Kinachoitwa uchaguzi wa CHADEMA ni maigizo na kiini macho cha Demokrasia

Shigganza

Senior Member
Joined
May 24, 2018
Messages
157
Points
500

Shigganza

Senior Member
Joined May 24, 2018
157 500
Katika uga wa taaluma ya sayansi ya Siasa moja ya viashiria vya uchaguzi kuwa huru na haki ni kuwepo kwa Wagombea wenye Sifa na Nguvu sawa au zinazokaribiana.

Kinadharia CHADEMA imekuwa ikijipambanua kama Chama chenye Demokrasia kuanzia jina lake, ni katika muktudha huo ilitarajiwa na Watanzania wengi kuona Chama hicho kinatafsiri kwa vitendo dhana hiyo.


Bahati mbaya CHADEMA kimeshindwa kutumia vizuri fursa ya zoezi la uchaguzi wa Ndani kudhibitisha kwa vitendo nadharia hiyo, kwani ni dhahiri kinachofanywa na CHADEMA sio uchaguzi tena bali maigizo na kiini macho ya uchaguzi na Demokrasia kwa ujumla.

Hebu tazama wagombea waliopitishwa kugombea katika nafasi mbalimbali na matokeo yake.

Nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Freeman Mbowe vs Cecil Mwambe, ukiangalia wasifu na wajihi wa wagombea hawa ni Mbigu na Ardhi, katika mazingira haya ni wazi MBOWE aliandallwa Mazingira ya ushindi na ni sahihi kabisa kusema hapakuwa na uchaguzi zaidi ya igizo la uchaguzi lililowasilishwa kwa hadhira ya wanachama na Wananchi.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti bara, wagombea walikuwa TUNDU LISSU vs SOPHIA MWAKAGENDA ukiondoa utofauti mkubwa wa wasifu wa Wagombea hawa, LISSU alipendekezwa kugombea na MBOWE ambae ndio ‘mmiliki wa Chama’ hapa hauhitaji kusubiri matokeo, hata kama ingetokea SOPHIA akashinda bado kamati ya Uchaguzi iliyochini ya MBOWE isingedhubutu kwenda kinyume na bosi wake (MBOWE)

CHADEMA kuanzia hatua za awali za mchakato wa kuchukua fomu kilihakikisha kinawadhibiti wagombea ambao wangetoa ushindani kwa MBOWE, mathalani SUMAYE aliwekewa Zengwe na hujuma na baadae akajitoa.

Ni wazi kuwa MBOWE na CHADEMA hakikuwa tayari kufanya Uchaguzi wa viongozi wa kitaifa kwa hiari licha ya Muda wa kikatiba kufika na kupitiliza, bali kilifanya ili kutii agizo la Msajili.

Ni wakati muafaka kwa wafuasi, wapenzi , mashabiki, wakereketwa na wanachama wa CHADEMA kuanza vuguvugu la kupigania kuwepo kwa Demokrasia hai Ndani ya Chama ili kupata uhali wa kimaadili ‘moral authority‘ wa kukemea na kuhubiri Demokrasia Nje ya Chama.
 

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
35,165
Points
2,000

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
35,165 2,000
Aiseee mna nini na CHADEMA? Yaani mara Mwambe atatuvusha, mara hakuna uchaguzi, mara sijui ujinga gani! You guys tafuteni kitu cha kufanya, Hii ya kuichafua CHADEMA hamuiwezi kabisa! Mnazidi kuwapa Promo!

Jana mwenyekiti wenu alikua anazindua Jengo LA Mahakama sijaona mkizungumzia chochote nyie wote macho yalikua kwa CHADEMA!!

SAA hizi umekuja na ujinga mwingine....haya MUNGU anatusaidia kutupa promo! Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,383
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,383 2,000
Huo utaalamu wako umeutolea wapi!. kwamba wawepo wagombea wenye sifa na nguvu zinazoshabihiana?!, kawaida mtu akiamua kugombea cheo fulani tayari yeye binafsi hujiona ana hizo nguvu za kushindana na mwenzie, sasa mpaka baadae matokeo yatakapotangazwa ndio atapata jibu sahihi kama kweli alikuwa na hizo nguvu au alijidanganya.

Vinginevyo unataka mtu kabla hajagombea akawaulize wapiga kura kama ana nguvu au hana!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

TzPride

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2006
Messages
2,598
Points
2,000

TzPride

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2006
2,598 2,000
Ulitaka nani awatafute hao wagombea unawataka wewe? Mwambe kachukua form na hakuna mwingine kataka hilo, sasa wewe unalalamika? Mwenyekiti wa CCM huwa anagombea na nani?
 
Joined
Nov 27, 2019
Messages
22
Points
75
Joined Nov 27, 2019
22 75
Wagomea wenye wasifu na sifa za kupambana na Mbowe walidhibitiwa kwa hujuma na zengwe kuchukua na kurejesha fomu. Muhimu zaid baraza kuu linapaswa kuhakikisha linapitisha watu wenye hizo sifa, bahati mbaya walitishwa wasijaribu kuonja sumu na MBOWE wakaufyata.
 

