Kinachowatisha CCM kwenye No Reforms no Election

Kinachowatisha CCM kwenye No Reforms no Election

Hoja wanayo, nimeongelea Wasiwasi wa ccm kwa hoja ya CHADEMA. Ikifanikiwa wataiba nini?
Kabisa, hofu ya ccm ni wapiga kura kuwa wachache, maana ile siri ya kuwa ina wapiga kura wachache , na huwa wanaiba za wengine itafahamika. Hawana hofu nyingine maana nguzo yao kuu ambayo ni vyombo vya dola viko upande wao, na tume ya uchaguzi inatii watakacho.
 
THey dont care
Kweli they don't care maana wanachojali ni vyeo, lakini wanakaribisha hatari ya mapinduzi, hasa ya kijeshi kwani wataona hata walioko madarakani hawana uhalali wa umma.
 
Hahahahaaha?
Mtaanzosha threads hata bilioni Moja Hadi uchaguzi ufike mkiongea yaleyale lakini Iko hivi;
Uchaguzi utafanyika, kwa amani na mama Samia ushindi wa 98%+ unamsubiri.
Screenshot_20250405_004437_X.jpg

Kwa mfumo huu hata 100% kinyume chake hata 30% hapati.
 
wakipiga kura watu 10 bado atapata kura milioni 70
Hatapata hizo kura, bali watatangazwa washindi kwa kura hizo. Chaguzo zote zilizifanyika chini ya utawala wa Magufuli zilikithiri kwenye upikaji wa idadi ya wapiga kura, na kansa ile naona imebebwa na utawala huu wa Samia.
 
Usiposhiriki NCCR,TLP ACT na wengine wakishiriki na kupata viti 20 unafikiri CCM inaona kuna shida yoyote.

CCM inaweza kuamua kuwaachia viti 30 kwa makubaliano maalum, wapate ruzuku kiasi flani, wawe viongozi wa kamati waseme uchaguzi ulikuwa wa wazi, huru na wa haki unafikiri Chadema haitapata sauti ikiwa nje ya mchakato wote na nje ya bunge.

Hata kama CDM haitapata Urais, itaibiwa wabunge wengi, bado itapata kura kwa mamilioni, 3- 5milioni. Hiyo ni nguvu tosha kuliko kuwa na zero,nil, sifuri. Kisha hukushiriki.
Mnajiona mna akili kabisa mnavyoandika ufedhuli wenu mnaofanyaga ili kuharibu haki za wananchi kupiga kura.

Maneno yenu humu yanadhihirisha kuwa nchi hii haina chaguzi huru na haki na kwa sababu nchi hii ina watu waelewa na sio wajinga basi eleweni lazima Taifa liponywe na siasa zenu hizi za kilaghai.

Mna leta masikhara sana kwenye haki za watu.

No Reform No Election lazima ifanikiwe. Tupo hapa.
 
Hatapata hizo kura, bali watatangazwa washindi kwa kura hizo. Chaguzo zote zilizifanyika chini ya utawala wa Magufuli zilikithiri kwenye upikaji wa idadi ya wapiga kura, na kansa ile naona imebebwa na utawala huu wa Samia.
huu ni wizi kama wizi mwingine
 
CCM wanafahamu kwamba huo wito ukiitikiwa na wananchi, Idadi ya watakao jitokeza kupiga kura itakuwa ni sawa na zero, au Negligible kabisa, hivyo itawawaacha uchi kwa matokeo wanayopika kila siku.

Kwa kufahamu hilo wana itaka CHADEMA ishiriki uchaguzi ili kutimiza ndoto za wizi wao.

Nami naamini CHADEMA ikifanikiwa kwenye hili, na wananchi wasijitokeze kupiga kura CCM itakosa legitimacy ya kuongoza.

Hizi tambo za CCM ni kwa sababu wanapojitokeza wana Chadema kwa wingi kwa nia ya kuitoa CCM madarakani, wao wanutumia mwanya huo kuchakachua kura za CHADEMA na kuwa za CCM na za CCM kuwa za CHADEMA.

