Kinachoiponza CCM ni katiba yao kuwa Rais wa nchi ndiyo mwenyekiti wao wa Taifa

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,155
3,798
Kama CCM ingekuwa na Mwenyekiti wa Taifa tofauti na Rais wa nchi hali isingekuwa kama ilivyo sasa ya msuguano ndani ya chama. Ndugai kama Mkuu wa muhimili wa Bunge angekuwa na uhuru wa kumkosoa Rais na Rais angeweza kujibu hoja bila jazba. Aidha Rais angeweza kukosoa udhaifu wa Bunge na Spika angeweza kujibu hoja bila jazba.

Kwa kuwa Ndugai kama Mkuu wa muhimili wa Bunge amemkosoa Rais Samia ambaye ndiye Mwenyekiti wa wake wa Taifa wa CCM, inaonekana kama amemdharau Rais. Naye Rais Samia akahamaki kuwa amedharauliwa na kudhalilishwa.

CCM ili kiwe chama imara cha kidemokrasia na kinachoruhusu uhuru wa maoni na uhuru binafsi wa wanachama wao lazima kipitie upya katiba yake na kuirekebisha.
 
Acha kife,tuliwashauri Sana juu ya katiba yao ya kidikteta.
Kwa katiba yao ni lzm mama asimame 2025 na jibu watalipata 2025 wakati ukifika haukwepeki
 
Na katiba ya nchi ilitakiwa kuweka sharti la mgombea wa kiti Cha urais ajivue vyeo vyote vya ki-chama ili aweze kulitumikia taifa. Lakini pia Taifa linatakiwa liwe na mission, vision na strategies ambazo rais atazifuata.

Bunge linatakiwa kuwa na utaratibu au mfumo unaojitegemea wa kumpata speaker badala ya huyohuyo m/kiti wa chama ambaye ni raisi ambaye pia ni mkuu wa mhimili wa serikali kuamua nani awe speaker mkuu wa mhimili wa bunge, kadhalika na mahakama.
 
Hakika tuna safari ndefu kupata ukombozi wa fikra!
 
Kama CCM ingekuwa na Mwenyekiti wa Taifa tofauti na Rais wa nchi hali isingekuwa kama ilivyo sasa ya msuguano ndani ya chama. Ndugai kama Mkuu wa muhimili wa Bunge angekuwa na uhuru wa kumkosoa Rais na Rais angeweza kujibu hoja bila jazba. Aidha Rais angeweza kukosoa udhaifu wa Bunge na Spika angeweza kujibu hoja bila jazba.

Kwa kuwa Ndugai kama Mkuu wa muhimili wa Bunge amemkosoa Rais Samia ambaye ndiye Mwenyekiti wa wake wa Taifa wa CCM, inaonekana kama amemdharau Rais. Naye Rais Samia akahamaki kuwa amedharauliwa na kudhalilishwa.

CCM ili kiwe chama imara cha kidemokrasia na kinachoruhusu uhuru wa maoni na uhuru binafsi wa wanachama wao lazima kipitie upya katiba yake na kuirekebisha.
Rais ni lazima pia awe kiongozi mkuu wa chama. Hii ni standard almost everywhere around the world. Haiwezekani Rais wa nchi akawa controlled na Mwenyekiti wa chama. Hell no.

Tatizo lililopo ni nguvu kubwa ya Rais na kwenye chama na serikali. Kwa katiba ya CCM, Mwenyekiti ndiye anateua Makamu, Katibu na Kamati kuu nzima. In my opinion, this is wrong.
 
Tuliwaambia zamani hawakusikia leo wakati unawalazimisha kusikia.
Tuliwaambia watenganishwe Mwenyekiti asiwe raisi.Raisi awe chini ya Mwenyekiti na raisi awe Mkubwa kuliko Mwenyekiti pia kama ilivyo ANC na Zanupf awakusikia
 
Rais ni lazima pia awe kiongozi mkuu wa chama. Hii ni standard almost everywhere around the world. Haiwezekani Rais wa nchi akawa controlled na Mwenyekiti wa chama. Hell no.

Tatizo lililopo ni nguvu kubwa ya Rais na kwenye chama na serikali. Kwa katiba ya CCM, Mwenyekiti ndiye anateua Makamu, Katibu na Kamati kuu nzima. In my opinion, this is wrong.
Hii ni kwa nchi za kijamaa, kwingine kote raisi hawezi kuwa juu ya chama Ili kuepuka madhara.
 
Katiba ya ccm ni ya kidikteta na inampa Mwenyekiti mamlaka yote ikiwemo kuprint fomu moja tu ya kugombea uraisi na hakuna wa kupinga atafukuzwa uanachama.
Tunapowaambia katiba mpya ni kwa maslai ya wote pia huwa awaelewi
 
Rais ni lazima pia awe kiongozi mkuu wa chama. Hii ni standard almost everywhere around the world. Haiwezekani Rais wa nchi akawa controlled na Mwenyekiti wa chama. Hell no.

Tatizo lililopo ni nguvu kubwa ya Rais na kwenye chama na serikali. Kwa katiba ya CCM, Mwenyekiti ndiye anateua Makamu, Katibu na Kamati kuu nzima. In my opinion, this is wrong.
Siyo kweli kuwa ni standard kwa nchi zote duniani. Hata baadhi ya nchi kubwa kama Marekani, German, France nk viongozi wa nchi siyo wenyeviti wa vyama vyao. Lakini ni kweli katiba ya CCM ina mapungufu mengi ambayo yanamfanya Mwenyekiti wao awe mungu mtu!
 
Katiba mpya ni muhimu sana, kwa wa Tanzania wote bila kijali itikadi ya chama, dini, kabila.
Hii ni kwa ustawi wa wananchi tulipo sasa na wale watakaozaliwa miaka ijayo.
 
Back
Top Bottom