukua hatua na muda uliobaki ni mfupi mno ambao hauwezi kuwatosha tena. Ndio maana ushauri unaowezekana kwa sasa anagalau ni ule wa kuwawezesha waendelee ku ‘savaivu’ lakini sio kushinda.

Tunawashukuru sana kwa kuelewa.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kwa wapenda demokrasia, udumavu au kufa kwa vyama vya siasa sio jambo la kufurahisha, kwa sababu hilo likitokea litapelekea siasa kupoa sana.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,645
2,000
Kuhusu Mbowe, je ikitolewa CCTV Camera ikaonesha tofauti na unavyofikiri utaendelea kuwa huu nsimamo wako?

Msigwa kukosea akaomba samahani sio dhambi, ni nani asiekosea huko ulipo?

Kuliko Membe apewe hiyo nafasi bora apewe yeyote aliejitokeza kuchukua form Chadema.
 
Fernando Jr

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
2,402
2,000
Ushauri wako mwana ccm umekaa ki ccm ccm! Yaani CHADEMA imsimamishe Membe ambaye yupo ccm!? Au unafikiri CDM ni kama wale TLP sijui NLD waliotangaza kumpitisha stone awe mgombea wao?

Unamkandia Nyalandu kuwa kalelewa ccm huku ukimpigia chapuo Membe ambaye si tu kalelewa ccm, bali bado yupo ccm!
 
Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
2,204
2,000
Kuhusu Mbowe, je ikitolewa CCTV Camera ikaonesha tofauti na unavyofikiri utaendelea kuwa huu nsimamo wako?

Msigwa kukosea akaomba samahani sio dhambi, ni nani asiekosea huko ulipo?

Kuliko Membe apewe hiyo nafasi bora apewe yeyote aliejitokeza kuchukua form Chadema.
Kama nakuona jinsi ulivyokua umeng'ata mdomo wa chini ulipokua una komenti
 
Mshumaa_Tz

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
684
1,000
Chadema sio wapumbavu kama ccm ,we subiri uchaguzi ufike ndo utajuwa , labda mgome kuwatangaza wabunge wetu na madiwani, upuuzi wa ccm wanazani kura zinapigwa na Yesu muuaji tu.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Msigwa kukosea akaomba samahani sio dhambi, ni nani asiekosea huko ulipo?
Kuomba msamaha ni kitu kizuri sana na yeye kafanya kitu kizuri sana ambacho ni cha mfano. Lakini kwenye mambo ya msingi, tunatakiwa kwenda hatua moja mbele kutoka kuangalia tukio 'event' hadi kuangalia 'essence'.

Mtu unaweza kujiuliza umempakazia mtu jambo kubwa sana la kumchafua, unajua umefanya hivyo makusudi na jambo hilo linamuumiza lakini unasisitiza kuwa na ushahidi unao, mwaka mzima unaisha msimamo wako ni huo huo, anakuambia anaenda mahakamani bado msimamo wako ni huo huo, anafungua kesi unatuma mawakili kukutetea huku ukijua unawatuma wakatete jambo la uongo na dhuluma, anakushinda unapigwa faini , kisha ndio unaungama. Hii 'essence' yake nini? Je, mtu akasema huyu akiwa rais anaweza kupakazia watu mambo ya hatari halafu akishastaafu ndio anaungama, mtu huyo atakuwa kakosea?

Nilifuatilia mjadala wa Msigwa na Lema mwezi uliopita ambapo Msigwa alitoa hoja ya msingi sana. Alisema 'Cheo hakimfanyi mtu awe na akili au tabia njema Zaidi bali humfunua jinsi alivyo' na hivyo kusisitiza kwamba ipo haja ya kujenga 'character ' za viongozi watarajiwa wangali wadogo. Sasa kwa kuwa hoja hii ya Msigwa ni ya kweli, je! mtu akihofia kwamba pengine hapo msigwa alikuwa hajajifunua vizuri na akipata cheo kikubwa atajifunua Zaidi? hiyo hoja majibu yake yatakuwa yapi?
 
Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
6,967
2,000
Ushauri ungetolewa kuwe na tume huru ya uchaguzi tu, Magu atashindwa hata na mwanasiasa yeyote asie na jina wa upinzani.
Magu, hajui kujieleza, hana busara ya uongozi, mipango yake ya uchumi imeshindwa vibaya, ubabe usio na akili n.k
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,645
2,000
Kuomba msamaha ni kitu kizuri sana na yeye kafanya kitu kizuri sana ambacho ni cha mfano. Lakini kwenye mambo ya msingi, tunatakiwa kwenda hatua moja mbele kutoka kuangalia tukio 'event' hadi kuangalia 'essence'.

