Kinacho endelea sasa TBC live "KONGAMANO"

Kinacho endelea sasa TBC live "KONGAMANO"

Kabudi alikuwa anawachana live, amesema tusilazimishe watoto wa miaka hamsini ijayo kuishi ujinga wetu. Amesema hakuna Muungano kisheria bali kirafiki. Makombora yamezidi Tbc wakakata matangazo!!!!
 
Prof. Kabudi kawaambia muungano huu wa sasa uko katika hali ya fatigue (umechoka). Akaendelea kusema ni lazima tuangalie tear and wear za muungano. Baada tu ya kuzungumza maneno hayo TBC1 wakakata matangazo.
 
Bora TBC ilipuliwe tu isiwepo. si busara kuweka Taraab za vijembe kuhusu muungano bila hata kutoa sababu za kukata mjadala.
 
Prof. Kabudi kawaambia muungano huu wa sasa uko katika hali ya fatigue (umechoka). Akaendelea kusema ni lazima tuangalie tear and wear za muungano. Baada tu ya kuzungumza maneno hayo TBC1 wakakata matangazo.

Nadhani waliona anaenda wasikokutaka!
 
ila tbc inatia aibu sana..... nasubiria hii taarabu ya muungano iishe labda wataturejeshea mawasilano!
 
Taarabu live ndo kongamano??? me naona wanaonyesha taarabu ....Isha Mashauzi anakata mauno huyo kudadadadeki!!!.
 
Wameweka taarabu ndio wanachofikiria tunakipeenda haya nimekubali....uzuri ujinga wa mwenzio haukufanyi wewe kuwa mjinga. Kwa maneno ya mtaani kivyao vyao....

Duh tbc mpaka najisikia kichevu chevu .wanasheria watusaidia kama kuna uwezekano wa kumchukulia hatua za kisheria huyu .mkuregenzi wa tbc Mshana kwa kosa la kugeuza tbc kuwa chombo cha ccm .
 
Kabudi alikuwa anawachana live, amesema tusilazimishe watoto wa miaka hamsini ijayo kuishi ujinga wetu. Amesema hakuna Muungano kisheria bali kirafiki. Makombora yamezidi Tbc wakakata matangazo!!!!

Aise kumbe ndio maana wamevunja tume ya katiba .kwa maana kwa maelezo ya Kabudi serikali 3 ni lazima .hakuna jinsi ccm wanaweza toa hoja ikashinda .
 
Hivi tbc bado mnaona mnayohaki ya kutuchagulia habari na kuamua kutukatia matangazo??? Dawa yenu iko jikoni. Sasa sisi tunafuatilia maelezo ya kina kuhusu muungano kutoka kwa wataalam nyie mnatukatia!
 
Itakuwa mkuu, mambo ya kuficha ficha taarifa haya.

Prof Kabuni ni hazina kubwa sana katika nchi hii nimefuatilia namna anavyowasilisha mada na hao wengi. mtazamo wangu ukiifahamu kweli itakuweka huru kweli kweli
 
Back
Top Bottom