Binafsi naona CHADEMA wakaze kabisa na wasiseme zile kauli tata, kama "Hatutasusia uchaguzi bali tutaamasisha watu wasiende kupiga kura" badala yake waseme "Hatutashiriki Uchaguzi kama hakuna mabadiriko ya sheria na taratibu za uchaguzi".
Kwenye nchi nyingi za Kidemokrasia wapiga kura wachache ndio hujitokeza kupiga kura na ndio maana hakuna kipengele cha kusema wapiga kura wakiwa wachache basi huo uchaguzi sio huru na haki.

Binafsi, naomba sana Chadema wasuse kabisa kupiga kura na wafuasi wao poa wasuse ili Uchaguzi Mkuu uende vizuri!
 
Si kweli maana wapiga kura walikuwa wengi siku ya nyuma, ila sasa hawapo wengi maana hawako tayari tena kupoteza muda wao kwenye mistari ya kura kisha, ccm wajitangaze washindi wakati hawawapi kura. Mara nyingi hali hii ya kutoheshimiwa kwa box la kura hupelekea machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi.
 
Nami naamini CHADEMA ikifanikiwa kwenye hili, na wananchi wasijitokeze kupiga kura CCM itakosa legitimacy ya kuongoza.
Kuna vyama matawi ya ccm yatatoa legitimacy ya uchaguzi maana wataingia kwenye uchaguzi.....

what next? watanzania wataweza kuingia barabarani kama Uturuki/Kenya "kuvunja" Vituo vya kupigia kura? Wataweza kuhimili risasi? watapanda juu ya maiti mbele yao kusonga mbele kuwakabiri polisi??
 
analysis yako sijui umekaa unachapa uzi eneo gan au upo under influence ya kinywaj gan to say least. Ccm ina wanachama hai milion 25. wenye kad.bado wapenz washabiki. sasa unaposema watakosa kura unamaanisha nini?
 
Si kweli maana wapiga kura walikuwa wengi siku ya nyuma, ila sasa hawapo wengi maana hawako tayari tena kupoteza muda wao kwenye mistari ya kura kisha, ccm wajitangaze washindi wakati hawawapi kura. Mara nyingi hali hii ya kutoheshimiwa kwa box la kura hupelekea machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi.
Turn out ya wapiga kura wa Marekani mwaka jana ilikuwa chini ya 65%. Tena ilikuwa chini zaidi ya miaka minne iliyopita kwani ilikuwa asilimia 66%. Hapo unasemaje?
 
Kwa kufahamu hilo wana itaka CHADEMA ishiriki uchaguzi ili kutimiza ndoto za wizi wao.

Nami naamini CHADEMA ikifanikiwa kwenye hili, na wananchi wasijitokeze kupiga kura CCM itakosa legitimacy ya kuongoza.
Kwa miaka mingi wananchi wamekuwa hawapigi kura kwa sababu hawaoni umuhumu ikiwa mshindi anajulikana ni wa kuchonga. Kimsingi tuliwachelewesha wananchi kwenye hili.
 
Turn out ya wapiga kura wa Marekani mwaka jana ilikuwa chini ya 65%. Tena ilikuwa chini zaidi ya miaka minne iliyopita kwani ilikuwa asilimia 66%. Hapo unasemaje?
Miaka mingine huwa inakuwa % ngapi? Na huko wako idadi hiyo maana hawana imani na uchaguzi?
 
Fake news
analysis yako sijui umekaa unachapa uzi eneo gan au upo under influence ya kinywaj gan to say least. Ccm ina wanachama hai milion 25. wenye kad.bado wapenz washabiki. sasa unaposema watakosa kura unamaanisha nini?
 
Miaka mingine huwa inakuwa % ngapi? Na huko wako idadi hiyo maana hawana imani na uchaguzi?
Ahahahahaha! Kwetu sisi mwaka 2020 wapiga kura walikuwa milioni 15 na pointi sawa na asilimia 50.72% ya waliojiandikisha. Marekani asilimia 65%. Kwa wewe mwenye akili nyingi, Uchaguzi wa Marekani ni wa kidemokrasia, lakini Tanzania sio eti? Ahahahahaha!!
 
2020 hawakufika hata wapiga kura 10m, ama unadhani kila mtu anaamini taarifa za kupika?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom