Asante Kanyagio kwa taarifa.
Hata nami nilipata taarifa za huko hivi karibuni na nimekuwa nikifuatilia uwezekano wa kulima kwa mwaka huu, lakini mpaka sasa sijapata shamba hata la kukodi kwani ninayemtumia ananipa hadithi kila siku. Nategemea kwenda mwenyewe weekend hii; vipi kuna mtu unayemfahamu ambaye anaweza kunisaidia upatikananji wa shamba even la kukodi. Je kwa jinsi ulivyoona itkuwa ni wakati muafaka kwangu kulima mwaka huu au nitakuwa nimechelewa kutokana na msimu wa mvua.
Je ulidadisi gharama ya kukodi tractor ni kiasi gani kwa heka,na mazingira ya mtu kuja na Tractor lake yakoje?msimu kwa kilimo unaanza mwezi gani.kuna uwezekano nikaja kusurvey kipindi hicho kwa kuja na ka-massey ili kulimisha and the same time kuona uwezekano wa kununua japo ekari70 hivi ,na kwa bei uliyotaja ya elfu 10 itakuwa around 700,000.
newmzalendo, [URL="https://www.jamiiforums.com/members/mgombezi.html"]Mgombezi na wengineo[/URL]https://www.jamiiforums.com/members/newmzalendo.html: kulima kwa trekta inaenda Tsh. 30-40,000 kwa ekari kutegemeana na sehemu. ila kumbuka kabla ya kulima na trekta ni lazima ufyeke na kungoa visiki. ekari moja wanafyekea Tsh 10,000/= na unaongezea fedha kidogo ya kung'oa visiki.. msimu wa kulima ndo huu kwa sababu mvua ndo zimeanza.. hutakiwi kuchelewa kwa sababu mvua kiteto ni msimu mmoja (mara nyingi).
Mhh kilimo cha kuvizra mvua hakina tija!bora ununue mazao wakati wa mavuno uyahifadhi ikifika jan au feb unauza bei maradufu!
Asante Kanyagio;
Kama nilivyosema ninaelekea huko weekend hii na tutapashana zaidi.
Yeah ni wazo zuri lakini ni vizuri kujaribu uwekeza kwenye kilimo pia - Mwaka jana nililima hekari 50 matokeo hayakuwa mazuri.
Kipindi cha mavuno May 2010 Debe la mahindi lilikuwa linauzwa 3,000 had 3500. Sikuwa na pesa za kununua na kuweka stock na kama ningefanya hivyo basi ningepata marafufu kwani kwa sasa debe linauzwa 7000 hadi 7500 Tshs.
Kwa sasa nitayauza mahindi kidogo ambayo nilipata msimu uliopita ili nijiweke sawa kwa msimu huu kwa kupunguza makosa yaliyojitokeza msimu uliopita kama kuchelewa kupanda na kutumia mbegu zisizo bora zaidi.
Kilimo cha Umwagiliaji kinahitaji mtaji mkubwa sana, hatuna njisi kwa sasa ni kutumia tu hizi hizi mvua na neema ya mwenyezi mungu. Kununua mazao na kuweka stock kipindi cha mavuno ni jambo zuri pia ingawa linahitaji mtaji mkubwa ili kupata mafanikio kwa mfano ukinunua mazao ya thamani ya Tshs 50m basi baada ya miezi 8 utapata 100m bila ubishi.
Mkuu,
ukirudi toka shamba njoo utumwagie data zote, mimi naomba uangalie vitu vifuatavyo huko porini uendako.
Kaangalie aina ya wadudu wote walioko huko porini
Kaangalie aina ya ndege wanaoishi huko
kaangalie aina ya wanyama wa porini na wafugwao
Kaangalie na aina ya matunda gani yako huko
Na ukiweza tuletee picha za misitu au vipori vya huko
Unaweza kupata haya kwa kuuliza pia.
Asante na safari njema.
Mkuu Malila pamoja na wadau wengine.
Ni kweli nilitoa ahadi ya kwenda Kiteto weekend iliyopita lakini kutokana na majukumu mengine yaliyojitokeza nilishindwa kutekeleza ahadi hii; hata hivyo kutokana na taarifa ambazo nimekuwa nikizipata kutoka huko ni kwamba msimu wa kulima umekaribia au umekwisha na sasa mahindi yapo kwenye hatua ya kupalilia, nami lengo langu ilikuwa ni kupata uwezekano wa kulima mwaka huu. Hivyo basi najiandaa kufanya ziara ya huko kwa wakati mwingine na ninajiandaa kwa mwakani. Samahani sana kwa wadau waliokuwa wanategemea kupata taarifa za huko, bali kama kuna yeyote mwenye taarifa zaidi tuendelee kujuzana. Vilevile kikao chetu tutakachokutana punde naamini tutapeana taarifa zaidi.