Kina Nani wanaorudisha pesa za EPA?

ni kweli nakubaliana na wazo kuwachochote chaweza kutokea Tanzania... lakini... JK alitangaza kuwa maagizo yake ni kwamba serikali itarudisha pesa, then itawa prosecute wahusika wote... This is what i want to c.kwanza... wafunguliwe mashtaka ya fraud, conspiracy to defraud, money laundering, theft, tax evasion... HAPO ndio tutajua kama kuna lolote.. Its very likely kuwa hamna kitakacho endelea.. lakini bila mashtaka hata kama yakuzugia...wazungu hawawezi KUTUCHUNIA ALAFU WATUPE HELA TUU TENA.. itabidi wachache wafungwe na wengine wale fine, wafilisiwe.. sasa hapa waliombali na JK ndio watachinjiwa baharini... wale maswahiba watachuniwa kiaina design... tungoje

Just wait in few days, watatoa majina yasiyojulikana (ya kutengeneza) na kusema kuwa ndiyo wamehusika na wizi huu na kuwa serikali imeiomba Interpol kusaidia kuwakamata. Majina yatakuwa kama ifuatavyo:

1. Urio Mangi - mkazi wa manzese Dar
2. Katayange Mwakipura - Mkazi wa Mwananyamala
3. Khirma Indighrayamavi - Mkazi wa Kariakoo....

na kadhalika!
 
Just wait in few days, watatoa majina yasiyojulikana (ya kutengeneza) na kusema kuwa ndiyo wamehusika na wizi huu na kuwa serikali imeiomba Interpol kusaidia kuwakamata. Majina yatakuwa kama ifuatavyo:

1. Urio Mangi - mkazi wa manzese Dar
2. Katayange Mwakipura - Mkazi wa Mwananyamala
3. Khirma Indighrayamavi - Mkazi wa Kariakoo....

na kadhalika!

Pamoja na machungu niliyonayo kuhusu hili jambo; lakini hapa MWk umenichekesha sana. Nilikuwa ninahuzuni lakini sasa siku imekuwa walau nzuri kidogo. Ngoja tusubiri hayo majina. Tutaona usanii mwingine hapa.
 
Pamoja na machungu niliyonayo kuhusu hili jambo; lakini hapa MWk umenichekesha sana. Nilikuwa ninahuzuni lakini sasa siku imekuwa walau nzuri kidogo. Ngoja tusubiri hayo majina. Tutaona usanii mwingine hapa.

Unajua muda mwingine inabidi utafute kitu cha kucheka maana haya mambo yanayoendelea hapo nyumbani yanatia hasira na uchungu sana.

Majina zaidi ni:

4. Kisakuri mwopombe - mkazi wa Tandale
5. Majiyairinga Majiyatanga - mkazi wa Kyela - Mbeya!
 
Tuna mfumo wa ubaguzi wa sheria ambayo naona unapply kwa wakubwa na watu wadogo kitofauti!

Angalia hata leo Ditto aliua mtu na yupo na anafanya biashara kuuza asali na JK anaona kwa vile ni rafiki yake ni poa tu!

Nachoweza kusema.. Tz ukiiba kuku ni lazima utafungwa tu ndugu yangu!


Nakuunga mkono juu ya hoja yako kwamba TANZANIA KUNA MFUMO MATAPISHI WA UBAGUZI WA SHERIA UNAOWAPENDELEA VIONGOZI WA SISIEMU.

Watanzania tulipeleka ndugu zetu kupigana huko Afrika ya Kusini ili kupambana na mfumo wa Ubaguzi wa rangi chini ya Serikali ya Makaburu wa Afrika ya kusini.
Tumepoteza muda wetu,rasilimali zetu na uelekeo wetu wa kufikiri kwa sababu ya kupinga mfumo huo wa ubaguzi wa Rangi.

Ina maana tulifanya kazi bure???