Mtu unaweza kujiuliza umempakazia mtu jambo kubwa sana la kumchafua, unajua umefanya hivyo makusudi na jambo hilo linamuumiza lakini unasisitiza kuwa na ushahidi unao, mwaka mzima unaisha msimamo wako ni huo huo, anakuambia anaenda mahakamani bado msimamo wako ni huo huo, anafungua kesi unatuma mawakili kukutetea huku ukijua unawatuma wakatete jambo la uongo na dhuluma, anakushinda unapigwa faini , kisha ndio unaungama. Hii 'essence' yake nini? Je, mtu akasema huyu akiwa rais anaweza kupakazia watu mambo ya hatari halafu akishastaafu ndio anaungama, mtu huyo atakuwa kakosea?

Nilifuatilia mjadala wa Msigwa na Lema mwezi uliopita ambapo Msigwa alitoa hoja ya msingi sana. Alisema 'Cheo hakimfanyi mtu awe na akili au tabia njema Zaidi bali humfunua jinsi alivyo' na hivyo kusisitiza kwamba ipo haja ya kujenga 'character ' za viongozi watarajiwa wangali wadogo. Sasa kwa kuwa hoja hii ya Msigwa ni ya kweli, je! mtu akihofia kwamba pengine hapo msigwa alikuwa hajajifunua vizuri na akipata cheo kikubwa atajifunua Zaidi? hiyo hoja majibu yake yatakuwa yapi?
Umeandika vizuri nimekuelewa but nikitazama hoja ulizotumia kuwakataa hao wagombea naziona nyingi ni 50%, zinaweza kubaki hivyo hivyo au isiwe.

Hiyo hoja ya Msigwa ni kwenda nayo taratibu tu, naamini hata yeye binafsi alikuwa na uhakika ushahidi aliokuwa nao kuhusu issue ya Kinana ungetosha kuishawishi mahakama kuamini hoja yake, mpaka alipokuja kuwa proved wrong na mahakama, na hili hutokea kwa wote wanaokuwa na kesi mahakamani.

Hivyo usimlaumu kwasababu alishindwa kesi, hilo ni jambo la kawaida kutokea wanaposhindana wawili mahakamani, vinginevyo uwe na hakika 100% kwamba Msigwa alijua anamchafua Kinana makusudi bila kuwa na ushahidi wa kutosha, something which I doubt on my part.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Ushauri wako mwana ccm umekaa ki ccm ccm! Yaani CHADEMA imsimamishe Membe ambaye yupo ccm!? Au unafikiri CDM ni kama wale TLP sijui NLD waliotangaza kumpitisha stone awe mgombea wao?

Unamkandia Nyalandu kuwa kalelewa ccm huku ukimpigia chapuo Membe ambaye si tu kalelewa ccm, bali bado yupo ccm!
Lakini ukumbuke kwamba walimsimamisha Lowasa ambaye alikuwa CCM. au hilo haulijui au umesahau? vile vile kuhusu Nyalandu, Nyalandu kulelewa na CCM sio jambo baya, ni jambo zuri kabisa kwa sababu pia hali halisi inaonesha haiba ya viongozi waliolelewa ndani ya CCM ina uafadhali mkubwa kuliko wale waliolelewa nje ya CCM. Ninachosema ni kwamba Nyalandu ushawishi wake kwa nafasi ya urais si mkubwa.

Kuhusu CCM, kama unanifuatilia toka zamani, msimamo wangu kuhusu CCM ni kuwa CCM sio tatizo na haijawahi kuwa tatizo. Tatizo ni baadhi ya mtu mmoja mmoja . Na matatizo hayo ya mtu mmoja mmoja ni matatizo ambayo yako kwenye jamii yetu. Sasa kwa kuwa vyama vya siasa vinaundwa na wanajamii na CCM ni chama cha siasa kinachoundwa na watu kutoka kwenye jamii hii hii, lazima wanachama watakuwa ni reflections ya jamii husika isipokuwa kama kitakuwa na mikakati ya kuwajengea uwezo wa kiuongozi na kifikra wanachama wake.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,775
2,000
Kwani hilo likifanyika, itakuwa ndio mara ya kwanza? anyway ni ushauri tu, ushauri sio amri. Na sisi wengine ni vidagaa tu, kwa hiyo wakati mwingine mawazo yetu ni kama mapovu ziwani.
Hapana Mkuu Aziz Mussa, nimesoma kwa makini hoja zako zote ziko very logical isipokuwa hili la Membe.
Membe ni mwana CCM, japo ilitamkwa kuwa emefukuzwa ila mpaka kesho hajapewa barua rasmi ya kufukuzwa na hajatamka kuacha CCM, sasa why wapinzani wawaze kusimamisha mtu ambae wala sio mwanachama wao?.
P
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Umeandika vizuri nimekuelewa but nikitazama hoja ulizotumia kuwakataa hao wagombea naziona nyingi ni 50%, zinaweza kubaki hivyo hivyo au isiwe.

