ilboru1995
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,329
- 268
Yan mm imeniuma Kwel Kwel lakn con Hata pa kuanzia kugoma....lol
Anza kujiunganishia umeme kinyemela! Mwisho wa siku mahakama na magereza watajaa wateja wa umeme ! Dunia itaingilia kati!...
Yan mm imeniuma Kwel Kwel lakn con Hata pa kuanzia kugoma....lol
Ama wajitahidi wafute hizo kodi kwenye umeme maana ndo zinaua bendi.
Anza kujiunganishia umeme kinyemela! Mwisho wa siku mahakama na magereza watajaa wateja wa umeme ! Dunia itaingilia kati!...
Yaani unatembea mule mule nilipo na mambo hayakai sawa! huu mlinganyo jawabu liko upande wa pili-ni kuilazimisha serikali ibatilishe hili ongezeko! kwa maana hata ukisema ubakishe vitu vya lazima tena kwa kujibana bado hesabu haivutii machoni!Kwa hili la umeme nimeamini Watz tu watu wa ajabu sana,na hao viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza ndio mizigo zaidi,inatia hasira........wachangiaji munashauri tupunguze matumizi wengine tulishapunguza muda mrefu,mfano mimi friji nilikuwa nawasha mchana tu ikifika usiku nalizima,sasa mkiniambie nipunguze maana yake nisiliwashe kabisa,pasi nanyoosha nguo za wiki nzima,tv siwashi maana siangaliagi,matumizi yangu makubwa ni computer kwa maana ya kufanyia kazi kucheki......jamani wengine tushapunguza vya kutosha lkn rhumba ni lile lile......
Swahibu wangu kwa hali ilivyo si wakati wa kumuomba kaka (mwnasiasa) akusaidie ,hapa ni kuchukua hatua stahiki kama mwananchi kuhusiana na dhahama hii,makali yake hayatupi nafasi ya kusubiri huruma za wajomba!Services charges ndio Janga sana,tuakikishe inafutwa viongozi wa upinzani tunaomba mtu saidie hili,mbona kwenye vocha za simu hatukatwi service charges?
Cc: Dr.W.Slaa ,Julius Mtatiro , John Mnyika, Rev. Mtikila, James Mbatia
Swahibu wangu kwa hali ilivyo si wakati wa kumuomba kaka (mwnasiasa) akusaidie ,hapa ni kuchukua hatua stahiki kama mwananchi kuhusiana na dhahama hii,makali yake hayatupi nafasi ya kusubiri huruma za wajomba!
Chadema wakwap??? Au Ndo nao wana maslah mle tanesco??
Tunabanwa kushoto, kulia. hakuna pa kukumbilia. Umeme na sasa kuna kilio cha EFD. Mama mmoja aliyefunga duka lake amenifurahisha kwa kusema hizo EFD zinajua mauzo tu hazijuia unanunua kwa gharama gani.Stabilaiza
Ni kweli mada yako ina mashiko, ila napata shaka EWURA ipo kwa masilahi ya nani?serikali, watumiaji huduma za umeme, maji, nishati na mafuta?
Kimsingi inatia shaka kama ipo kwa masilahi ya wananchi au kama ni kupata posho na mishahara minono kwa kazi ndogo sana za ubabaishaji kama kusingizia wadau wamekutana na EWURA , hivyo kuridhia kupanda bei.Tatizo la kupanda bei ya umeme ni makosa ya wizara kwa kuridhia capacity charges, kuridhia kuendelea kuendesha mtambo wa IPTL, kuridhia kuwa na mikataba ya mitambo ya kutumia mafuta yapata miaka minne sasa, huku bei zao za umeme ni kubwa mno kiasi tanesco haikuwa na uwezo wa kununua umeme huo.
Nakumbuka akina JOHN MNYIKA walipinga kiasi kikubwa bungeni hiyo mitambo kuwa italeta mzigo wa watumiaji ikasemekana ni kwa muda tu.na serikali wakati huo kukopa pesa kwenye vyombo vya fedha kwa riba kubwa kulipia mafuta. Hiyo yote ndo imeleta hii kadhia.Kimsingi hao walioridhia walipashwa kufikishwa mahakamani kulinginza taifa kwenye utata huu na gharama kubwa za umeme ambao umeongeza bei ya umeme. Tatizo nchi yetu watanzania si watu wakuhoji ubabaishaji.
Simbachawene alipohojiwa akasema mtu atakaye shindwa kulipa bei ya kupanda umeme akawashe kibatari , ikuwa kuwa kila namna umeme lazima upande hata kama wadau mtahusishwa kama daganya toto kuridhia, lakini iwe funika kombe serikali ipandishe bei.
Kimsingi kupanda bei ya umeme, ni kupandisha ugumu wa maisha , hivyo tukaze kamba tu, maana mfumko wa bei inakuja sasa hivi.
CHADEMA yale maandamano yetu mbona kimya????? Au kwa sababu na nyinyi hamuoni shida kama MACCM?? tambueni sisi wananchi tunateseka
Nimeshangazwa sana na ukimwa wa wanasiasa kuhusu kupanda kwa bei ya umeme.
Ifike mahali wanasiasa wawajibike kwa wananchi dhidi ya ugumu wa maisha kila kukicha. Kupanda kwa bei ya umeme kutasababisha ugumu wa maisha na mfumko wa bei hivyo kuimarisha umaskini kwa wanachi. Au ni maandalizi ya uchaguzi mwaka 2015 ili kuwahonga kirahisi watu chumvi, kanga na sukari kwa sababu ya ugumu wa maisha?