Leo hii Chama cha SISIEMU chama chenye historia ya kupinga ubaguzi wa namna yeyote ile Afrika na kwingineko duniani kimekengeuka na kuikumbatia siasa matapishi ya Ubaguzi.
Sheria zetu zinatumika kwa namna tofauti kwa watu tofauti juu ya makosa ya namna moja.
MWizi ni mwizi.
Tendo la wizi likifanywa na Waziri ni wizi.
Tendo la wizi likifanywa na Askofu ni wizi
Tendo la wizi likifanywa na Mufti ni wizi.
Mkuu wa mkoa akiua ni kosa la jinai
Jambazi akiua ni kosa la jinai
Hata Rais akiua ni kosa la jinai( Japo katiba ya Sir Richard Turnbull inamlinda)
Mtuhumiwa wa wizi siku zote anashitakiwa chini ya sheria ya jinai na ni lazima afikishwe mahakamani kujibu mashitaka ya tuhuma za wizi.
Ni Mahakama pekee yake ndiyo yenye mamlaka ya kuamua mwizi huyu afanywe nini.
Rais wa nchi,Waziri,Mwanasheria mkuu au kiongozi yeyote ndani ya serikali hana mamlaka ya kuamua mwizi afanywe nini.
Zaidi hawana mamlaka ya kuamua kilichoibiwa kifanywe nini. Ni kinyume cha sheria mtu au kikundi au cha cha siasa kuchukua majukumu ya mahakama kwa kisingizio chochote kile.

Kitendo cha kuwaruhusu Viongozi wa serikali na watu wengine wajionao maarufu kurudisha fedha moja kwa moja mahali wanapotuhumiwa kuiba ni kinyume cha sheria zaidi ni UBAGUZI WA KISHERIA NCHINI TANZANIA.
Wezi wa kuku,mbuzi,ndoo,mikungu ya ndizi na mahindi mabichi na wezi wa mifukoni na wezi wengine wote wasio vingunge tunajua wazi kwamba kamwe serikali ya sisiemu haiwezi kuwapa starehe hiyo ya kurudisha fedha na kuendelea kutembea kifua mbele.

Kitendo hiki zaidi ya kuwa ni cha kibaguzi na kikaburu kinazusha maswali mengi
Je ni kweli fedha zinarejeshwa?
Kwa nini wezi hawa wa mabilioni hawashitakiwi?
Waziri mkuu kajihudhuru kwa wizi wa wazi je hii si dalili kwamba viongozi wakuu wote wa serikali wamo kwenye wizi wa EPA sasa wamejipa kinga ili wasichukuliwe hatua?
Tunajuaje fedha hizi si zile za makusanyo ya kawaida ya kodi ambazo serikali imeamua kuweka huko kwenye fuko la EPA ili kuhararisha wizi wa fedha za EPA?

Hivi leo nikichukua Tinga Tinga au TNT na kwenda kubomoa kuta zote za Gereza la ukonga ili niwaachie vibaka na wezi wa kuku kosa langu chini ya utekelezaji wa iana hii wa sheria litakuwa nini?

Ni kiasi gani cha chini ukiiba sheria ya wizi Tanzania inakubana ili wananchi wote tujihadhari kuiba fedha ndogo ndogo?

Kuna mtu au kundi la watu au chama nchini Tanzania ambacho kiko juu ya sheria?

Watanzania tuko wapi kupinga Ubaguzi huu wa sheria unaowapendelea Viongozi wa serikali wafanyao makosa ya jinai,tena hadharani?

Hivi Watanzania tunadhani kuna mtu atakuja kupigania haki zetu kwa niaba yetu?


SAA YA UKOMBOZI NI SASA NA WAKOMBOZI NI MIMI NA WEWE.
 
Unajua muda mwingine inabidi utafute kitu cha kucheka maana haya mambo yanayoendelea hapo nyumbani yanatia hasira na uchungu sana.

Majina zaidi ni:

4. Kisakuri mwopombe - mkazi wa Tandale
5. Majiyairinga Majiyatanga - mkazi wa Kyela - Mbeya!

hapa umenichekesha kweli
 
Ninachojiuliza ni sababu gani wanazotoa zilizopelekea wao kurudisha hizo fedha?
 
Bado swali halijajibiwa
Ni akina nani wanarudisha hizo hela??
Walimu wanalalamika mishahara, kumbe kuna vyura wanaomeza,
Madaktari wa mhimbili wanatoa rufaa kwenda hospitali binafsi hii yote ni kwa kuwa mishahara yao haikidhi viwango.
Polisi wamekubuhu kwa rushwa na ubambikiaji kesi kwa sababu hawalipwi vizuri,
Wanavyuo wanagoma kuingia madarasani kwa kuwa bodi ya mikopo haiko fair kutoa mikopo kwa wakati, Hii inaonesha kuwa mito ya maji inakimbilia jangwani na inapotelea mchangani pasipo na rutuba yeyote. Lazima tusikubali kutamalikiwa na lazma tuupige vita ufisadi kwa gharama za maisha yetu.
Jamani mwenye data atupatie wakuu. Au serikali ilifaulu kututisha kwa kuwakamata Mods wetu?? Tusikubali, lazima kundumbwendumbwe kiimbwe......
 