Hiyo hoja ya Msigwa ni kwenda nayo taratibu tu, naamini hata yeye binafsi alikuwa na uhakika ushahidi aliokuwa nao kuhusu issue ya Kinana ungetosha kuishawishi mahakama kuamini hoja yake, mpaka alipokuja kuwa proved wrong na mahakama, na hili hutokea kwa wote wanaokuwa na kesi mahakamani.

Hivyo usimlaumu kwasababu alishindwa kesi, hilo ni jambo la kawaida kutokea wanaposhindana wawili mahakamani, vinhinevyo uwe na hakika 100% kwamba Msigwa alijua anamchafua Kinana makusudi bila kuwa na ushahidi wa kutosha, something which I doubt on my part.
Wewe jamaa nakupendea kitu kimoja. Unajadili hoja kwa hoja na bila matusi. Hiyo ni 'Strength ' moja muhimu sana kwako na dalili ya kuonesha 'maturity' kwa upande wako. Hongera kwa hilo na keep it up.

Tukirudi kwenye hoja yako, ukumbuke mhusika mwenyewe anakiri kuwa alimsingizia. sijui unaelewa maana ya kumsingizia mtu? hapo sio suala ya ushahidi sasa, hapo maana yake alifanya hivyo makusudi kwa malengo ambayo aliyajua yeye. Kwa hiyo hilo ni kosa la wazi sana, lakini kufanya kosa hilo sio ishu maana sote tunakosea, bali kukawia kuomba radhi kwa miaka hadi hatua zote hizo huku akifahamu anamuumiza mtu mwingine, hiyo inaogopesha kidogo. Na wakati mwingine kukosa haiba ya kuwa kiongozi wa level flani, haimaanishi kuwa mtu husika hufai kabisa, bali unafaa lakini kwa level nyingine .

Kwa mfano, kuna watu kwa personalities zao, sio kwamba ni watu wabaya kakini hawafai kuwa viongozi wenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya mwisho kwa sababu kwa mfano unaweza kukuta wana 'emotional swinging' yaani wana hisia kali sana juu ya mambo.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,347
2,000
Eti Lissu atashindwa kurudi Tz hivi kocha wa Yanga alikuwa wapi mwezi uliopita na sasahivi yuko wapi?

Naona unampigia chapuo mwana kitengo mwenzio ili aje kuua na kuuzika upinzani ili muendelee kula mvinyo kwa kumaliza kazi yenu. vipi usharudi Tanzania?
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,645
2,000
Wewe jamaa nakupendea kitu kimoja. Unajadili hoja kwa hoja na bila matusi. Hiyo ni 'Strength ' moja muhimu sana kwako na dalili ya kuonesha 'maturity' kwa upande wako. Hongera kwa hilo na keep it up.

Tukirudi kwenye hoja yako, ukumbuke mhusika mwenyewe anakiri kuwa alimsingizia. sijui unaelewa maana ya kumsingizia mtu? hapo sio suala ya ushahidi sasa, hapo maana yake alifanya hivyo makusudi kwa malengo ambayo aliyajua yeye. Kwa hiyo hilo ni kosa la wazi sana, lakini kufanya kosa hilo sio ishu maana sote tunakosea, bali kukawia kuomba radhi kwa miaka hadi hatua zote hizo huku akifahamu anamuumiza mtu mwingine, hiyo inaogopesha kidogo. Na wakati mwingine kukosa haiba ya kuwa kiongozi wa level flani, haimaanishi kuwa mtu husika hufai kabisa, bali unafaa lakini kwa level nyingine .

Kwa mfano, kuna watu kwa personalities zao, sio kwamba ni watu wabaya kakini hawafai kuwa viongozi wenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya mwisho kwa sababu kwa mfano unaweza kukuta wana 'emotional swinging' yaani wana hisia kali sana juu ya mambo.
Hapa cha muhimu tujue kitu kimoja, huko "kumsingizia" alikutambua muda gani, kabla ya hukumu au baada ya hukumu kutolewa mahakamani, kama ni baada ya kutolewa hukumu mahakamani basi inawezekana ndio maana akatambua alikosea na ndio akatumia huo msemo kumsingizia, but kumsingizia huku kutakuwa na maana zaidi kama alijua toka mwanzo kuwa anachosema alikuwa anakosea, lakini akaendelea kuwa na msimamo wake.

Kuthibitisha hili kwa upande wetu itakuwa ngumu, ukweli anaujua mwenyewe Msigwa.

Lakini pia, hivi tukianza kuwahukumu wagombea kwa makosa yao waliyowahi kuyafanya before, hivi kuna atakaebaki salama kweli kwenye siasa?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom