Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,988
Hali ya kisiasa wilayani Tarime inazidi kuwa tete baada ya jana mwenyekiti wa Chadema wilayani humo kuandika barua polisi kusitisha mikutano ya mwenyekiti wa BAVICHA John Heche. Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba kamanda John Heche anasakwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya kwa tuhuma za kumkashifu raisi Kikwete.
Katika mkutano wake wa juzi alioufanya katika mji mdogo wa Sirari, Heche aliwaeleza wananchi kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ombaomba wakati ina rasilimali nyingi sana za kuiwezesha kujitegemea. Akawaeleza wananchi hao kuwa raisi Kikwete ndiye anaongoza zoezi hilo la kuwa ombaomba, kwa kwenda ulaya na marekani kila mara kutembeza bakuli.
Heche alielezea masikitiko yake kwa raisi Kikwete kupishana angani na ndege zilizojaza madini yetu kupeleka ulaya na marekani huku yeye akiwa amefungashiwa vyandarua na hao wazungu wanaopora rasilimali zetu. Bado nafuatilia kujua hatma ya sakata hili na nitaendelea kuwa update kadri inavyowezekana.
UPDATES 2:
Taarifa rasmi kutoka Tarime ni kwamba Kamanda Heche amefika kituo cha polisi Tarime kama alivyoitwa na kaimu kamanda wa Tarime Rorya lakini amegoma kuhojiwa hadi atakapokuwa na wakili wake. Kufuatia hali hiyo uongozi wa jeshi la polisi umekubaliana nae na kumpa muda hadi kesho saa tisa afike na wakili wake kwa ajili ya mahojiano.
Kwa upande mwingine Heche anaendelea na mikutano ya hadhara kjama kawaida na muda huu anaelekea eneo la Muriba kuzungumza na wananchi. Zengwe lililokuwa limewekwa na mwenyekiti wa wilaya limeshindwa na sasahivi mwenyekiti huyo anahaha huku na kule asijue hatma yake itakuwa ni nini.

UPDATES 1:
Nimezungumza na kamanda Heche muda mfupi uliopita, amenifahamisha kwamba amepigiwa simu na kaimu kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime Rorya ili afike kituoni kwa mahojiano.
Sasahivi ndio anaelekea kituo cha polisi Tarime mjini kwa ajili ya mahojiano hayo.
Taarifa za ndani kabisa toka polisi Tarime ni kwamba kuna shinikizo/maelekezo toka juu kwamba Heche akamatwe ama akijisalimisha azuiliwe mahabusu ya polisi hadi kesho atakapopandishwa kizimbani.
Nadhani wale mliopo Tarime mnaweza kufuatilia kwa karibu na kutujuza kinachojiri huko.