Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
Nimeshangazwa sana na ukimwa wa wanasiasa kuhusu kupanda kwa bei ya umeme.

Ifike mahali wanasiasa wawajibike kwa wananchi dhidi ya ugumu wa maisha kila kukicha. Kupanda kwa bei ya umeme kutasababisha ugumu wa maisha na mfumko wa bei hivyo kuimarisha umaskini kwa wanachi. Au ni maandalizi ya uchaguzi mwaka 2015 ili kuwahonga kirahisi watu chumvi, kanga na sukari kwa sababu ya ugumu wa maisha?
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,236
2,000
Tangu lini aliyeshiba akamjua mwenye njaa!? Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe, bila Watanzania kuja juu na kuukataa huu mfumo dhalimu wa MACCM hali ya maisha kwa Watanzania walio wengi itazidi kudidimia. Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele.
 
Sasa tuanzie wapi, maana suala hili linagusa wengi. Swali ni nani ataratibu kupinga kupanda kwa bei ya umeme?. Sisi tunawalipa mishahara wanasiasa kupitia kodi tunazotoa. Kuna ruzuku kwa vyama vya siasa, wasifikiri wanalipwa bure. Sasa wawajibike ili kwa pamoja tupinge kupanda kwa bei ya umeme
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,863
1,250
Nimeshangazwa sana na ukimwa wa wanasiasa kuhusu kupanda kwa bei ya umeme. Ifike mahali wanasiasa wawajibike kwa wananchi dhidi ya ugumu wa maisha kila kukicha. Kupanda kwa eni ya umeme kutasababisha ugumu wa maisha na mfumko wa bei hivyo kuimarisha umaskini kwa wanachi. Au ni maandalizi ya uchaguzi mwaka 2015 ili kuwahonga kirahisi watu chumvi, kanga na sukari kwa sababu ya ugumu wa maisha?

Wanasiasa pekee wanaoweza kusema juu ya bill ya umeme ni Chadema sasa nyie kila mnawatukana mara Babu , mara hawana shule , mara Saccos sasa you face it .Maana wao wana pesa they can afford wako kimya tuumie wote .Wanaungana na wabunge wa CCM kukaa kimya .Si ni Saccos ? Tafuteni isiyo saccos iwasemee .
 
Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
Wanasiasa pekee wanaoweza kusema juu ya bill ya umeme ni Chadema sasa nyie kila mnawatukana mara Babu , mara hawana shule , mara Saccos sasa you face it .Maana wao wana pesa they can afford wako kimya tuumie wote .Wanaungana na wabunge wa CCM kukaa kimya .Si ni Saccos ? Tafuteni isiyo saccos iwasemee .
Wanaotukana ni wale wanaokula kuku kwa mrija, siyo wananchi wa kawaida.
 
Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,144
2,000
hata wanaharakati wanalo la kutusemea katika hili.................huenda tunahitaji Big Bhang
 
  • Thanks
Reactions: BAK

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,384
2,000
Watanzania nasi tumekuwa mno wapole, huvi kwa umoja wetu tukikubaliana wstumiaji wa umeme tukubali kutotumia hiyo nishati kwa wiki moja tu watapata wapi income hao tanesco??? Viwanda wazime umeme wstumie generators na sisi hohehahe tutumie vinatari tuone
 
Ngoso

JF-Expert Member
May 26, 2012
528
250
magamba in action wanafanya usanii,wanapandishe bei ya umeme wenyewe kisha watakuja MAJUKWAANI na mashairi na vibwagizo serikali yenu sikivu inawajali ,INAWATAKIA MEMA NA MSHIKAMANO na kupunguza kama walivyopitisha kodi ya line ya simu kwa kishindo mara wameondoa ili waonekane wana huruma kwa wananchi tusahau ujangiri,wageni waliokamatwa na maliasili zetu ,mikataba mibovu ya gesi,mafuta,pesa za Uswiz na uranium subiri utaona!!!!!
 
Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,058
2,000
hili swala halihitaji wanasiasa ni letu sote mimi na wewe. lakini naona kama hizi gharama zimepita na kukubarika na jamii.
Hili ndio tatizo letu Watanzania kuona yanyotuhusu kuwa si yetu na kuwakabidhi na kuwategemea wana siasa kama akina Zitto watuongoze na kupinga upuuzi unaofanywa na watawala wetu wakati wana Siasa wenyewe wanajishibishaa matumbo yao
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,083
1,500
wametegea watu wako busy na sikukuu, magamba wakapiga hapo hapo, mijamaa mijizi sana
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,831
2,000
Tatizo letu ni hilo la kutegemea wanasiasa watutatulie kero zetu,
hao hawana shida sisi ndio wenye shida kwa nini tusi react kwa nguvu zetu zote?
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,071
0
Tangu lini aliyeshiba akamjua mwenye njaa!? Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe, bila Watanzania kuja juu na kuukataa huu mfumo dhalimu wa MACCM hali ya maisha kwa Watanzania walio wengi itazidi kudidimia. Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele.

Ask not what your Country can do for you ask what you can do for your Country. - John F. Kennedy
 
Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,834
2,000
Alafu si nasikia kuna bil 400 imepatikana kwenye hisa...!
Walipe madeni yao sie tupunguziwe bei.

Wanasiasa sio wenzetu, wapo kwa msimu na msimu wao 2014 zaidi 2015
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,495
2,000
Ask not what your Country can do for you ask what you can do for your Country. - John F. Kennedy

Hiyo ni kwa America sio Bongo kaka..Kwa bongo it's vice versa kwa ushahidi zaidi muone uncle Lukuvi
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom