FortJeasus
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 604
- 405
Tatizo kubwa la mtoa maoni wetu ni udhaifu wa fikra na kwa hakika unakwaza kwa kiasi kikubwa matamanio yake ya kutaka kutambulika kama mtu mweledi ,mahiri,mtu anayepaswa kusikilizwa!Asichoelekea kuelewa,nasi tusingependa kuacha kukumbusha kila mara,ni kuwa,kuweza kujivika wajibu wa kuelimisha umma mpana,sharti la awali kabisa ni mhusika kufanya jitihada za makusudi kujielimisha kiasi cha kutosha.Vinginevyo,ukinzani dhidi ya 'tafsiri' zake utaendelea kwa kuwa mapambano hayajafikia tamati.