Kwa nini asijitokeze mwanaJF mmoja naye akaenda na kusema kuwa anarudisha pesa kwani zilichukuliwa na bibi yake ili tuweze kuijua ukirudisha unaambiwa kitu gani.

Hapo ndipo tunaweza kuanza kupata ukweli juu ya hizi pesa zetu na wanaozirudisha wanakutana na nani na wanazirudisha kwa nani, na kama wanapewa risiti kuwa zimepokelewa ama kunatokea kitu gani hapo.
 
Back to our roots...

Kwani jamani hamjui kwamba hapa wazee wameshikwa pabaya??? hizo pesa ni hao wenyewe walizichukua... na ndizo zilizowaweka madarakani...... Lowasa yeye amekuwa "Kilongola" wa dhambi kwa kujiuzulu.
Unadhani nani yeye atabeba msalaba kwa kujisema amechukua? na nani atamtaja? Unadhani katika hao nani atakubali yeye ndio aende jela?

Ila tuwasubiri wanaendelea kujadiliana.
 
wamegundua makosa yao na kuamua kujirudi na kuonesha uzalendo wao..


Mwanakijiji naomba unisaidie hivi nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya sheria au sasa imekuwa kama nyumba ya mtu ambapo mtu una option ya kuamua kumwagilia maua yako au lah ! What is wrong with Tanzanians ? Why we keep electing these idiots who don't have testicular fortitude to enforce our laws .

CCM leaders are living in delusional, they think the public is so uninformed and will buy every crap they are going to throw. It is imperative for them to understand that CHEO NI DHAMANA but more importantly they were elected to defend our constitution and not manipulate it. Enough is enough, it is mandatory for these lame ducks to enforce our laws by arresting all who were involved in that scam and allow the due process to take its course.
 
Kwa mtizamo ni kwamba kama JK ni mtoto wa mjini lets wait and see. Maana tunaambiwa kwamba tume iliyoundwa kufuatilia imeingia mkataba na hao mafisadi ili warudishe hizo hela kwanza. Then JK kwa kutumia utoto wake wa mjini atawageuka wote na kuwakamata.
 
We mzalendo mbona unaanza kutushtua wengine tena. Ila hilo unalosema mpaka kieleweke ni hoja nzito sana ambayo kimsingi ni hoja ya kisheria.

Mzee Mwanakijiji, naamini kuwa sheria ya Tanzania haisemi kuwa inatumuka kwa watanzania wenye hadhi fulani au watanzania wenye hali fulani. Hili suala naona sio la kisheria bali linahusu utekelezaji wa Sheria. Tumeona kuwa Kiongozi akiua hata kukamatwa ni vigumu, acha kumwadhibu kisheria, na sasa tunaona kuwa Kiongozi akiiba hata kutajwa hatajwi, hata akirudisha alichoiba jina lake halitajwi.
Hili si jipya kwa Tanzania. Mnyonge hana haki, labda mwenye nguvu apende. Kwa hiyo walala hoi wakifanya uhalifu basi wanaishia jela na kuadhibiwa, lakini hao kina EPA wanaendelea kupeta na tena wanaendelea kulindwa. This is how it is.
Kuna siku Mzee Makamba alikuja Loyola alisema Mwamvua akifukuzwa shule baba yake atakuja atapanda gari na ataondoka naye na kwenda pazuri zaidi, lakini kina kapuku mkifanya hivyo, mnaweza kuwa wa kutupwa, that is the reality.
Kwa hiyo sio sheria ni hali halisi na utekelezaji wa sheria zilizopo!
 
hao wanaorudisha pesa za EPA wanarudisha wapi na wanarudisha kwa njia ipi?
cash? hundi?
na wamejuaje warudishe wapi iwapo haijatangazwa?
na kama mimi ni mmoja ya wezi wa EPA lakini jina langu kwa bahati halikutajwa, na nimeingiwa na imani nataka kurudisha pesa, nifanyeje?
hawa serikali wanachekesha kweli kweli, wanafikiri bado tupo katika kipindi cha kuitikia tu kila wanachokisema!1
 
Back
Top Bottom