Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

Tujipiganie wenyewe, no body cares about us. Umeme haushikiki na gesi nayo ndo usiseme. MABADILIKO NI LAZIMA YAFANYIKE 2015 SIO MBALI.
 
eura walikosea wangepiga 100% unajua wakuu hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania.
kuna mama alikuwa analalamika kwenye hiace nauli zilivyopanda 400 nikasema kwa nguvu kwanini wasingefanya 1000 ili na makonda wasipate shida ya chenji,mama alinicheki kwa hasiraaa.
nikamwambia ukiambiwa andamana utakubali?

Wewe mburura kweli sasa kuandamana ndio umeona suluhisho unakumbuka siku ambayo uliongoza darasa angalau kwa somo ata la michezo?
 
Asante kwa Matusi lakini ukweli ni huo kuwa Maisha ni Magumu na Tunachopata leo kina liwa leoleo.

So nikipata La Kumi leo basi ndio nannunua umeme, Nikikosa mwendo wa Giza na Fanilia ipo kama kawa na Inadunda.

Sijuhi wewe ndugu yetu wakwenye Apartment unaijua bei ya Umeme?

Lete familia yako kwenye apartment tukulelee kama maisha ya mjini yamekushinda.
 
we dada unaishi Tz au? mimi pia nimenunua umeme wa sh 10,000 nimepata units 8.7, hakuna deni la zamani hapo. hiyo fixed amount huwa inakatwa (kama servise charge) kila mwanzo wa mwezi unaponunua umeme kwa mara ya kwanza. lililopo, fixed amount imepanda na price per unit imepanda pia.
fixed amount (service charge) + kodi inafika shs 6700 kwa sasa. ukilipa hiyo ndio unaanza kununua units za umeme

Sasa ulitaka usilipe service charge? umeshafikiria gharama za usafiri na muda ulizopunguziwa kwenda kulipia bill yako TANESCO kila mwezi?
 
Huko kwa wapiga kura wenyewe wanatumia koroboi na moto
Huku mijini wapiga kura hamna..siku ya kura wanalewa tu...wamepoteza vitambulisho...hawakujiandikisha...wapo busy na biashara zao...wanashinda jf kusubiri matokeo
Kijijini voters kadi ni mali...unadhaminiwa mikopo..unadhamini mtu polisi na mahakamani..unafungulia akaunti hivyo zinatunzwa na siku ya kura zinauzwa pia!!!
 
Bei ya umeme ni jambo linalowahuzunisha na kuwatia hasira wananchi. Na hasira zao watazionesha kwenye sanduku la kura. Uchaguzi wa 2014 utakua mgumu sana kwa CCM. Kinana usishughulikie mawaziri mizigo tu, shughulikieni na mashirika mizigo.

na oporesheni majangili iliyoua ndugu zetu na kuwaingizia chupa sirini! Laana
 
Mi leo hii nimenunua Unit 22.4 kwa Tsh. 15,000/=

Na mwezi wa 12 nilinunua Unit 38 na mwezi wa 11 nilinunua unit 31

Bila shaka ni wakati mwingine wa kufikiri sana na kuhitaji mabadiliko ya kweli.
Ccm haifa kuwepo madarakani kamwe!
 
[mimi pia nimenunua umeme wa sh 10,000 nimepata units 8.7, hakuna deni la zamani hapo. hiyo fixed amount huwa inakatwa (kama servise charge) kila mwanzo wa mwezi unaponunua umeme kwa mara ya kwanza. lililopo, fixed amount imepanda na price per unit imepanda pia.
fixed amount (service charge) + kodi inafika shs 6700 kwa sasa. ukilipa hiyo ndio unaanza kununua units za umeme]

Mdada nashukuru kwa maelezo yako ya hii Service charge (fixed amount). Jambo la kujiuliza ni kwa nini uwalipe EWURA na REA Mara mbili ? Kwani uhusika wao EWURA na REA katika service charge unatokana na kitu gani?
Inabidi sie walaji tupinge hii kitu kwa ya kuwalipa EWURA na REA Mara mbili mbili. Kwani ndio wanaoongeza gharama zisizokuwa na ulazima wowote.
 
eura walikosea wangepiga 100% unajua wakuu hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania.
kuna mama alikuwa analalamika kwenye hiace nauli zilivyopanda 400 nikasema kwa nguvu kwanini wasingefanya 1000 ili na makonda wasipate shida ya chenji,mama alinicheki kwa hasiraaa.
nikamwambia ukiambiwa andamana utakubali?
Mimi ningependa upande zaidi..simu ile kodi ya buku iwe per day..
Kubipu...jero
gesi iwe laki kwa 15 kg na petrol lita iwe buku tano
Daladala buku na route ndefu iwe buku 2
Maji ya uhai... buku
Abood mpaka moro.. mbau
Kumuona dr....mwekundu!
EFD milioni
Hapo ndo watz watauliza Katiba,Tume ya uchaguzi na vyama vya upinzani ni nini.sasa hivi kwao ni msamiati wa kichina
 
Sasa ulitaka usilipe service charge? umeshafikiria gharama za usafiri na muda ulizopunguziwa kwenda kulipia bill yako TANESCO kila mwezi?

dada unapenda sana ligi a.k.a ubishani,
nilikuwa najibu comment yako uliyosema kwamba fixed amount ni madeni ya nyuma, nikakwambia hiyo ni service charge ambayo customer analipa kila mwanzo wa mwezi anaponunua umeme for the first time, na kwa sasa inafika Tshs 6700

pia, sijasema kwamba mtu asilipe service charge, nimesema both, service charge na price per unit zimeongezeka.

nimeongea facts bila kuleta ushindani kama unavyotaka wewe. it's up to you, kuzikubali au kuzikataa
 
18%+3%+1%+Service charge
VAT+REA+EWURA+Service Charges
Hapo bado hujapata units
 
dada unapenda sana ligi a.k.a ubishani,
nilikuwa najibu comment yako uliyosema kwamba fixed amount ni madeni ya nyuma, nikakwambia hiyo ni service charge ambayo customer analipa kila mwanzo wa mwezi anaponunua umeme for the first time, na kwa sasa inafika Tshs 6700

pia, sijasema kwamba mtu asilipe service charge, nimesema both, service charge na price per unit zimeongezeka.

nimeongea facts bila kuleta ushindani kama unavyotaka wewe. it's up to you, kuzikubali au kuzikataa

Facts ni facts na ahsante sana kwa hilo nami umenielimisha na wala sina tatizo huko.

Sasa unalalamika nini? umeme ndio umeshapenda. Kama unaona gharama zinazidi punguza matumizi ya umeme au vumbuwa umeme wako wa rahisi au kata matumizi mengine uende sambamba na mabadiliko hayo. Njia za kufanya nyingi badala ya kukaa kulalamika bila kutafuta ufumbuzi wa tatizo kama ni tatizo.

Kulalamika lalamika inasaidia nini? halafu umeme ukikatika-katika mnalalamika, zinapotakiwa pesa za ziada muwe na umeme wa uhakika mnalalamika.

Hizo shule mlizokwenda badala ya kuwafutia ujinga zimewaongezea ujinga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom