Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Mwaka Jana nimelima heka moja ya vitunguu na jumla gharama nilitumia 1,700,000/= nikafanikiwa kupata gunia 72 ambayo kila gunia niliuza kwa 90,000/= sawa na tsh 6,480,000/= ukitoa gharama zangu unapata baki ya tsh 4,780,000/= Nilipotoa gharama zangu zote nyingine kama usafiri na chakula nilipokuwa shamba nikabakiwa na 4,300,000/= Nilitumia miezi minne mpaka kuvuna na approximation ni kama kila mwez niliingiza 1 million. Ni kiasi kidogo na ni kikubwa pia.
Tujifunze kuwekeza shambani
Safi sana, tatizo kubwa miongoni mwa watanzania ni kuogopa KUTHUBUTU
 
Mwaka Jana nimelima heka moja ya vitunguu na jumla gharama nilitumia 1,700,000/= nikafanikiwa kupata gunia 72 ambayo kila gunia niliuza kwa 90,000/= sawa na tsh 6,480,000/= ukitoa gharama zangu unapata baki ya tsh 4,780,000/= Nilipotoa gharama zangu zote nyingine kama usafiri na chakula nilipokuwa shamba nikabakiwa na 4,300,000/= Nilitumia miezi minne mpaka kuvuna na approximation ni kama kila mwez niliingiza 1 million. Ni kiasi kidogo na ni kikubwa pia.
Tujifunze kuwekeza shambani
Naomba unipe mwanga kidogo ndg maana nna huo mpango wa kulima vitunguu pia
 
Fanya utafit kwanza ndipo utoe ushaur, japo ushaur wako ni mzur sana
Lakin tuangalie risk katika kilimo tanzania tena kilimo endelevu.
Ni kweli mazao ya chakula soko lake ni lauwakika sana
Ila swali la kujiuliza shortage ya mahid iliyopo maeneo ya mikoa ya kaskazin wakulima wa kusuni ambao wanasuplus ya mahid wataweza faidika na hali hiyo
Je nyanya za dumila, mkulima anaweza faidika na shortage ya nyanya dar.
Kisha waza mtu alie chukua mkopo bank na anatakiwa kulipa na riba, kwa hali kama hiyo ataweza.
Maana utafit unasaidia kupunguza riski, ila kuingia ktk biashara bila utafik na kuangalia flan alipata nin tena kwa kipind kifup ni hatar sana.
Ni vema kujua taarifa za zao utakalo kulilima kama sehemu ya uwekezaji wako kuanzia mazingira ya uzalishaji (inputs) kama chanzo ya maji yako kwa hali ya sasa, usafirishaji, pembe jeo na mambo mengine.
Naunga mkono wazo lako
Unatoa uoga kwa watu bila maana wewe.mtu alieleta haya maneno hapa nakiishi hicho kilimo wewe unaleta maneno.haya ni madhara ya kukaa chuoni bila kunaribu na kuja mtaani kuzunguka na bahasha kutafuta viti vya kuzunguka
 
Fanya utafit kwanza ndipo utoe ushaur, japo ushaur wako ni mzur sana
Lakin tuangalie risk katika kilimo tanzania tena kilimo endelevu.
Ni kweli mazao ya chakula soko lake ni lauwakika sana
Ila swali la kujiuliza shortage ya mahid iliyopo maeneo ya mikoa ya kaskazin wakulima wa kusuni ambao wanasuplus ya mahid wataweza faidika na hali hiyo
Je nyanya za dumila, mkulima anaweza faidika na shortage ya nyanya dar.
Kisha waza mtu alie chukua mkopo bank na anatakiwa kulipa na riba, kwa hali kama hiyo ataweza.
Maana utafit unasaidia kupunguza riski, ila kuingia ktk biashara bila utafik na kuangalia flan alipata nin tena kwa kipind kifup ni hatar sana.
Ni vema kujua taarifa za zao utakalo kulilima kama sehemu ya uwekezaji wako kuanzia mazingira ya uzalishaji (inputs) kama chanzo ya maji yako kwa hali ya sasa, usafirishaji, pembe jeo na mambo mengine.
Naunga mkono wazo lako
 
iko siku utakuja hapahapa kutuambia hakuna biashara mbaya kama ya kilimo note me kila jambo na wakati wake kuna wakati wa kucheka na wakati wa kulia
Hata ajira watu wanafukuzwa kaz au kuumia kazini bro everything has risks
 
Mada inatoa ushaur kwa mwanafunz akimaliza chuo anaweza kujiajir kwenye kilimo.
Atajiajiri vip bila kuwa na initial capital?

