Kinamama hoyee! Ewe mama, unataka kuwa Askofu? Ruksa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Wanawake wanaruhusiwa kuwa Maaskofu(Waangalizi).
Ushahidi huu hapa:
1 Tim 3:1-10
"Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema."

Kama una hoja za kupinga mwanamke kushika wadhifa huo wa juu, yaani kama unadai mwanamke hafai kuwa Askofu, tuanzie kwanza hapo kwenye kifungu hicho: mwanamke sio mtu? Kifungu hicho kinasema mtu akitaka kazi ya Askofu...

Please, hoja zote ziambatane na vifungu vya Biblia, sio mapokeo. Biblia ndio taa yetu.
 
kumbe ww n ke ngoja niandae posa sasa
 
Attachments

  • Screenshot_20250426-101114_Biblia.jpg
    Screenshot_20250426-101114_Biblia.jpg
    160.7 KB · Views: 9
Hawa TEC wanapingana na TIMOTHEO?

Au Wana mamlaka zingine wanazo zitii?

Au Kuna kitabu kingine katika Bible wanakitumia kujenga hoja yao?
 
Wanawake wanaruhusiwa kuwa Maaskofu(Waangalizi).
Ushahidi huu hapa:
1 Tim 3:1-10
"Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema."

Kama una hoja za kupinga mwanamke kushika wadhifa huo wa juu, yaani kama unadai mwanamke hafai kuwa Askofu, tuanzie kwanza hapo kwenye kifungu hicho: mwanamke sio mtu? Kifungu hicho kinasema mtu akitaka kazi ya Askofu...

Please, hoja zote ziambatane na vifungu vya Biblia, sio mapokeo. Biblia ndio taa yetu.
1Timotheo 3:2
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja,

Sasa huyo mwanamke unayetaka awe askofu ataiweza hiyo sifa ya kuwa MUME WA MKE MMOJA?
 
Kuna Lesbian siku hizi
 
Mimi siwezi sali kwenye kanisa analoongoza mwanamke

Ndo yale Yale shalom mama, shalom baby girl 😍 😂 Depal afu nimemuona maa mchungaji ana mkia wa haja na nyonyo la haja duuh

Ila zile shuhuda hapana , niacheni nisali chini ya mti au nisilimu tuu Malaria 2
 
Ila zile shuhuda hapana , niacheni nisali chini ya mti au nisilimu tuu malaria
 
Wanawake wanaruhusiwa kuwa Maaskofu(Waangalizi).
Ushahidi huu hapa:
1 Tim 3:1-10
"Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema."

Kama una hoja za kupinga mwanamke kushika wadhifa huo wa juu, yaani kama unadai mwanamke hafai kuwa Askofu, tuanzie kwanza hapo kwenye kifungu hicho: mwanamke sio mtu? Kifungu hicho kinasema mtu akitaka kazi ya Askofu...

Please, hoja zote ziambatane na vifungu vya Biblia, sio mapokeo. Biblia ndio taa yetu.
Tunakoelekea mtahalalisha ndoa za mashoga Kwa vifungu vya biblia, shetani ametawala Kila Kona maaaaamae
 
Mimi siwezi sali kwenye kanisa analoongoza mwanamke

Ndo yale Yale shalom mama, shalom baby girl 😍 😂 Depal afu nimemuona maa mchungaji ana mkia wa haja na nyonyo la haja duuh

Ila zile shuhuda hapana , niacheni nisali chini ya mti au nisilimu tuu Malaria 2
Shalom kaka Monetary 🤣🤣

Mama mchungaji amejaaliwa mema mengi 😂😂 yale Makanisa ya vile achia wanawake.. sie twende zetu Alhamis kuabudu Ekaristi Takatifu.
 
