Kinachowatisha CCM kwenye No Reforms no Election

Kinachowatisha CCM kwenye No Reforms no Election

Kwa miaka mingi wananchi wamekuwa hawapigi kura kwa sababu hawaoni umuhumu ikiwa mshindi anajulikana ni wa kuchonga. Kimsingi tuliwachelewesha wananchi kwenye hili.
Miaka mingi wametumia wingi wa wapiga kura kwa kusema ccm walihamasika wakawapigia kura wao

Sasa wananchi wakihamasika wasiende kupuga kura itakuwa aibu kubwa kwa ccm.

Ndio maana wanatafuta njia kuilainisha chadema.
 
CUF walisusia uchaguzi. Wakapita wabunge wa CCM kwa kura chache sana. Wakakejeliwa na CCM na wapinzani.
Ikitokea CDM wasishiriki CCM watafurahi sana.
Ni sawa hivyo kuliko kusindikiza ujinga. Mnadanganywa mnashiriki, wanaitangazia dunia wameshinda kidemokrasia.
 
CCM hawana hoja za kujibu kuhusu No reform ni weupe..

Sasa hivi wameanza kuomba poo kwa mapolice wao wawasaidie.

Na bado - huko ni mbiga tu bado Kanda ya Ziwa - mtapandisha presha hadi 389 kwa 10

Lissu si Mbowe mliyezoea kumchezea chezea sharubu
 
CCM hawana hoja za kujibu kuhusu No reform ni weupe..

Sasa hivi wameanza kuomba poo kwa mapolive wao.

Na bado - huko ni mbiga tu bado Kanda ya Ziwa - mtapandisha presha hadi 389 kwa 10

Lissu si Mbowe mliyezoea kumchezea chezea.
CCM hawahitaji kujibu hoja, hawayaki Chadema kueleza ukweli kwa wananchi.

Kushinda wanashinda kwa wizi , hoja wajibu hoja ili iweje?
 
Miaka mingi wametumia wingi wa wapiga kura kwa kusema ccm walihamasika wakawapigia kura wao

Sasa wananchi wakihamasika wasiende kupuga kura itakuwa aibu kubwa kwa ccm.

Ndio maana wanatafuta njia kuilainisha chadema.
Hahaha kweli aisee
 
Tundulisu dakika zile zamwisho ,alizoongea alitakiwa awambie wakinamama warudi nyuma wamaume wote ,wasogee mbele jukwani watoto watoke eneo husika

Kila mwananchi ,aandae maji

Na mikutano ijayo Kila mwananchi awe na makopo mawili ya maji kwajili ya kunawa yakipigwa mabomu
 
Kwanini wasishiriki uchaguzi, huku wakihamasisha kama wataibiwa wataleta maandamano nchi nzima kila kituo cha kupiga kura, kila sekemu, mkoa Tanzania?

Wakishiriki hawawezi kukosa kura hata milioni tano. Itawapa wabunge hata 30. Hao wanaweza kuwa sauti yao bungeni. Duniania. Pia watapata ruzuku. Ipi ni better options.

Usishiriki uchaguzi uwe pembeni, irrelevant, mfu, usiye na sauti au ushiriki uwe na sauti, pesa, relevant?

..Cdm wakishiriki uchaguzi DOLA itahakikisha wanapewa kura kiduchu zitakazopelekea kupata ruzuku isiyo na manufaa yoyote kwa chama.
 
Chama pekee kinaweza kushinda jimbo ni CHADEMA hivyo vingine labda vipewe kama CCM ifanyavyo miaka yote.

CHADEMA wasishiriki, ni ujinga kushiriki ukiwa unayajua matokeo.

Kitendo cha CHADEMA kuto kushiriki HUTOONA wanachi wakienda kupiga kura, amini hilo.

Kupata kura Milioni 5 halafu huna mbunge na huna urais inakusaidia nini?

Serikali za mitaa walipata zero, na Ubunge Zero, Urais Zero, sasa unashiriki kumfurahisha nani?

..hawawezi kupewa kura halali.

..dola itahakikisha Cdm wanapewa kura kiduchu ili ruzuku nayo iwe kiduchu washindwe kuendesha chama.
 
Dawa ni kutoshiriki kabisa uchaguzi ujao kama hakuna reforms na Tume huru ya uchaguzi. CHADEMA hawapaswi kuwa baridi na moto kwa wakati mmoja #NoreformsNoelection ndio njia sahihi inayoeleweka na tayari kuna watu kwa chaguzi zote zilizopita hawakuinua mguu kwenda kupiga kura ambayo ni maigizo.

Nchimbi anajidanganya kufikiria kuwa uchaguzi hauwezi kuzuiliwa licha ya uwepo wake kuwa kikatiba. Wananchi wanaopiga kura ndio wenye hoja hiyo
CHADEMA ni watekelezaji tu na Tundu Antipas Lissu ndie yule Mussa wa kwenye Biblia na sio LAZIMA yeye ndie awe Rais, mwelekeo ni kung'oka kwa hicho chama chakavu tena dharimu.

Kuna ujinga mwingine unapenyezwa eti uchaguzi utafanyika tu hata kama CHADEMA hawatashiriki eti kuna vyama vingine....Nasema THUBUTU!
Credibility ya CCM kushinda uchaguzi inaamuliwa na chama chenye wafuasi wengi na kina angalau structure ya uongozi inayotabilika.
Hapa ACT_Wazalendo inahusika na iko upande wa wananchi. CCM ikitegemea majigambo yake ya kuwa na wanachama million sijui ngapi ya wajinga vikiwemo vyama mamluki vidogo vidogo vya mfukoni... Huwezi kuuita uchaguzi. CCM kama wana mtaji huo kwa nini wanahangaika na Lissu sasa na jana tu wameanza kupiga watu risasi na mabomu? 😲
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom