Kinacho muangamiza Lowassa ni Ukimya wake!

lowassa ni mgonjwa hawezi kuongea labda mumtafutie vidonge vya hamu ya kuongea
 
Ukimya upi??
Mbona mouth pieces zake ziko loud kabisa??
Kama unabisha muulize ocampo four.
 
Last edited by a moderator:
Haya yooooote uliyoandika ni siasa!! na mimi sio mwanasiasa!! hiyo sentensi ya mwisho ndiyo point ya msingi!!! mafisadi hawakubaliki tanzania na duniani kote.
 

Too late. Hata akifunguka leo nani atamwamini? Ili aonekane mwadilifu ilimbidi kufunguka wakati ule.
 
Tatizo la vijana wa Joka la mdimu ni wachanga na mwana mfalme anayewaongoza naye anayomatatizo makubwa. Lowassa mtamsema sana lakini siku moja ukweli Wa Richmond utajulikana tu. Na haya mapanga mnayo yanoa uko siku moja mtayatumia dhidi yenu wenyewe. Hofu kubwa ya wengi ni wako traumatized na wanaugua homa ya Lowassa (Lowassa Fever) inayosababishwa na virus uoga. Uoga huu unatokana na dhambi ya kisiasa ilotendwa na baadhi ya myopic CCM cadres dhidi ya Lowassa. Ndiyo dhambi dhidi ya mwamba Lowassa. Ndiyo mkitaka kujua kuwa yeye huko hatua ya mbali kwenye mbio za nyika dhidi ya mahasimu na wapinzani wake Wa kisiasa, kila kuchao jina lake linazidi kutatajwa. Wa kubwa Lowassa, watoto Lowassa, dini zote Lowassa.

Dawa ya wanaougua homa hii ya Lowassa siyo mizegwe. Bahati mbaya sana hakuna tiba ya homa hii, zaidi kinachoweza kufanyanyika ni kuzuia isienee Kwa kukubali ukweli kuwa Lowassa hazuiliki tena!

Lowassa nakuomba tangaza nia ili watu wapone homa yako. Uliposema "tatizo ni uwaziri mkuu" ulikosea tatizo lilikuwa ni urais 2015. 2015 ndiyo hii hapa. Kwa heshima kubwa naomba tangaza nia watu watapona homa ya Lowassa. Wanaugua homa hii zaidi ni wakubwa ambao wanaotaka kutumia mizengwe kukabiliana nawewe lakini hawakuwezi. Kwa nini hawakuwezi? Kwa sababu watanzania wengi wanamtala Lowassa wao. Waamuzi ni watanzania, na wengi wa wao wanamhitaji Lowassa! Najua wengi wataamua sahihi Kama walivyoamua watu wa Sumbawanga majini walivyo amua CHADEMA tosha.
 
siri ya nini, EL ni mpuuzi Fulani tu, mpaka akishgulikiwa ndo anatishia kusema ukweli basi ni fara Fulani tu ambaye hana mapenzi na TZ bali tumbo lake na familia yake

Mkuu hapa umemkosea sana EL, sasa nikuambie miongoni mwa wazalendo wa nchi hii ni EL, kuwahi kuitafuta pesa kwa kufanya biashara isiwe dhambi. Mpaka sasa hivi mmeshindwa kutengeneza katiba bora ya namna viongozi wanaweza kuendesha biashara zao pasipokuwa na mgongano wa kimaslahi. Nahisi kama ni kosa kubwa basi ni yeye kuwahi kufanikiwa kifedha. Kafanya mengi sana mazuri hata kuliko hao wanaojiliza bungeni bila hata kuchukua hatua. EL ni mtu jasiri na mwenye kufanya maamuzi magumu, labda nikujulishe kuwa miongoni mwa watu wanaokubaliwa na wanyonge ni EL. Sishabikii siasa ila huo ndio ukweli na ikitokea akateuliwa basi jua kazi itakuwa nyepesi sana ccm kuliko wengi mnavyodhali. Hakika huu ni ukweli unaouma.
 

Mkuu labda nikukumbushe tuu kwamba EL hakupigwa chini bali alijiuzuru, kujiuzuru ni ku-respond kwa kuguswa na sakata zima hata hivyo hii isifanye jamaa ahukumiwe kiviile. Kwahiyo ni bora hao ambao hawajiuzuru ili waendelee kuonekana wasafi?
 
Lowasa ni mgonjwa Kama mjuavyo wagonjwa hawapaswi kusema Sana
 
Mkuu labda nikukumbushe tuu kwamba EL hakupigwa chini bali alijiuzuru, kujiuzuru ni ku-respond kwa kuguswa na sakata zima hata hivyo hii isifanye jamaa ahukumiwe kiviile. Kwahiyo ni bora hao ambao hawajiuzuru ili waendelee kuonekana wasafi?

Waziri Mkuu hajihudhuru bila maelekezo ya RAIS, labda huna uwezo wa kuunganisha dots, that is the fact. Yaani tulimfukuza kijanja ili wenye akili ndogo wasijue kafukuzwa aibu ikawa kubwa. Sasa wewe uko pande ipi ya akili?
 

Ujasiri wake upo kwenye kukwapua mali za umma kwa mikataba mibovu ya richmond, hilo tunakubaliana wote. Ujasiri wake mwingine ni kusema anayosiri kubwa, yaani nchi inahaki ya kujua iwapo ametunza siri kwa mambo ya kitaifa huyu ni jambazi wa umma, fedha kuwa nazo sio dhambi suala ni amezipataje? Nyerere alihoji na EL hakuwahi kujibu utajiri wake kaupata vipi? BUNGE LIKISEMA MWIZI UJUE NI MWIZI au huamini BUNGE???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…