nimegundua humu watoto wengi sana.
na wengi wenu hamjawahi kuajiriwa kwenye corporates na kuona mfumo wa formal sector ulivyo.
sikilizeni kwa makini vijana. msijidanganye.
mshahara haupangwi kutokana na elimu uliyonayo. bali unapangwa kutokana na position scale.
hata kama wewe ni profesa. kama kwenye kampuni ukipangiwa kufanya kama secretary wa bosi. basi utalipwa mshahara wa level ya secretary wanavyolipwa.
hata kama wewe ni darasa la saba. kwenye kampuni ukiajiriwa kama ceo.. hapo utalipwa mshahara kwa scale ya ceo ilivyopangwa..
ukiwa bank teller hata uwe na master, cpa sijui phd.. utalipwa kwa scale ya bank teller.
inshort mshahara unapangwa kutokana na cheo ulichonacho. au kazi unayoifanya salary scale yake ni shilingi ngapi.