‘kimobitel’ arudi nyumbani twanga pepeta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘kimobitel’ arudi nyumbani twanga pepeta

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Feb 8, 2011.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  MKURUGENZI wa kampuni ya African Stars Entertaiment (Aset), Asha Baraka, leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mwanamuziki Khadija Mnoga (Kimobitel) ambaye ameamua kurejea katika bendi yake ya Twanga Pepeta.

  Akizungumza katika ofisi za Aset zilizoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam mara baada ya kumtambulisha msanii huyo aliyetokea bendi ya Extra Bongo, Baraka alisema kuwa Kimobitel ameamua kuejea katika bendi hiyo baada ya kuchoka na kile alichokiita “ubabaishaji” katika bendi hiyo ya awali iliyo chini ya mwanamuziki Ally Choki.

  “Nimeamua kurudi nyumbani kwani sikufukuzwa na mtu yeyote ndani ya Twanga Pepeta. Niliamua tu kupumzika. Mbaya zaidi, kule nilipotoka kumezidi sana tabia za ubabaishaji,” alisema Mnoga.

  Wakati huohuo, Asha Baraka amewatambulisha waimbaji wengine na uongozi mpya wa bendi hiyo tangu kifo Abuu Semhando, aliyekuwa meneja wa bendi hiyo.

  Mwimbaji mwengine aliyejiunga na Twanga Pepeta akitokea Bagamoyo Sound, Venance Joseph, akiwa katika pozi mara baada ya kutambulishwa.

  Meneja wa Aset, Martin Sospeter, leo ametambulishwa rasmi kuwa ndiye mrithi wa aliyekuwa meneja wa bendi hiyo marehemu Abuu Semhando.
   
 2. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  @lutala,peleka jukwb la sports and entartainment ndio pake huku umebaka venue ,pliz move
   
 3. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mshaanza mashabiki wa Ali Choki. Sitawabaka tena kwenye venue yenu
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hiimkuu mbona kama ni entertainment issue???? :twitch:
   
Loading...