Kinacho endelea sasa TBC live "KONGAMANO"

Kinacho endelea sasa TBC live "KONGAMANO"

Watu wanaoitetea Tanganyika wakiwa wanaongea wanakata mawasiliano. Mfano kabudi alipoanza kuongea wakatoka hewani wamerudisha kashamaliza.
 
TBC wanapata tabu sana kwa kuukataa ukweli na itafikia siku hata kupata habari kwao itakuwa tabu sana
 
Tena zilikuwa ni nondo za usoni, maana Prof. Kabudi alikuwa anaongea kwa ujasiri usio wa kawaida mbele ya Makamu Rais wa JMT kwamba muungano tulionao umechoka na tusilazimishe vizazi vijavyo vikaishi kwa ujinga wetu. Aisee, ilikuwa ni balaa. TBC1 kama kawaida yao walivyoona nondo za usoni zinazidi wakakata matangazo. Aibu kubwa kwa TBC!

kiukweli leo nimekubali kuwa tume ilijaa weledi wa hali ya juu. Tbc kwa kweli mh
 
sasa ni wakati muafaka wa kufanya kitendo kwa hii Tbc inayoendeshwa kwa kodi zetu wote
 
Eti bado wako lunch time tu au TBC hawajapata walichokuwa wanataka walizani Pro. Kabudi ni kama yule anaye geuka geuka kila kukicha? mbona hawasemi chochote, Je kongamano limeisha au?
 
TBC1 sasa, wakiona mtu anashusha NONDO wanatoka hewani, miye nipo Mza vipi huko Dar mvua inanyesha tena? Maana siku ya Tundulisu Dodoma walisema mvua ilikatisha mambo.

ni matope ndo yamesabisha mitambo ikakatika...sio kosa letu samahani kwa usumbufu.ndugu wa tanganyika
 
Hivi ni kwanini shughuli muhimu kama hizi zirushwe na tv moja kama tbc? Kwanini wadau wengine wasialikwe??
 
PROF.KABUDI katoa fact,amesema muungano una FATIQUE kusema ukweli,mwisho wa kunukuu.alipotamka hivyo TBC wakakata mitambo yao.
 
Wakuu tunaweza mfuatilia prof. Kabudi yuko live sasa naona anafafanua masuala mbalimbali ya kikatiba. Amesema muungano wa mkataba unavunja muungano.

kabudi mccccccccm damu ni proccccccmmm pure hana lolote
 
Safari hii TBC watasingizia nini?

Bahari ilichafuka ndo maana matangazo yalikatika. Yaani frequency zilikuwa zinaishia chumbe tu sbb ya mchafuko huo.
 
kiukweli leo nimekubali kuwa tume ilijaa weledi wa hali ya juu. Tbc kwa kweli mh

Kaka ujue bado tunamatatizo ya kuamini kama watanzania wa leo ni wa kidigitali na si wa kianolojia,bado hatujaamini ndiyo maana tunajifanya ngangari.

Wale wazee wazamani walisema "Ukipigana na Ukuta........."
 
Back
Top Bottom