MAPITO Mwanza

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2018
Messages
1,041
Points
2,000

MAPITO Mwanza

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2018
1,041 2,000
toka nimezaliwa Leo ninakalibia kuitwa babu lakini sijawahi ona au kusikia uchaguzi wa MWENYEKITI ndani ya chama chakavu zaidi ya kupendekeza JONH Pombe awe MWENYEKITI Mbowe kachaguliwa tena kwa uwazi hata mshindani wake mwambe hajalalamika nyinyi pilipili ya shamba yawawashia nini
 

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
6,181
Points
2,000

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
6,181 2,000
Chadema kuanzia hatua za awali za mchakato wa kuchukua fomu kilihakikisha kinawadhibiti wagombea ambao wangetoa ushindani kwa MBOWE, mathalani SUMAYE aliwekewa Zengwe na hujuma na baadae akajitoa.
Wagomea wenye wasifu na sifa za kupambana na Mbowe walidhibitiwa kwa hujuma na zengwe kuchukua na kurejesha fomu. Muhimu zaid baraza kuu linapaswa kuhakikisha linapitisha watu wenye hizo sifa, bahati mbaya walitishwa wasijaribu kuonja sumu na MBOWE wakaufyata.
Ninacho wapendea hawa wapambe nuksi wa CHAMADOLA ni kufikiria kuwa ile mizwenge yao ndiyo hiyo hiyo vyama vingine hutumia.
Waulizeni Mzee Sumaye kawekewa zengwe gani kwenye uenyekiti wa chama, alijitoa mwenyewe wakati Mwambe alisimama. Tuambie nani kazuiwa kuchukua fomu, nani alishindwa kurejesha fomu (style ya Korogwe, au kufungiwa ndani hadi muda upite). CCM ndio baba lao kwenye haya kumbuka 2010 Mzee Malecella aliposimama ili aje kuomba kura, CCM walimuuliza "Sasa wewe ukienda huko, nani atamsaidia mwenyekiti?". Bilali alipata kura za ushindi Zanzibar, Dodoma jina lake halikufika. Sio kila chama kinatumia mbinu za kishenzi cha Chamadola.
Mmepiga kelele uchaguzi wa CDM, umefanyika kwa mafanikio makubwa , sasa mnalia nini?
 

PTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
7,741
Points
2,000

PTER

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
7,741 2,000
Aisee!!!
Taaluma ipi ya sayansi ya siasa inayosema ili uchaguzi uwe huru na wahaki lazima wagombea wawe na sifa sawa na nguvu zinazolingana?
Unamaanisha sifa zipi ?
Unamaanisha nguvu zipi?

Hivi tafsiri yako ya uchaguzi kuwa huru na swa ni wagombea kuwa na sifa sawa au ni taratibu za uchaguzi kufuatwa?

Hivi kuna mtu yoyote aliyechukua form ya kugombea hajapewa nafasi ya kugombea na kupigiwa kura ?

Kama wagombea walikuwa Mbowe na Mwambe ulitaka kamati ya uchaguzi ifute uchaguzi kwa sababu Mbowe ana nguvu kuliko Mwambe ?

CCM imekuwa ikienda kwenye uchaguzi wa kitaifa kupambana na vyama vya upinzani visivyo na raslimali nyingi kama ccm mfano DP hivi uchaguzi huo huwa siyo huru na wa haki ?

Una ushahidi wowote unaonyesha Mbowe ni mmiliki wa CHADEMa?

Ulitaka Lissu angepambanishwa na nani ?


Tunafahamu ccm wengi akili zenu ziko matakoni tu hebu jaribuni kuficha hivi viaibu vidogo vidogo.

Pumbavu kabisa.
Shigganza,
 
Joined
Nov 27, 2019
Messages
22
Points
75
Joined Nov 27, 2019
22 75
PTER, tatizo vijana wengi wa upinzani mnajenga hoja kwa mrengo wa itikadi za vyama, mtoa mada ameandika kuhusu Chadema ambayo saizi iko kwnye uchaguzi, nyie mnazungumzia habari za CCM. subirini uchaguzi wa CCM ukifika akatoa uchambuzi mmkosoe, saizi tuijadili Chadema.
 

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,791
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,791 2,000
Shigganza,
Hivi kuna uchaguzi wa maigizo zaidi ya ule wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni?

Iweje Leo uuone uchaguzi wa Chadema kuwa wa maigizo wakati ulifunga mdomo wako na macho yako wakati wa UCHAFUZI wa serikali za mitaa, wala hukutaka hata kunyanyua mdomo wako kama ufanyavyo sasa kukemea uhuni ule?
 

Forum statistics

Threads 1,390,621
Members 528,220
Posts 34,056,665
Top