Kinachofanywa na watu wanaojiita maafisa wa bima Kwa waendesha pikipiki wilaya ya Mbogwe kinapaswa kuangaliwa kina sasa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,564
3,472
Kinachofanywa na maafisa bima wilaya ya Mbogwe kinatia mashaka sana kwa wamiliki wa pikipiki na kwa waendeshaji wengine wa pikipiki kwa jina maarufu bodaboda katika wilaya ya Mbogwe. Niliwahi kutoa malalamiko ya aina hii lakini Kwa Sasa naona ni kama historia inajirudia.

Ukusanyaji wa hela za bima unaofanyika unatia fedheha sana na ni hatarishi hata kwa wakusanyaji. Mambo yafuatayo yamenisukuma kuyaandika haya Kwa lengo la kusaidia, mambo hayo ni:

1. Mtindo wanaoutumia kukamata pikipiki Ili watu walipe bima ni mtindo usiofaa na uliopitwa na wakati. Wamekuwa na tabia ya kutumia mgambo na baadhi ya vijana ambao siyo wakazi wa eneo husika kuvizia watu wanapopaki pikipiki tu, wao huzikokota mpaka kituo cha polisi na mwenye pikipiki anapoifuatilia huelekezwa kulipa bima.

2. Ulipaji unaofanyika unafanywa katika namna inayotia mashaka sana kwa mfano leo tarehe 2/6/2023 afisa bima aliyekuwa akipokea pesa aliweka kambi kwenye stationery fulani karibu na kituo cha polisi ambapo ndipo alipokuwa akipokea hela za bima shilingi elfu hamsini na tisa 59,000/= kwa kila pikipiki inayokombolewa. Nilimwambia ni atupe Control number tukalipe akanijibu .."huwezi kupata control number" . Hili lilinistua sana nikaamua kwenda NMB Benki kuuliza na cha ajabu nilipewa maelekezo mazuri na nikapewa control number nikalipa, nilipotoka Benki nilimfuata tena afisa bima ila sikutaka kuongea naye zaidi ya kumuonesha kuwa nimeshalipia na nikaichukua pikipiki yangu. Hivi ni sawa kweli Afisa bima kutoka Kahama kuja Mbogwe na kukusanya hela kwa utaratibu huo anaofanya huyu?.

3.Vijana wanaotumika kukokota pikipiki za watu hata kama wanapewa posho ya kazi hizo zisizofuata utaratibu wanawekwa hatarini sana. Hivi unakokota pikipiki ya mtu uliyoikuta ameipaki mahali kama wakikuita mwizi?... Hawa jamaa wanatumia Utaratibu mbovu sana na ni hatari wasaidiwe hata kwa ushauri kutoka kwenye vyombo vyenye mamlaka.
4. Wanatumia nguvu kubwa kukamata pikipiki Ili zilipiwe bima kuliko kutumia nguvu kubwa kuelimisha watumiaji kulipa bima. Bodaboda wengi hawaelewi maana ya bima ya pikipiki na hakuna fidia yoyote inayotolewa licha ya ajali nyingi za bodaboda Ili angalau watu waone matunda ya bima zao. Itolewe elimu na uhamasishaji utakaoamsha uelewa na kujitambua.

Ushauri.
Ipo haja suala la bima likapewa uzito unaostahili kutokana na umuhimu wake katika ulinzi wa mali na usalama kwa raia. Ni bora kiasi hicho cha bima kingewekwa kwenye mafuta, yani ukinunua mfuta unalipia na bima hapohapo kama tunavyolipia kodi za nyumba tunaponunua umeme TANESCO.
 
Huku bima kule polis kazi ipo

Bima yenyew ni wiz tu haina msaada
Mstari wa pili hapo juu ndiyo tatizo letu...Nina hakika ukifanyika utafiti juu ya bima hizi watanzania wengi tutajibu kama ulivyoandika hapo juu.
........................

Watu wa bima wanatumia nguvu kubwa kukusanya pesa za bima za pikipiki bima ambazo wengi tunaona ni za kijanjajanja au wizi.
 
Back
Top Bottom