Kinana aingia wilayani mpya ya Mkalama, ahutubia umati wa watu wa kata za Nkungi na Nduguti.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nkungi, wilayani Mkalama wakati wa mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kinana akisoma majina ya vijiji lukuki vitakavyopata umeme katika Wilaya mpya ya Mkalama, Kata ya Nduguti,Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nkungi, wilayani Mkalama

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nkungi, Mkalama.

Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Singida, Martha Mlata pia alipata wasaa wa kuwahutubia wananchi.

Katibu Mkuu akihutubia kikao cha wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Wilaya ya Mkalama.

Kinana akipata chai nyumbani kwa Balozi Fatuma Kasimu katika Kata ya Gumanga alipoenda kumtembelea na kuongea na wanachama wake wa shina namba 5.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone na Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone (kulia), wakitoka kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Simiti linalounganisha wilaya za Meatu mkoani Simiyu na Mkalama, Singida
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tume imetoa sababu mbili kubwa za kupendekeza muundo wa Serikali tatu. Sababu ya kwanza ni kwamba ndiyo matakwa ya Watanzania wengi kote Zanzibar na Tanzania Bara. Inaeleza kuwa idadi kubwa ya Watanzania waliotoa maoni, yaani asilimia 60.2 wa kutoka Zanzibar wanaunga mkono muundo wa Serikali ya Mkataba, na asilimia 61.3 wa kutoka Tanzania Bara wanaunga mkono muundo wa Serikali tatu. Sababu ya pili ni kwamba muundo huo unatoa majawabu ya uhakika na endelevu kwa changamoto za muundo wa sasa wa Serikali mbili zinazonung’unikiwa na watu wa pande zetu mbili za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Sababu hizi mbili kuu zilizotolewa na Tume zimezua mjadala mkali katika jamii. Wapo wanaokubaliana na Tume na wapo wasiokubaliana nayo. Wapo wanaosema Tume imesema kweli kwamba Watanzania wengi wanaunga mkono muundo wa Serikali tatu, hivyo muundo wa Serikali tatu hauepukiki. Ndiyo matakwa ya wengi hivyo msemo wa Kiswahili usemao wengi wape uheshimiwe.

Lakini wapo wanaodai kuwa takwimu za Tume hazionyeshi ukweli huo. Wanasema kuwa taarifa ya Tume imeonesha kuwa Watanzania waliotoa maoni yao kwa Tume kwa mdomo na maandishi walikuwa 351,664. Kati yao ni wananchi 47,820 au sawa na asilimia 13.6 ndiyo waliokerwa na muundo wa Muungano hivyo wakauzungumzia. Wananchi 303,844 au sawa na asilimia 86.4 muundo wa Muungano kwao halikuwa tatizo, ndiyo maana hawakuuzungumzia kabisa. Wanahoji kuwa iweje leo asilimia 13.6 ya Watanzania wote waliotoa maoni wageuke kuwa ndiyo Watanzania walio wengi!

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Wanasema pia, kwamba mbona Taarifa ya Tume yenyewe, kuhusu takwimu (uk. 66 na 67), inaonesha kwamba kati ya hao watu 47,820 waliotoa maoni kuhusu Muungano, ni watu 17,280 tu ambao ni sawa na asilimia 37.2 ndiyo waliotaka muundo wa Serikali tatu, asilimia 29.8 walitaka Serikali mbili, asilimia 25.3 walipendekeza Serikali ya Mkataba na asilimia 7.7 walipendekeza Serikali moja. Hii hoja ya Watanzania wengi kutaka Serikali tatu msingi wake upi?

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Takwimu za Tume (uk. 57) zinaonyesha, vilevile kuwa Tume ilipokea maoni 772,211. Kati ya hayo asilimia 10.4 tu ndiyo yaliyozungumzia muundo wa Muungano na asilimia 88.6 hayakuzungumzia Muungano bali mambo mengine. Hivyo basi wanahoji pia kwamba kama muundo wa Muungano ungekuwa ni jambo linalowakera Watanzania wengi, lingedhihirika kwenye idadi ya watu waliotoa maoni na kwenye idadi ya maoni yaliyotolewa. Yote hayo hayakujitokeza. Waliouzungumzia Muungano walikuwa asilimia 13.6 tu ya watu wote waliotoa maoni na maoni yanayohusu Muungano yalikuwa asilimia 10.4 ya maoni yote. Hivyo basi, wanauliza “usahihi wa hoja ya Watanzania wengi kutaka Serikali tatu uko wapi?”-RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, 21 MACHI, 2014, DODOMA
 

Deshmo

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
4,777
2,000
Sema kinana alikua na kikao cha familia, vipi salome mwambu alizomewa au? Tunawasubiria Mbulu tulikomzomea Mwenyekiti wa ccm taifa
 

Deshmo

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
4,777
2,000
Sema kinana alikua na kikao cha familia, vipi salome mwambu alizomewa au? Tunawasubiria Mbulu tar 28 tulikomzomea Mwenyekiti wa ccm taifa
 

iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
0
Hili la muungano serekali mbili bado wanazingumzia naona kama ccm imechemka kwenye hili.. wao waendelee kubeba matofali ya oungo na kweli na kuendelea kunywa gongo na kula kwa mamantilie tu..maana nndo mbinu zinaenda ukingoni hivyo..usisahau ukawa inapita kufuta kila kitu..
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Ukawa hakikisheni mnakanyaga sehemu zote ambazo interahamwe wanapita! Wanapita kushangilia kupinduliwa kwa rasimu ya warioba bungeni...
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Ukawa hakikisheni mnakanyaga sehemu zote ambazo interahamwe wanapita! Wanapita kushangilia kupinduliwa kwa rasimu ya warioba bungeni...

Ndugu, Kama hawa ni Interahamwe basi hao wengine ni Boko Haram.

Hicho kikundi kinachojiita UKAWA hakiwezi kupambana na nguvu na uwezo kifikra wa Mzee Kinana.

Huwaoni hawa wanaojiita UKAWA kwa sasa ajenda kuu ni kulitaja taja jina la Mzee Kinana. Jina la Mzee Kimana linatajwa zaidi ya jina la Katiba ambalo wanadai ni msingi wa UKAWA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom