Kinachoitisha CCM ni hiki!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinachoitisha CCM ni hiki!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, May 30, 2010.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna mitazamo tofauti kuhusu ni kwa nini msajili wa vyama vya siasa nchi hataki kukisajili Chama Cha Jamii (CCJ).

  Kwa mitazamo yangu na uchunguzi binafsi ndani ya ngazi za juu za uongozi wa CCM nimefikia kuamini kuwa hofu ya CCM si chama chenyewe cha CCJ bali ni Jina la chama hicho.

  CCM kwa miaka mingi tangu mwaka 1995 imekuwa ikifaidika kuwekwa mwanzoni mwa karatasi ya kupigia kura kwenye kila uchaguzi kutokana na jina lake kuwa na herufi inazoipa nafasi ya kialfabeti kukaa mwanzoni mwa karatasi za kupigia kura. Kwa kusajliwa kwa CCJ nafasi hiyo ya kukaa mwanzoni mwa karatasi ya kupigia kura itapotea.

  Kama utafiti wa REDET ulivyowahi kuonyesha ni kwamba wanaoichagua CCM wengi wao ni wale wasiojua kusoma na kuandika, kwa hiyo ilikuwa ni rahisi kwa CCM kuwaelekeza kwamba kazi yao ni kumchagua mgombea ambaye picha yake ni ya kwanza kwenye karatasi ya kupigia kura, sasa CCJ ikisajiliwa itakuwaje?

  Kwa hivyo hofu ya CCM siyo kwenye nguvu ya CCJ kama chama bali ni nguvu ya kiuchawi wa kialfabeti (Alphabetical Magic) iliyonayo CCJ kwa kuwa "J" imeitangulia "M" katika alfabeti. kwa maana nyingine kama CCJ ikisimamisha mgombea wa Urais basi jina na picha yake vitamtangulia yule wa CCM (Kikwete?)
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I am afraid to comment, to allow others on monday may be I will be back then after.
   
 3. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good observation...
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mhhhh,

  Kwani "Chama Cha Mapinduzi" na "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo" kipi kinatakiwa kuwa cha kwanza kwa mpangilio wa herifu zake?
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Labda kama wana imply chadema ni CDM,then yes ccm comes first and then cdm,and so therefore if im right,now itakuwa ccj,tehn cdm and ccm being the last,hopefully wananchi wataelewa.
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kama kuna kaukweli flani hivi.
  Ni utafiti mzuri.
   
 7. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hata miminilishawahi kuisikia hiyo thus why wana shinda,na wengine wanafikiria bado ni chama cha nyerere ndo maana wanakipigia kura!
   
 8. P

  Paul S.S Verified User

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Inaweza kuwa nimoja ya sababu,na kama ndio sababu kuu je watakizuia kisisajiliwe kamwe kulinda hiyo advantage. Minadhani kuna sababu nyingi na nzito kuliko hiyo
   
 9. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nakubaliana na wewe kuwa inawezekana CCM ina sababu zingine za kuzuia kusajiliwa kwa CCJ,lakini kwao ushindi ni zaidi ya kitu kingine kile duniani. Kimsingi CCM haishindi nje ya sanduku la kura na kizuuizi chochote kile kinachotokea mbele ya mazingaombwe yao lazima kichukuliwe kwa uzito unaozidi ule wa kuokoa maisha ya mgonjwa.

  Binafsi nimewahi kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali na mara zote wapiga kura wasiojua kuandika na kusoma ndiyo mtaji wa CCM, na wao ama wasaidiwe na watu wengine kupiga kura au wapewe maelekezo "mazuri" ya jinsi ya kupiga kura na njia rahisi ni kumwambia akachague mgombea ambaye picha yake ni ya kwanza kwenye karatasi ya kupigia kura.

  Pia sielewi ni kwa nini mpaka sasa vyama vingine havizuii kisheria mtindo wa watu wengine kuwapigia kura wale wasiojua kusoma na kuandika kwani kunakiuka ile sheria inayosema kura ni SIRI!!
   
 10. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimewahi kusimamia uchaguzi; ni kweli observation ya jamaa; huwa wanafanya kuwa 1. CCM 2. Chadema 3. CUF na wakati mwingine 1. CCM 2. CUF 3. Chadema; wanageuza kutegemea na upepo huwa wanafanya analysis kabla; na wamekuwa sana wanatumia vinafasi kama hivi n k.
  Unajua Chadema kifupi chake ni CDM lakini wanatumia neno zima; hata kwa msajili ni hivyo; so hata hivyo CDM ingekuwa ni baada ya CCM so hilo nakubaliana na swala la jamaa kuwa ni kimojawapo ndio m aana tendwa kakatazwa kusajili kabisa; CCM wanaogopa; CCJ hawako serious kabisa ni waharibifu wa siasa ila ina mpangilio wa herufi unaofanana na ccm na ndio maana malengo yake ni kama CCM haijajua itambana nayo vipi; uoga tu na kutojiamini si unajua siasa za kibongo uhuni tu hamna lolote; mhuni ndiye mtawala mkuu; nimewahi kulalamikia CCJ naona haina jipya; kama ina ;lengo kupigania Ufisadi kuna vyama vimejiweka mbele kama majemedari ali mradi unahabari inakuwa habari n k kwa nini uanze na chama kipya kama kweli uko serious-Ila CCM haijajua lengo la CCJ na mbaya hawajaweka watu wao kule ndio maana wanaangalia CCJ watatika vipi; si unajua mamluki wako kibao vyama vya siasa-angalia Mrema wakuu mfano tu; naamini Chadema ndio chama cha kizazi kipya na ambacho dira yake imesimama kwa usahihi; mamluki huwa wanasumbua sana kule ila naamini iko siku watu wataona kuwa bambata iko kule CHADEMA
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kigarama haki hii si ya Vyama pekee vya upinzani bali ni hata wewe waweza kutinga mahakamani maana ina haki yako pia kuona Tanzania inaenda kisheria so weka nguvu zako tafadhali nawe saidia hao unao waita Vyama vya Upinzani wewe ukijiweka nje .
   
Loading...