Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu...

Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu...

Tatizo Msingwa anaiga
tabia ya Lema, lakini inabidi ajue kuwa hulka ya mnyalukolo ni tofauti
kabisa na hulka ya chalii.

Hizi zote ni harakati za Msigwa kujaribu kujisafisha jina lake baada ya
kujidhalilisha kwa hotuba mbovu aliyotoa. Kama hotuba kashatoa, maji
yameshamwagika, ajitahidi tu next time atoe hotuba yenye mashiko.

Maggid, poleni sana hapo. tafadhli jitahidi kumtafuta Msigwa muongee,
afanye siasa za kujenga nchi. Naona katuma vijana wake waje kusema
kashikwa na polisi kumbe yuko kwenye Harambee!!!

hivi wewe upo? umenawa uso kweli au unavamia sherehe za watu bla mwaliko. Taifa hili limezidiwa na watu malimbukeni! Jaman nachoka kuelimisha,huwezi tibu malaria kwa Panadol!?
 
We nae unyamaze tu ulikua wa maana zamani toka wamekununua umekua mchumia tumbo. Nishaisahau hata blog yako, na uache kujitamba msigwa hamna ujirani wowote yeye anasema anakujua kama muandishi wa habari aliekua makini zamani ila kutokana na uoga wake amekua muandishi wa habari wa CCM. Sasa sijui wajikomba kwake??.
 
Ndugu Mjengwa, hapo siwezi kukuunga mkono kwa sababu umeangalia upande mmoja tu! Nasema hivi kwa sababu hata hao watawala wangewenza kufanya hicho unachosema Mh. Msigwa angefanya. Mfano, badala ya kutumia nguvu wangemwita mbunge ili waongee naye. Cha msingi sana serikali kwa ujumla wake ukae chini ione nini wanachokikosea katika uongozi wao. Leo tunaongelea Iringa na tunashangaa lakini sehemu zingine pia kuna matatizo haya yanatokea sana. Hao wanaosema wamachinga wanaziba barabara ya magari, magari ya nani maana wamachinga hawana magari!! Mambo haya yafikiriwe vizuri zaidi!!
 
Wahenga walisema 'Akili ni nywele na kila mtu ana zake'Aliyoyasema Mjengwa ndio uwezo wake wa kufikiri na kuchambua hali halisi inayotokea Iringa ulipoishia na mimi simlaumu maana aliyoyasema ni yake na kila mtu ana yake,kuna mambo ya msingi ya kuangalia kabla ya kuanza kuzungumzia suala hili na kwa wale ambao wanayajua tunataka wayaweke hapa ili tujadili toka chanzo cha tatizo mpaka hapa tulipofika,tusiwe watu wa kuangalia matokeo pekee bila kuangalia chanzo cha tatizo.
Nilimsikia Kigoda akisema kuwa Wamachinga waachwe wafanye biashara ila sikusikia mtu kusema chochote wala wazee wa makala hawakuja na makala kuwa anakiuka sheria za Halmashauri ambazo hutunga sheria ndogo ndogo kulingana na eneo husika,leo tunaona Dar wamachinga walitengewa Machinga Complex,tujiulize,je wapo pale kama sheria ya Halmashauri ilivyotaka?Tujaribu kuwa wakweli kwenye mambo ambayo tunaona kabisa kuwa yana manufaa kwa nchi,wale vijana wakigeuka majambazi baada ya kushindwa kufanya biashara mtalaumu nyie ambao mnashabikia wao kubaki katika maeneo ambayo hawawezi kufanya biashara?
Anayeujua kwa undani mgogoro huu basi atupe tatizo lilipo tujadili maana kwa hali ilivyo haujaanza jana na hautaisha kwa kumkamata mbunge.
 
huyu mwandishi ana jambo na msigwa tena ni gamba toka msigwa awaseme wanaomaliza tembo mnavurugia jimboni hamjengi ndo mnazidi toboa mtumbwi uzame haraka
 
Umeandika vizuri majid, ila kwakua wabongo hatupendi ukweli tutamtetea mchungaji wa kiti moto. Sipendi siasa za vurugu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
...Lakini unaipenda CCM na Kamuhanda
 
We nae unyamaze tu ulikua wa maana zamani toka wamekununua umekua mchumia tumbo. Nishaisahau hata blog yako, na uache kujitamba msigwa hamna ujirani wowote yeye anasema anakujua kama muandishi wa habari aliekua makini zamani ila kutokana na uoga wake amekua muandishi wa habari wa CCM. Sasa sijui wajikomba kwake??.
yani amenikera sana mjengwa
 
