Katika hati ya madai amenukuu baadhi ya kauli za Msigwa, ikiwemo "Kinana (naomba waandishi wa habari mnisikie na nyie Usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia Watanzania waiamini CCM. Kinana mikono yake si misafi."
"Hata kwenye Nassaco, Shirika la Meli Tanzania kuna harufu ya ufisadi ndani yake; ajibu hoja...Kinana meli zake ndizo zinazohusika kubeba pembe za ndovu nchini. hajajibu hoja hizo! Kwa siku nchi hii tembo 67 wanauawa. Hao ndio wanaokifadhili Chama Cha Mapinduzi, halafu wanakuja eti kuwashawishi Watanzania muwasikilize na kwamba Chama Cha Mapinduzi eti ni kizuri."
".Haya mambo ninayoongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangili ni organized Crime. Ni mtandao wa Kimafia, uko duniani kote, unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea..."