Mhhhh,
Kwani "Chama Cha Mapinduzi" na "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo" kipi kinatakiwa kuwa cha kwanza kwa mpangilio wa herifu zake?
Inaweza kuwa ni moja ya sababu,na kama ndio sababu kuu je watakizuia kisisajiliwe kamwe kulinda hiyo advantage. Minadhani kuna sababu nyingi na nzito kuliko hiyo
Hata mimi nakubaliana na wewe kuwa inawezekana CCM ina sababu zingine za kuzuia kusajiliwa kwa CCJ,lakini kwao ushindi ni zaidi ya kitu kingine kile duniani. Kimsingi CCM haishindi nje ya sanduku la kura na kizuuizi chochote kile kinachotokea mbele ya mazingaombwe yao lazima kichukuliwe kwa uzito unaozidi ule wa kuokoa maisha ya mgonjwa.
Binafsi nimewahi kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali na mara zote wapiga kura wasiojua kuandika na kusoma ndiyo mtaji wa CCM, na wao ama wasaidiwe na watu wengine kupiga kura au wapewe maelekezo "mazuri" ya jinsi ya kupiga kura na njia rahisi ni kumwambia akachague mgombea ambaye picha yake ni ya kwanza kwenye karatasi ya kupigia kura.
Pia sielewi ni kwa nini mpaka sasa vyama vingine havizuii kisheria mtindo wa watu wengine kuwapigia kura wale wasiojua kusoma na kuandika kwani kunakiuka ile sheria inayosema kura ni SIRI!!