Kinachoendelea huko Pretoria South Africa

Kinachoendelea huko Pretoria South Africa

Hawa ndiyo uliyowasaidia kupata uhuru eti na kuwalaza ardhi yetu kule Mazimbu Morogoro. Ukweli tumepoteza hela sana na sasa hakuna return kabisa. Sasa itabidi na sisi watanzania tuwaze sana hawa wageni tunakumbatia wanauza mpaka yeboyebo kariakoo!! Sidhani kama katika nchi zao tunaweza kufanya hizi kazi. Eti ni wawekezaji!!! Tanzania Investment Centre imeshindwa kazi na ukweli Mh. Rais ninaomba ivunjwe kabisa ianze upya kwa mikakati ya kuhakikisha watanzania wana nafasi kubwa katika uchumi wa nchi hii. Iko siku tatakuwa full manamba katika nchi yetu na siku si nyingi. Subiri wakamate rasilimali zote wawekeze uone jinsi tutahenyeshwa katika kila eneo.
 
Walizoea kubaguliwa na wenyewe wameanza kubagu wenzao.cha ajabu awabagui wazungu. Waafrika tumelaaniwa
 
Walizoea kubaguliwa na wenyewe wameanza kubagu wenzao.cha ajabu awabagui wazungu. Waafrika tumelaaniwa
Baba wa Taifa mwalimu Nyerere alisema ukianza kula nyama ya mtu hutaacha(ukianza ubaguzi hutaacha)utasema hawa ni wabara na hawa ni wazanzibari,hawa ni watanzania na hawa ni wamsumbiji na hawa ni wasouth Mungu atuepushie mbali
 
Upo sahihi kabisa hii mijamaa aijui chochote Kuhusu historia na ni mkaburu alifanya hivo makusudi ili wasijanjaruke aendelee kuwaburuza
Hata serikali ingeweza kuweka mikakati za kuzuia madhara kams haya yasitokee ama kujirudia kwa kuweka sheria kali dhidi ya hawa vijana wanaodhuru wenzao. Maendeleo hayafikiwi kwa akili za wenyeji tu. Mgeni huleta mbinu mbadala ya ufumbuzi wa matatizo. Ndugu zetu hawa wanahitaji waelimishwe.
 
Hata sielewi Nyerere alijihangaisha nini kuwakomboa hawa watu na ukaburu, angewaacha tu wasote na mandela wao
 
Tanzania moja,Africa moja,dunia moja.kwanini hatupendani!?
 
Sio SA tu, hata US Trump nae anakomaa na uzalendo ndo habari ya sasa kwa dunia. Utofauti ni namna ya utekelezaji.

Afu sio lazima kila nyerere aliposaidia lazima Tanzania turudishiwe return. Kurudishiwa return ni utashi tu wa viongozi waliopo mf kwa mawazo yangu baada ya kuanguka ZANU-PF, ANC, FRELIMO etc tusitegemee hata kusikia historia ya Tz na hizo nchi
 
Dhaaa hawa jamaaa

Kama ckosei n last years
Ndo walikua na huu
Ujinga wao wakaja
Wakaacha

Sasa naona wameanza tena
 
Mi nashauri kila mtu asake maisha nchini kwake ngoja nifanye mpango nitoke ureno niwaachie nchi yao
 
Back
Top Bottom