Usikurupuke kama ulisoma rudi kafunue upya daftar zako na pitia sehemu ambayo mwalimu wako aliweka alama ya vema kama hakuna
Unaweza kwenda qt.

Kama ulisoma mambo ya kicheketile tuuu hapo sawa maana unajifunza na kuamin kwenye maneno ya watu wakale na sio hali ya sasa
Nenda kwa balozi wako atakupa elimu ju uwezaji na biashara

Umekariri hujaelimika.Maisha halisi elimu yake haiko darasani inapatikana mtaani.Ukisubiria ya darasani utabakia kuwa mwana nadharia.Maisha hayana huruma ya nadharia yanaheshimu vitendo.

Nikurudishe darasani.Jikumbushe siku ya kwanza ulipofundishwa kuandika a,e,i,o,u je ulipewa hadithi ya simulizi tu au uliambiwa tenda kwa kuonyeshwa namna ya kufanya.Ukimaliza elimu ya kiwango chochote ile iwe shule ya Msingi,Sekondari ya kidato cha nne,sita au chuo ukajikuta huna chochote cha kufanya tambua tatizo si hicho wanacholalamikia wengi.Tatizo ni wewe au waliokulea.

Yawezekana ukawa wewe kwa kuwa ulitegemea miujiza au baba na mama,wajomba na ndugu wengine.Yawezekana mchango mkubwa ni walezi wako walikulea kama kuku wa kisasa anayesubiri kuletewa kila kitu alipo.Mletaji akiumwa nawe waumwa njaa.Akifa wafa kwa njaa.

Nisamehe najua ujumbe huu unamaumivu makubwa lakini kwa kuwa nakupenda lazima niuseme,vinginevyo utaishia kulaumu tu.Lawama haizai ,uthubutu unazaa.
 
Kulima nilitumia ng'ombe zangu, ila kama ningelinunua basic gharama yake isingelizidi 80,000/= mbolea niliweka ya kupandia tu, nililima ekari mbili sio moja.
Mkuu achana Na kuwashauri masharobaro wavaa mitepesho ngoja waendelee kula ugali Wa shikamoo!
 
Watanzania wengi wanaishi vijijini na shughuli yao kubwa ya kiuchumi ni kilimo, karibu theluthi moja ya watanzania ni masikini na sehemu kubwa ya theluthi hii wanaishi vijijini ambako shughuli kubwa ya uchumi ni kilimo.
We ni kilaza Wa kiwango cha lami hivi hujui watu Wa mijini wanastarehe kwa kunyonya jasho la mkulima!!
Umaskini Wa vijijini unatokana kwa kiasi kikubwa Na Huduma duni za elimu afya umeme Na miundo mbinu.
 
Kilimo ilikua inaonekana ni kazi za mafukara,sasa hivi kila mtu anakimbilia kulima,magu kabana biashara mjini haziendi km kipindi cha jk.watu sasa wameamua kulima tu.tatizo linakuja wakilima wengi,supply inakua kubwa,demand inashuka,bei inaenda chini.profit inakua ndogo
 
Na wengi hili hawalijui.
 
We ni kilaza Wa kiwango cha lami hivi hujui watu Wa mijini wanastarehe kwa kunyonya jasho la mkulima!!
~Umaskini Wa vijijini unatokana kwa kiasi kikubwa Na Huduma duni za elimu afya umeme Na miundo mbinu~.

Ningekuuliza aina gani ya elimu. Maana kiuhalisia mimi ninayeishi kijijini naweza kukudhibitishia kuwa umaskini wa kijijini ni matokeo ya fikra mbovu za watu, matumizi mabaya ya pesa.
Hata watu wa mjini wana matumizi ya ovyo, tofauti ni vitu tunavyonunua.
Kijijini tunashindana kunywa mataputapu huku mjini wakishindana kuweka sofa za gharama, magari nk wakati uwezo wa kumudu bado
 
We ni kilaza Wa kiwango cha lami hivi hujui watu Wa mijini wanastarehe kwa kunyonya jasho la mkulima!!
Umaskini Wa vijijini unatokana kwa kiasi kikubwa Na Huduma duni za elimu afya umeme Na miundo mbinu.

Wewe ambaye sio kilaza naomba majibu ya maswali haya kwa vielelezo, hivi ni watu wa mjini au serikali ndio yenye jukumu la kuboresha huduma za elimu, afya, umeme, maji, na miundo mbinu ya vijijini pamoja na mijini? Watu wa mjini wanamnyonyaje mkulima? Na kama kuna unyonyaji serikali ipo wapi? Je, sera na sheria za kilimo na biashara zinasemaje juu ya jambo hili?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom