Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,039
Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Abel ameongoza kamati ya ulinzi na usalama wilayani kusaka miili ya marehemu waliouawa katika mapigano ya Wakulima na Wafugaji wilayani Kilindi.

Tayari miili mitano imeshapatikana na polisi wameweka ulinzi mkali.

d awa s.jpg


Chanzo: ITV habari

=====

Watu watano akiwemo mtoto wameuawa baada ya kufuatia mapigano baina ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Elerai kilichopo wilayani Kilindi mkoani Tanga ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo amefika katika eneo la tukio na kuzitaka pande zote mbili kusitisha mapigano hayo wakati serikali ikitafuta suluhu ya jambo hilo.

----
Watu watano wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na kukatwa mapanga huku wengine watatu wakijeruhiwa kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji yaliotokea Wilayani Kilindi mkoani Tanga katika kijiji cha Kibirashi na Elerai.

Wakielezea chanzo cha mapigano hayo mashuhuda wa tukio hilo wamesema ni mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wakulima na wafugaji wa vijiji hivyo ambao vuguvugu zake zilianza muda mrefu bila kupata ufumbuzi wa kudumu, ambapo leo Januari 30 ndio ikatoa tukio la mapigano katiya pande hizo mbili.

Mkulima Richard Masaki amesema waliona vijana jamii ya kimasai wakiingia katika eneo lao na kuanza kuwashambulia, kwa kuwapiga na baadae yakaanza mapigano ya mapanga na risasi hadi kutokea vifo hivyo.

Aidha mfugaji David Kimaki amesema ampoteza mjukuu wake Betina ambae ameuwawa kwa kukatwa na Panga katika shambulio hilo.

"Tulivyopita mbele kidogo tukashambuliwa kwa risasi, nikajua ni wale wale watu nikachukua hatua nikampigia OCD kumpa taarifa kwamba huku kuna mauaji mengine, tukaongozana na kuona miili mingine zaidi", amesema Kimaki.
Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama akiwa eneo la tukio licha ya kuongoza zoezi la kukusanya miili ya marehemu amesema watu watano wamefariki dunia na watutu kujeruhiwa, kutokana na tukio hilo.

Aidha amezitaka pande zote mbili kusitisha mapigano na kusalimisha silaha zao ili utatuzi wa mgogoro huo ufanyike kwa njia ya amani kwani njia wanayotumiwa hawawezi kupata utatuzi.

"Wito ninaotoa kwa pande zote mbili zinazozingamana hapa ni kuacha mapigano haya haraka, kwani mapigano haya hayawezi kusaidia katika kutafuta ufumbuzi na waweke silaha zao chini", amesema DC Busalama.
 
Now days Mauaji ni left and right...anyway tutavuna tulichokipanda...Tumeacha kumgeuzia Uso wetu Mungu tupo bize na mizimu ya machifu....
 
Intelligensia ya polisi Tanzania inakomea kuwadhibiti CHADEMA wasiandamane, ila hawana Intelligensia ya kuzuia mauaji na uhalifu mkubwa.

Sirro amekosa ubunifu
 
Now days Mauaji ni left and right...anyway tutavuna tulichokipanda...Tumeacha kumgeuzia Uso wetu Mungu tupo bize na mizimu ya machifu....
Roho za kipuuzi ni upuuzi tu huko watu na Imani zao Mfano Northern Ireland ilipelekea watu kuuana tena katika hili vuguvugu la upuuzi na watu kujali vitu materialistic ukiweka na Imani watu wanaweza kuchinjana mchana kweupe.

Kama Mizimu nayo ni Imani kwanini wewe uone kwamba mizimu ndio inaleta hii shida.

Anyway sikubaliani na serikali kufungamana na Imani yoyote ile above any, na kama ni uchifu, iwe symbolically na sio kushinikizana au kupena ruzuku ya pesa zetu za kodi.

To each his/her own...
 
Back
Top Bottom