Maguge Maguge
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 2,734
- 1,781
Salaam hapa JF!
Nina zigo la maumivu moyoni juu ya hicho kinachoendelea Mtwara!
Habari zinasambaa kwa kasi kwamba kuna mtoto aliyezaliwa, kufumbua macho na kutoa ujumbe kwamba, kuna mvua itakayonyesha maeneo ya Mtawara ikiambatana na wadudu waumao na kusababisha mauti!
HIZI NI HABARI ZA KUTUNGA!
Nasema hivo kwa sababu, Hakuna yeyote anaejitokeza na kuthibitisha kumuona mtoto huyo!
Mwaka 1984 ktk Mkoa wa Kigoma lilitokea tukio linalofanana na hilo;
Ujumbe ulienea kwamba kuna kiumbe kinaingia ndani ya kila nyumba usiku, kikiwakuta mmelala, kitahitaji mzaliwa wa kwanza afe!! pia kwamba wengine waliokuwa usingizini wataota manyoya kama nyani!
Waliokuwepo Mkoani humo,wakiwa na uelewa wakati huo, kama wapo hapa mtanisapoti!!
Nakumbuka nilivyokuwa najiviringisha kwenye Branketi nimeachwa ndani peke yangu kwamba hilo tatizo halinihusu mimi,
watu wazima walikusanyika kwa mabalozi wa nyumba kumi, wakikesha kugongagonga chochote kilichosababisha makelele, Ngoma filimbi, kengere, mapipa majembe, mayowe nk ili mradi kelele zienee eti ndo ufumbuzi wa kufukuza kiumbe hicho!!
Taabu ile ilichukua zaidi ya wiki mbili!!
Nakumbuka maumivu yale na kuwahurumia watu wa mtwara!
Poleni watanzania wenzetu kwa kuzushiwa mambo yaliyopitwa na wakati karne hii ya 21!!