Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 491
- 781
Taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuamika ndani ya Chadema, leo Jumatatu Asubuhi, Juni 01, 2026, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza atafika Makao Makuu ya Chadema (Edwin Mtei House), Mtaa wa Daima, Mikocheni Dar es Salaam.
Nitaleta taarifa zaidi kuhusu kitakachoendelea.
Mnyika: Ujio wa Nyahoza ofisi za CHADEMA unalenga masuala ya kijinsia, si barua ambazo amekuwa akituandikia
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amefika katika ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA (Edwin Mtei House), Mikocheni, Dar es Salaam, leo Juni 1, 2026, kwa ajili ya kikao na uongozi wa chama hicho.
Akizungumza kabla ya ujio wake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kuwa Ofisi ya Msajili iliwaandikia barua tarehe Aprili 28, 2026, ikiwajulisha kuwa ingetembelea ofisini hapo kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa sera ya dawati la kijinsia.
Mnyika amesema kuwa kumekuwa na taarifa za upotoshaji zikidai kwamba Msajili anafika katika ofisi hiyo kwa ajili ya kujadili barua zilizotolewa na ofisi yake kuhusu masuala ya maadili.
Ikumbukwe kuwa Gazeti la Nipashe limenukuu kauli inayodaiwa kuwa ya Naibu Msajili ikieleza kwamba:
“Ndiyo maana nimesema kuwa kama kutatokea kosa jingine, tutawashughulikia kama kawaida. Ndiyo maana hata kesho (leo) saa tano asubuhi tutawatembelea ofisini kwao; tuna mambo ya kisheria ambayo tunakwenda kuelimishana.”