Kinachopenda ni moyo au ubongo?

Fredinho

JF-Expert Member
May 18, 2016
971
1,160
Kazi ya moyo ni kusukuma damu tu,kazi ya ubongo ni kuongoza mwenendo wa matukio mwilini ikiwemo kufikiri na kufanya maamuzi,kwa nini basi moyo unahusishwa sana na mapenzi?mara utasikia mtu anamwambia mpenzi wake moyo wangu wote nakupa,mara nilikupa moyo wangu ukautupa jalalani, mara sitampa tena mwanaume moyo wangu mara nitakupenda kwa moyo wangu wote nk,kwa nini isiwe nitakupenda kwa ubongo wangu wote,nakupa ubongo wangu nk?
 
Katika mapenzi tunatumia neno moyo kwa sababu moyo una umuhimu sana katika mwili wa binadamu ukisimama basi mtu uhai haupo tena hivyo tunaposema moyo huwa tunajaribu kuonyesha ni jinsi gani upendo ulionao una thamani kwa huyo umpendae...
 
Upendo wa dhati unatoka moyoni!!!
Ndo maana mtu anaona mabaya yote na usaliti toka kwa mwenzake na bado anampenda... Kazi ya ubongo ni kufikiri na kupambanua mambo...
Ndo ile mwenzako akifukuzwa kazi ubongo unafanya mahesabu ya kua utaishije, kama upendo haujapandikizwa moyoni utaishia kumuacha tu mwenzako...
Ata kama upendo unatoka moyoni, inabidi akili pia itumike, ka aivyo utaumizwa sana na kua bwege
 
This increasing heart rate is the reason the heart is associated with love. ... However, one could argue that without blood in the brain, it would not function and thus we would not physically be able to love. The two organs therefore have a symbiotic relationship when it comes to this popular emotion that we call love.

Brain v.s Beat: Does love come from the heart?

Symbiotic relationships are a special type of interaction between species/organs
 
hamna kinachohusika hapo vyote mnavisingizia tu

ningekua nnafahamu hiko ki-organ kinachohusika na kupenda ningefanya operation at any coast maan am tired of this womens
 
Katika mapenzi tunatumia neno moyo kwa sababu moyo una umuhimu sana katika mwili wa binadamu ukisimama basi mtu uhai haupo tena hivyo tunaposema moyo huwa tunajaribu kuonyesha ni jinsi gani upendo ulionao una thamani kwa huyo umpendae...
Asante mkuuu hii kweli
 
Kazi ya moyo ni kusukuma damu tu,kazi ya ubongo ni kuongoza mwenendo wa matukio mwilini ikiwemo kufikiri na kufanya maamuzi,kwa nini basi moyo unahusishwa sana na mapenzi?mara utasikia mtu anamwambia mpenzi wake moyo wangu wote nakupa,mara nilikupa moyo wangu ukautupa jalalani, mara sitampa tena mwanaume moyo wangu mara nitakupenda kwa moyo wangu wote nk,kwa nini isiwe nitakupenda kwa ubongo wangu wote,nakupa ubongo wangu nk?
Kuna connection kubwa sana kati ya ubongo na moyo from biological science point of view, mambo ya blood na oxygen..
 
Back
Top Bottom