Kuna watu wapo busy kuhangaika kutafuta ajira Serikalini na mashirika binafsi, wengi hufikiri kuwa wanaweza kutoka kwa kuajiriwa, vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo aidha wanafikiri kuwa kilimo hakilipi na wajanja waliopo huko hawawambii wenzao kuwa kilimo kinalipa.
Nitoe ushuhuda kidogo mwezi wa 9 mwaka jana nimelima ekari mbili gharama haikuzidi laki 5 lakini nimeuza mahindi hayo zaidi ya milioni 3. Na bado mengine nikaacha kwa ajili ya chakula, hebu fikiria sasa ni biashara gani ya laki tano ambayo unaweza ifanya kwa mtaji wa laki tano ukapata mil 3 kwa muda wa miezi 4 kwa kifupi haipo.
Mishahara mingi ya waajiriwa wenye shahada ni 450,000/=(kwa wale wenye mikopo) na 560,000/= kama huna mkopo, sasa tufanye hesabu fupi tuchukulie uhalisia kwamba vijana wengi wamesoma kwa mkopo, 450,000 ukilipia nyumba, umeme, maji na matumizi mengineyo unajikuta haifiki tarehe kumi tano unaanza kukopa tena, lakini ukichukua 450,000×12 =5,400,000/= kwa mwaka mzima, hii pesa kwa mkulima ni msimu mmoja tena huyo ni mkulima mdogo kabisa na kwa mwaka kuna misimu miwili.
Ushauri wangu kwa vijana tujaribu kuwekeza kwenye faida yake ni kubwa lakini pia kilimo ni mradi endelevu, idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo mahitaji ya chakula ni mengi kuliko idadi ya watu.