Bob Lee Swagger
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 1,362
- 519
Hapana, mambo ya bongo hayajanishinda kwa sababu mimi siyo mwanasiasa. Kuhusu kushauri Tanzania, binafsi nimeshatoa ushauri mwingi sana kwa kutumia njia mbalimbali; kutoa ushauri ni jambo moja, na kuutekeleza ni kitu kingine. Nikiwa kwenye siasa sitafanya ujinga kama unaofanywa na wanasiasa wa Tanzania leo au kama ujinga uliofanywa na huyu bwana mdogo. Kumbuka kuwa kinachotofautisha vichaa na watu wengine ni zile bongo zao; ubongo wangu uko kwenye spectrum tofauti sana na wanasiasa wa Tanzania pamoja na ule wa huyu bwana mdogo.
Kikulacho ki nguoni mwako, asingemuua huyo mjombake, basi mjombake angemuua yeye kwa kushirrikiana na Marekani.
Dawa ya wasaliti ni kifo tu, haswa yanapokuja maslah ya taifa.
Ukikamata muuza unga nyonga, haramia kama yule mbeba matofali ua tu, walioibiaa BOT, ua tu, wahujumu ucvhumi wa kila namna, ua tu....
China isingekuwa inanyonga leo isingefika hapo ilipo.
Ili nchi iendelee inahitaji watu wenye discipline ya hali ya juu na wachapakazi.
Unadhani kuwa huna la kuifanyia nchi yako hadi uwe mwanasiasa?! kama unadhani wale wote wanaoharibu na kuuza rasilimali zetu ni wanasiasa, fikiria vizuri!
Hichi kitoto kimeanza kuua wazazi na walezi, Aluuuu
Sijajua unachonieleza hapo sasa una maana gani. Topiki iliyopo hapa mbele yetu inahusu wanasiasa, na nilikuwa natoa ushauri wa kisasa; ukanisema kuwa nimeshindwa ya Tanzania nitawapaje wengine ushauri, ndipo nikakuambia kuwa mimi siyo mwanasiasa ila ushauri nilishautoa mwingi kwa wanasiasa wetu. Sasa hii post yako ya mwisho inaonyesha kuwa wewe ni mkurupukaji asiye kuwa makini na anachoandika. Sijui ndugu yangu unataka nifikirie kitu gani vizuri kwani inaelekea unadhani kuwa sijui kufikiri vizuri. Mimi ni mwalimu wa karibu miaka 30 nikiwa nafundisha vyuo mbalimbali, ninajua kufikiri na ninafanya kazi yangu ya ualimu vizuri sana; ushauri wa Kim ndio huo niliotoa tena kwa kufikiri vizuri sana. Ukiua mtu mmoja influential huwa una-create kundi kubwa la maadui ambao walikuwa followers wake. Huwezi kuongoza nchi vizuri ukiwa na maadui wengi, simple and clear! Usimamizi wa serikali ni kazi ya wanasiasa; wanaposhindwa kufanya kazi yao ya kuisimamia serikali ndipo wanaporuhusu watu binafsi kuiba raslimali za umma.
Inasemekana pia mkasa mzima ni issue za mapenzi, kuwa huyu uncle wake(Jang Song Thaek) alikuwa ni mpenda vimwana sana(womaniser) na alikuwa ameanza kumtongoza mke wa mwenye kaya(simply his son) mrembo Ri Soul Ju na dogo akapata taarifa. Huyu mke wake inasemekana hajaonekana hadharani karibia miezi miwili sasa.
North Korea's Jang 'Tried to Woo Kim
Ingawa ni kweli huyu uncle wake Kim amekuwa kwa muda mrefu akitofautiana kimawazo na chama na serikali yake lakini wachambuzi wengi wanapinga kuwa msimamo wake huo ungeweza kumpelekea kupanga mapinduzi maana kwa mfumo wa North Korea hiyo ni almost impossible.
Huyu dogo(Kim Jing Un) anaonekana ni mtata sana kuliko hata baba na babu yake. Toka aingie madarakani tayari amemfukuza aliyekuwa mkuu wa majeshi Gen. Ri Young Ho ambaye mpaka sasa naye hajulikani alipo. Pia miezi kadhaa tu nyuma inasemekana alimnyonga mpenzi wake wa zamani bibie Hyon Song Wol kwa tuhuma za kurekodi mkanda wa ngono. Kwa maoni yangu sidhani kama dogo Kim anaweza kudumu madarakani muda mrefu kama watangulizi wake.