Kimbembe cha VAT: Wawekezaji wanaondoka!!

Kimbembe cha VAT: Wawekezaji wanaondoka!!

VATI INALIPWA NA MRAJI KWANINI KAMPUNI IFUNGWE

Bei ya bidhaa inapanda hivyo mauzo yanapungua, kuna watu wataona bora kutengeneza wenyewe pia kuna viwanda vingi vidogo vidogo kama hivyo vya kuku ambavyo mkono wa TRA haufiki, watauza bila VAT hivyo bidhaa zao zitauzwa asilimia 18 chini ya bei na wateja watahamia huko.
 
Hizi habari ndio huwa Furaha kwa majizi Chadema..

Kwa taarifa yenu hata abaki muwekezaji mmoja nchi nzima lazima alipe kodi
Unakinena usichokijua, we unafikiri nchi inaendeshwa kwa kuwatoza kodi wauza vitumbua? Hii issue ni serious
 
Wadau, habari za majukumu! Baada serikali mpya kuingia waliingiza VAT kila sehemu hata kwa waliosamehewa kodi hiyo, nasemea upande wa watengenezaji chakula cha kuku! Kampuni ya thailand CPF wanafunga operation na kuondoka mwisho wa mwezi huu!! Nawasilisha

Bora waondoke kuliko kuchuma pasipo kulipa kodi, kuwepo kwao siyo hisani, kama watumishi wa umma wanalipa kodi how come mwekezaji tena foreigner asilipe kodi
 
Hao watakuwa walikuwa waki-survive kwa kukwepa kodi. Sasa udhibiti umekuwa mkali mambo hayaendi, inabidi kufunga duka.

Waende salama. Tutabaki na wawekezaji ambao ni walipa kodi. Mradi wenyewe hata vijana wa kijiweni wanaweza kuuendesha.
 
Wadau, habari za majukumu! Baada serikali mpya kuingia waliingiza VAT kila sehemu hata kwa waliosamehewa kodi hiyo, nasemea upande wa watengenezaji chakula cha kuku! Kampuni ya thailand CPF wanafunga operation na kuondoka mwisho w mwezi huu!! Nawasilisha
Yaani kutengeneza chakula cha kuku tulete watailand? Let them go! Watanzania hamjui hata maana ya wawekezaji. Kama unaweza kulima mwenyewe utakuwa mjinga kutafuta mtu wa kumkodisha ili akulipe ushuru badala ya kulima mwenyewe ukapata faida zaidi. Shughuli tunazoweza kufanya serika wenyewe serikali iweke mazingira magumu kwa wageni na bidhaa za nje na kuwawezesha watanzania kuzalisha wenyewe. Hiyo ndio mikakati ya kiuchumi sio kukalili wawekezaji hata sehemu zisizo
 
Wadau, habari za majukumu! Baada serikali mpya kuingia waliingiza VAT kila sehemu hata kwa waliosamehewa kodi hiyo, nasemea upande wa watengenezaji chakula cha kuku! Kampuni ya thailand CPF wanafunga operation na kuondoka mwisho wa mwezi huu!! Nawasilisha

Akiondoka chukua fursa maana hvyo viwanda hata mtanzania yoyote yule anaweza kuzifanya ,hata na hivyo vyati analipa mteja wa mwisho na si mwekezaji
 
Masikini watanzania!!! yaani inafikia hatua ya kuona ni afadhali muwekezaji aendelee tu kuingiza fedha kwa biashara anazofanya nchini bila kulipa kodi za serikali!!!

Saa nyingine hasa ni kiwango cha hiyo VAT. Mfanyibiashara anapoamua kuondoka ujue yamemfika shingoni. Si jambo rahisi kufungasha biashara kama bado unapata faida.
Lazima ufikirie kwa akili na siyo kwa mihemko tu.
 
Waondoke waende huko pasipolipwa VAT. Hata meli ambazo hazileti VAT zisije, ziende huko. Pia watalii wasiotaka kulipa VAT wasije.
 
Wadau, habari za majukumu! Baada serikali mpya kuingia waliingiza VAT kila sehemu hata kwa waliosamehewa kodi hiyo, nasemea upande wa watengenezaji chakula cha kuku! Kampuni ya thailand CPF wanafunga operation na kuondoka mwisho wa mwezi huu!! Nawasilisha
Huyo atakuwa alikuwa halipi kodi labda wala si VAT..
 
walipenda dezo waende tu. kwao kwani hawalipi VAT?
Kuna kitu hukielewi! Usitoke povu ka huelewi mambo! Bora ungesubiri wajuzi wakuelezee uelewe kwanza!!
 
New Zimbabwe is around the corner!

Kweli. Mfano mwingine mzuri zaidi ni wa Venezuela - nchi tajiri yenye visima vingi vya mafuta. Kiongozi wao (Maduro) ana tabia hizi hizi tunazozishuhudia ... ukurupukaji, ubabe dhidi ya wapinzani wake, ukanda, uvunjaji wa katiba, u-Mungu mtu, kulaumu wawekezaji & kuwaita wanyonyaji, etc. Matokeo yake wawekezaji wameondoka na mitaji yao, hakuna ajira, hakuna mzunguko wa fedha, serikali haina hela ya mishahara na katoa decree wafanyakazi wa serikali waende kazini siku 2 tu kwa wiki, biashara zimesimama na hamna bidhaa madukani - badala yake akiamka vizuri anaamua mipaka ya nchi ifunguliwe ili watu wakafanye shopping Colombia. Na sisi inaonekana tunaelekea huko huko
 
Back
Top Bottom