Tetesi: Kilio cha simu bandia(fake) huenda kikazidi hata kilio cha sukari

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,117
1,369
Zipo taarifa za kutoka TCRA kuwa ifikapo June simu nyingi zitazimwa ,ambazo kwa viwango vyake sio halisi.

Kwa utafiti wangu huku mtaani kutakuwepo kilio ambacho na malalamiko huenda kushinda cha uhaba wa sukari.Hii ni kutoka na ukweli kuwa karibia kila familia inamiliki simu moja ,na ukizifuatilia nyingi si halisi.

Matumizi ya simu siku hizi sio jambo la hiyari limekuwa ni jambo la lazima kutokana na mtawanyiko wa watu na mahitaji, Nani hataguswa hats mie ntaguswa maana simu anayotumia mama yangu Kule kijijini huenda fake. Ina maana nnunue simu nyingine.

Najiuliza hivi hizi simu zimepitia wapi?

Je ,hii mamlaka in mpya? Nani atafidia gharama zetu? Je, hizi simu fake zimeiathiri nchi kwa kiwango gani?
Nawasilisha!
 
Ndio kuisoma namba kwenyewe huko!!!
Mijitu ikipewa madaraka badala ya ku-exercise usomi yenyewe ina exercise UJINGA.
 
Kama kweli maamuzi mabaya yaliyotolewa na awamu iliyotangulia lakini awamu hii inayojipambanua kama ya uadilifu inashindwa kuyabadilisha ni kitu cha kusikitisha sana.
Wakati maumivu ya Watanzania kuzimiwa simu zao yakianza sote tusisahau kuwa TBS, TRA, Fair competition nk wote walikuwepo na kodi zilitozwa kikamilifu wakati simu hizi zikiingizwa nchini! Tunasubiri Tanzania ya viwanda.
 
Mkuu inauma sana kuona watu wasio na kosa lolote wakizimiwa simu zao walizonunua kihalali na serikali ikachukua kodi yake.Nchi hii yaelekea wapi jamani?
 
Je kama simu zinazimwa mwezi WA 6 arafu umeingiza mzigo toka inje na baadhi hazikupita TCRA inakuwaje lakini hz simu ni original
 
mkuu hii ni kama analog kwenda digital walivyotoa antena wakaleta ving'amuzi, sio serikali ndio imeamua ni huko duniani ndio wametoa tamko, nchi nyingi duniani wameshafanya, kenya, uganda etc sisi ni wa mwisho mwisho
 
Kama kweli maamuzi mabaya yaliyotolewa na awamu iliyotangulia lakini awamu hii inayojipambanua kama ya uadilifu inashindwa kuyabadilisha ni kitu cha kusikitisha sana.
Wakati maumivu ya Watanzania kuzimiwa simu zao yakianza sote tusisahau kuwa TBS, TRA, Fair competition nk wote walikuwepo na kodi zilitozwa kikamilifu wakati simu hizi zikiingizwa nchini! Tunasubiri Tanzania ya viwanda.
Hapo ndo wengi tunahoji?hivi hatuwezi Songa mbele kwa kuzuia bidhaa feki ktk soko kuanzia sasa bila kuathiri nyuma.
 
Kama kweli maamuzi mabaya yaliyotolewa na awamu iliyotangulia lakini awamu hii inayojipambanua kama ya uadilifu inashindwa kuyabadilisha ni kitu cha kusikitisha sana.
Wakati maumivu ya Watanzania kuzimiwa simu zao yakianza sote tusisahau kuwa TBS, TRA, Fair competition nk wote walikuwepo na kodi zilitozwa kikamilifu wakati simu hizi zikiingizwa nchini! Tunasubiri Tanzania ya viwanda.
Hapo ndo wengi tunahoji?hivi hatuwezi Songa mbele kwa kuzuia bidhaa feki ktk soko kuanzia sasa bila kuathiri nyuma.
 
Je kama simu zinazimwa mwezi WA 6 arafu umeingiza mzigo toka inje na baadhi hazikupita TCRA inakuwaje lakini hz simu ni original
IMEI ya simu ndio inayotambulisha simu ni original au fake hata kama haikupitia TCRA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom