Kimenuka Ufipa, Makao Makuu yahamia Mikocheni kinyemela

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Wakuu, kama mnavyojua makao makuu ya chama chetu yako hapa ufipa, lakini katika hali ya kushangaza ndugu Edward Lowasa amegoma kutumia ofisi hizi pale anapotekeleza majukumu ya kichama na badala yake kazi za kichama kahamishia ofisi yake binafsi iliyoko Mikocheni ambayo haina hata bendera ya chama.

Mpaka sasa mikutano yote ya kichama ambayo inamuhusu Lowassa inafanyika huko Mikocheni, hata maalim Seif alipokuja kuonana na bwana Lowasa kama mgombea wa UKAWA, alienda huko mikocheni, Juzi wazee wa Dar es Salaam walipoenda kumtembelea mgombea urais wa chadema (Lowasa) walienda huko Mikocheni.

Huyu tuliyemkabidhi ugombea kagoma kabisa kutumia ofisi ya chama, na amekuwa akihamishia mikutano na vikao vya chama kufanyika katika ofisi yake binafsi ambayo haina hata bendera ya chama. Hapa ufipa watu hawaji tena.

Yani tumebaki sisi makamanda na meza zetu tu, wanachama wote wanaelekea hukoo mikocheni, hata baadhi ya makamanda wameanza kureport huko.

Hali ni tete wakuu.
 
Kama ni kweli una uchungu na hayo uliyoandika na ni kamanda wa kweli, peleka malalamiko yako kwa wahusika hapo Ufipa. Hapa utaonekana unafanya porojo tu!
AMsikilize nani?sasahvi ataitwa msaliti...infact luwasa kashanunua cdm.mbowe na mtei wamebaki na parcent ndogo sna sidhani hata kumi itafika
 
Lowasa hakuwahi kufanikisha lolote kitaasidi kwenye utendaji wake. Anajijenga binafsi,siyo taasisi,mwenye kinyongo na kulipa kisasi.CCM walimtema kwani alijiona mkubwa kuliko CCM,kumbuka mafuriko ya Monduli,rejea ya Dodoma wajumbe kuimba kuwa wana imani na Lowasa,siyo CCM,baada ya kukatwa. CDM kinamalizwa na huyo mmeru,hana ubunifu ili kupambana na wakati.
 
Lowasa hakuwahi kufanikisha lolote kitaasidi kwenye utendaji wake. Anajijenga binafsi,siyo taasisi,mwenye kinyongo na kulipa kisasi.CCM walimtema kwani alijiona mkubwa kuliko CCM,kumbuka mafuriko ya Monduli,rejea ya Dodoma wajumbe kuimba kuwa wana imani na Lowasa,siyo CCM,baada ya kukatwa. CDM kinamalizwa na huyo mmeru,hana ubunifu ili kupambana na wakati.
WACHACHE WENYE UELEWA HUO.luwasa huwa ni mbinafsi nahuo ubinafsi wake ndyo mana kanunua cdm mbowe pale nikm meneja tu.mtei mzee wa ushauri.maskini cdm tulikulea ukakua leo umeharibika kwa tamaa za wachache...hujui hata unasimamia wapi sera yako yaufisadi imebakwa leo hata chenge anakemea ufisadi..pole sna cdm
 
Kwani Lowassa ana wadhifa gani ndani ya CHADEMAmpaka alazimike kutumia ofisi za ufipa?
shughuli zozote za kichama lazima zifanyike katika ofisi halali ya chama, pia lowasa alikuwa ni mgombea wa urais kwa tiketi ya chama, hiyo peke yake ina mqualify kuwa senior official wa chama
 
Kwani Lowassa ana wadhifa gani ndani ya CHADEMAmpaka alazimike kutumia ofisi za ufipa?

mkuu, kwani lowasa alikuwa na wadhifa gani mpaka tukampa nafasi ya kuteua wabunge 10 wa viti maalumu atakaopenda yeye?? na lini mwanachama wa kawaida, asiyena wadhifa wowote aliwahi kupewa nafasi kama hiyo katika historia ya vyama vingi hapa nchini from 1992
 
Back
Top Bottom