Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,575
Kwa masikitiko makubwa sana nashindwa kuamini kile kinachoendelea kwenye taifa hili eti kuna mtu ama watu wanaweza kutuibia mabilioni ya pesa na kisha wakigundulika wanaambia warudishe na hakuna hatua zinachukuliwa wala hata kuwataja ni nani hao inakuwa jinai.
nitaweka mifano michache kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari juu ya watanzania hawa walivyofanywa kwa kosa la wizi.
1.Mkazi wa Dar alifungwa jela kwa kuwatoroka Askari polisi, na alikuwa anashtakiwa kwa kumdhalilisha mtu, basi akafungwa miezi 6. (Mwananchi 32/2/2008)
2.Kondakta afikishwa polisi na kutozwa faini baada yakukosa sare za kazi(kulikoni 25/2/2008
3.Afungwa miaka 30 kwa kupatikana na hatia ya wizi wa sh 250,000/= (mwananchi 2/2/2008
4.Mkazi wa Buguruni atinga mahakamani kwa wizi wa cherehani, wakati huo huo mkazi wa kiwalani amefikishwa mahakamani kwa kujipatia kilo 250 za mchele kwa udanganyifu (mwananchi 21/1/2008)
Ukiangalia mtiririko wa matukio hapo juu unaweza kujiuliza kama mtu anaiba mchele , mwingine anaiba mabilioni hata hafikishwi ama kuhojiwa na polisi huku ni kututukana watanzania.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema , namnukuu Fikra nzito hazifi kwa urahisi hivyo, zinabaki zikikera na kila jamii ya binadamu katika historia inajipalia makaa kwa kuzipuuza fikra hizo” (Mwalimu Nyerere 22/10/1987).