Mjengwa na waandishi wa magazeti ya uhuru hawanatofauti,umekuja na matokeo badala ya kuanzia na chanzo,hili tatizo Msigwa aliliongelea bungeni na inaonyesha huo mgogoro sio leo,jana au juzi niwamuda mrefu,tatizo letu wa bongo tukishakaa kwenye kiyoyozi tuna-assume maisha kwa wote ni kama yako,hivi unamtupa mtu porini hakuna miundo mbinu,huduma za kijamii akawauzie panya,acheni hizo na kwa haya mtajibu kwa Mungu
 
Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Mungu lete utulivu watu Wako tumalize kazi,Yesu urudi kulichukua kanisa lako,Amen
...Itabidi aamue nani anayetaka ambariki kati ya "mungu" wa akina Igondu, Kamuhanda, Mwigulu au Mungu wa akina Ulimboka, Kibanda, na Mwangosi.
 
Majjid amenena jambo la kweli kabisa. Tatizo la Msigwa (ambaye nina shaka na uchungaji wake), ni kwamba anataka kujipatia umaarufu kwa nguvu kubwa kwa staili ya Lema. Wahenga walisema ukimwiga tembo kunya, utapasuka msamba!

Msigwa anapaswa kutumia weledi na busara. Hata kama Chadema wataongoza nchi hii, lazima wafuate taratibu za mazungumzo na kuheshimu sheria. Kumbuka, kuondolewa kwa machinga hapo walipo ni kutokana na kuonekana kunaweza kutokea maafa ya ajali na kupoteza vijana/watu wengi. Sioni kosa la Manispaa kuchukua hadhari mapema kabla ya kufikwa na maafa.

Siasa nyepesi na kutafuta umaarufu haraka haraka ni mambo yasiyoweza kuisaidia tanzania. Siasa za kina Gandhi na kina Martin Luther King Jr, hata kina Mwalimu Nyerere za kutumia nguvu za hoja bila vurugu, zina tija kubwa sana. Msigwa anapaswa kujitafakari na kurejea maandiko ambayo anataka tuamini kuwa ameyasoma kiasi cha kustahili kuitwa Mchungaji.

Naunga mkono hoja ya Majjid.
 
Maggid, wewe ni mwandishi wa Habari. Naomba unijibu kwa ukweli na uwazi maswali yafuatayo:

Nani aliyechagua Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa?
Full Council ya Halmashauri ya Manispaa ina Uwiano gani kati ya CCM na Chadeama?

Mamlaka (Authority) ya kiongozi yeyote katika mazingira yoyote huwa inajigawa katika njia mbili: Ushawishi binafsi wa kiongozi, na Ushawishi wa shurti ambao unaletwa na Nafasi ya Kiserikali anayopewa Kiongozi kwa jina la cheo.

Power Base ya msigwa inasimamia wapi? Je hili haliwezi kuwa ni mgongano wa power base mbili ambazo zimeshindwa kukubaliana katika vikao ambavyo si vya wazi?

MY TAKE:

You are jumping to conclusions! Una uhakika Msigwa hajaongea na structure za Kiserikali kutoa mtizamo wake?
Una uhakika hakuna upuuzwaji wowote wa mapendekezo umefanywa kabla ya tukio la leo? Hii post yako ni propaganda kumhusisha Msigwa peke yake katika tatizo la wengi. Shape up!

Hili si tatizo la Msigwa peke yake.... Tatuta lugha tofauti kidogo urudi hapa.
 
Ubarikiwe mkuu magid kwa maoni yako constructive kwa nchi na distructive kwa waovu wa taifa letu ila mungu anawashuhudia na kamwe hawatoweza kupata watakacho.
 
Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Mungu lete utulivu watu Wako tumalize kazi,Yesu urudi kulichukua kanisa lako,Amen

Kutokulijua na kutolitafakari Neno! Faida yake ndio haya maandishi yako machafu uliyojiandikia hapa Yesu tunayemjua siye huyo uliyemuelezea.kama hujui Bora kujikalia kimya kuliko kuandika utumbo.

The nation that destroys its destroys itself.
 