Tuheshimiane bwana wewe,hakukua na mtume mwanamke wala nabii
 
Shalom kaka Monetary 🤣🤣

Mama mchungaji amejaaliwa mema mengi 😂😂 yale Makanisa ya vile achia wanawake.. sie twende zetu Alhamis kuabudu Ekaristi Takatifu.
Shalom darling sis, you look beautiful, sisi 😍😂

Kwakweli mm nasemaga tujifunze kujiombea wenyewe, tujifunze kuwa na subra na uvumilivu basi,

Hakika ukiweka imani kwa Mungu hakuachi, hasa ekaristi napenda sana sana siwezi kuelezea Ila ni Ibada ambayo ina majibu
 
Wanawake wanaruhusiwa kuwa Maaskofu(Waangalizi).
Ushahidi huu hapa:
1 Tim 3:1-10
"Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema."

Kama una hoja za kupinga mwanamke kushika wadhifa huo wa juu, yaani kama unadai mwanamke hafai kuwa Askofu, tuanzie kwanza hapo kwenye kifungu hicho: mwanamke sio mtu? Kifungu hicho kinasema mtu akitaka kazi ya Askofu...

Please, hoja zote ziambatane na vifungu vya Biblia, sio mapokeo. Biblia ndio taa yetu.
Wewe umemsikia nani au imeandikwa wapi kwamba wanawake wasiwe maaskofu?
Maaskofu wanawake wapo mbona unajihami sasa?
 
Hawa TEC wanapingana na TIMOTHEO?

Au Wana mamlaka zingine wanazo zitii?

Au Kuna kitabu kingine katika Bible wanakitumia kujenga hoja yao?
TEC wanahusikaje hapa? Timotheo keshatoa ruksa wewe nenda kawe askofu
Wakatoliki nao wana andiko lao toka kwa paulo. Usiwapangie
 
1Timotheo 3:2
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja,

Sasa huyo mwanamke unayetaka awe askofu ataiweza hiyo sifa ya kuwa MUME WA MKE MMOJA?
Ni kweli katika 1 Timotheo 3:2-7 imeandikwa kwamba Askofu awe “mume wa mke mmoja”

Kwenye andiko hilo, kuna mambo mawili muhimu ya kuelewa:

Kwanza, mtazamo wa wakati ule (Context ya kitamaduni)
Katika utamaduni wa Wayahudi na Warumi karne ya kwanza, wanaume ndio waliokuwa wakiongoza nyumba zao na jamii. Hivyo, Paulo aliandika kwa muktadha wa wakati ule — ndivyo jinsi jamii ile ilivyotarajia.

Paulo hakusema kwamba hiyo ni sheria ya milele isiyobadilika. Hakuandika kuwa "wanawake hawaruhusiwi kuwa maaskofu." Alikuwa anatoa mwongozo tu wa jinsi mtu aliyetaka uaskofu katika mazingira yale alivyopaswa kuwa.

Leo hii katika jamii nyingi, wanawake wanakubaliwa kushika nyazifa za juu za uongozi. Hivyo Paulo angekuwa anazungumza na jamii za leo, zinazomruhusu mwanamke kuwa kiongozi wa juu, angeweza pia kusema askofu awe mke wa mume mmoja.

Kama hujaridhika na hoja hiyo, hebu tuangalie hoja ya pili:

Katika lugha ya Kigiriki(lugha ya mwanzo iliyotumika kuandika Agano Jipya), "mume wa mke mmoja" ni tafsiri ya maneno "aner mias gynaikos" — maana yake ni mtu asiye mzinzi, mtu mwaminifu katika ndoa yake.

Kwa tafsiri hiyo ni wazi hata mwanamke anaweza kuwa askofu mradi tu awe na mume mmoja na pia azingatie sifa zote zilizoainishwa katika andiko hilo:
"asiye na lawama, awe mwenye kiasi, nidhamu na utaratibu; ni lazima awe mkarimu na anayeweza kufundisha; asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha; anapaswa awe mtu awezaye kuongoza vema nyumba yake, na kuwafanya watoto wake wawe watii kwa heshima yote...Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi."

Sifa zote hizo, mwanamke anaweza kuwa nazo.

Bado tu unapinga kuwa mwanamke hawezi kuwa Askofu? Leta hoja mpya
 
Back
Top Bottom