Ndugu zangu, Leo saa mbili na nusu asubuhi nilifika Jengo la NSSF nikitokea kufanya jogging yangu ya asubuhi. Nilifika hapo kuwahi kununua magazeti. Hali ilikuwa shwari kama ilivyo kawaida ya Iringa Jumapili asubuhi. Kunako saa tatu asubuhi nilipokuwa nyumbani nikisoma magazeti, ndipo niliposikia mlio wa kwanza wa bomu la machozi. Idadi yake ikaanza kuongezeka. Nikiwa na kamera yangu nikajisogeza hadi katikati ya mji kufahamu zaidi kinachotokea. Nilichokiona ni vurugu kati ya Wamachinga na Jeshi la Polisi. Tatizo? Ni dogo sana, lakini linakuzwa kwa vile siasa imepelekwa mbele badala ya kutanguliza hekima na busara. Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi. Kinachotokea Iringa kwa sasa ni doa kubwa kwa mji wetu wenye sifa ya muda mrefu ya utulivu. Kina athari kubwa kiuchumi pia. Pale Iringa mjini nilichokiona leo ni kama mji ulio katika mapigano ya kivita. Watu ni wachache na wenye hofu. Biashara nyingi zimesimama. Niliziona Daladala zikitoka Kituo cha Miyomboni bila hata abiria, watoke wapi? Wakati kwa sasa walio nje ya mji wameambiwa na jamaa zao walio katikati ya mji kuwa wasijaribu kufika mjini, kwamba hali imechafuka. Nimeongea na mwuza nyama ya bucha aliyeniambia kuwa mgomo wa Daladala wa hivi karibuni ulimfanya apate hasara kubwa kwenye biashara yake ya nyama kwa vile wateja wake wengi wanatoka nje ya mji. Na anachokiona leo ni hasara nyingine kwa vile hakutakuwa na biashara nzuri. Je, ni wafanyabiashara wangapi watakaoathirika na hali hii ya leo? Na kwa kuwa mkweli, kisiasa kinachotokea Iringa kwa sasa kinaweza kuwa na athari hasi kwa Mchungaji Msigwa badala ya kumjenga kisiasa, kwani, wengi niliozungumza nao katikati ya mji wanamwona Mchungaji Msigwa kuwa ni mtu ambaye angeweza kuiepusha hali hii kama asingeyatumia majukwaa ya siasa kuwahamasisha Wamachinga kuendelea kufanya biashara, na hivyo, kutokutii amri ya Manispaa. Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu. Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye Harambee pale Tumaini University. Kama Mchungaji Msigwa angejibu simu yangu, basi, ningemwambia haya ninayoyaandika hapa. Maggid Mjengwa, Iringa. 0754 678 252MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
Naomba nikuulize swali kidogo, wewe ni mkazi wa hapo Iringa1. Hao wamachinga tangu wameanza kufanya biashara katika maeneo hayo wameleta madhara gani?2. halmashauri ya mji kuna eneo lolote lililotengwa ambalo linafaa/ litafaa kwa biashara za kimachinga?3. Katika fujo za leo walioanzisha fujo ni nani kati ya Polisi na wamachinga?4. Wakati wamachinga wanavamiwa na Polisi Mchungaji Msigwa alikuwepo kwenye tukio?5. Hao Pilisi waliomkamata Msigwa walimkuta wapi hadi wakamkamata?
 
Maisha ni magumu sana....vijana wanaamua kujiajiri kwa kuuza bidhaa tofauti tofauti kwa kufuata kanuni za uchumi (4p's or 7p's of marketing mix) mojawapo ni people (customer) ili waweze kuuza bidhaa zao na wajikwamue kichumi....tumeona mifano jinsi ya wamachinga wa karume walivyogoma kuhamia machinga complex kwa kigezo hiki. Msigwa akichangia bajeti ya wizara ya viwanda na Biashara alimsihi waziri kwa dhati awaonee wamachinga wa Iringa huruma, ili wafanye biashara eneo la Mashine tatu huku akimsihi kuwa serikali iache kuwaona wamachinga hao kama kero, ilihali na wao ni watanzania ambao wameacha kufanya shughuli ziso halali na kufanya zilo halali. Hii inaonesha tu (kwa nadharia) kuwa Mchungaji amefanya mambo mengi kutatua tatizo hili bila mafanikio. Shida ya viongozi wetu ambao wengi maisha yao ni mazuri ni kushindwa kuwakumbuka vijana wengi walio masikini......na shida kama hii ikitokea usidhani kuwa wana hofu ya amani katika mioyo yao bali wana hofu ya kupoteza mali zao......kwa kuwa ni walafi waso na utu hata kidogo. Majid fikiria kwa pande zote kaka.
 
Tatizo la huyu kibaraka wa CCM akibandika uzi wake humu anaenda kulala usingizi, yeye kama ni mwenyeji wa Iringa na mwandishi wa habari alitakiwa aeleze chanzo cha mgogoro na sio kukurupuka tu na kuweweseka tu kuwa msigwa hajapokea simu yake na haya ndiyo alitaka amwambie, angemtumia sms basi au angemtumia e-mail, mwanzo ulileta uzi ukimshambulia msigwa kuwa amebadilika, ana magari. Cha muhimu mpigie simu chilisosi lukosi mpeane moyo wa kwamba mtakuja kulichukua jimbo mwaka 2015.. Peter Serukamba!
 
Back
Top Bottom