Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Mnapouliza maswali jaribuni kuwa waungwana, porojo za social media zinatoka wapi? Kuna ajabu gani hapo? Mbona hayo mavuno ni ya kawaida kwanza nipo chini ya malengo.
Mkuu asante kwa yoote. Ila je unaponunua mbegu kutoka kenya pale mpakani hawazikamati kwa sababu mbegu na madawa ni lazima yathibitishwe na mamlaka husika.
Kama inawezekana naomba nitumie mawasiliano inbox, na mimi nipo kwenye project ya mahindi na tunatumia mbegu kutoka kenya seed co.
 
Ni kweli kilimo kinalipa sana, naandaa mtaji wa milion 3 nataka nizipeleke shambani, kwa sasa naanda business plan lakini kazi yangu serikalini siachii...kilimo kitakuwa ni nyongeza tu basi

Mkuu wengi wa walioingia hasara katika kilimo ni wale wako ofisini kisha wanaagiza watu wawalimie. Hebu kwenye kilimo hesabu ni kosa namba moja, hiyo lazima ile kwako.
 
Mkuu wengi wa walioingia hasara katika kilimo ni wale wako ofisini kisha wanaagiza watu wawalimie. Hebu kwenye kilimo hesabu ni kosa namba moja, hiyo lazima ile kwako.
Sasa waofisini mnatushauri tufanyeje na tunapenda kilimo sanaa...?
 
Kuna watu wapo busy kuhangaika kutafuta ajira serikalini na mashirika binafsi, wengi hufikiri kuwa wanaweza kutoka kwa kuajiriwa, vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo aidha wanafikiri kuwa kilimo hakilipi na wajanja waliopo huko hawawambii wenzao kuwa kilimo kinalipa.

Nitoe ushuhuda kidogo mwezi wa 9 mwaka jana nimelima ekari mbili gharama haikuzidi laki 5 lakini nimeuza mahindi hayo zaidi ya milioni 3. Na bado mengine nikaacha kwa ajili ya chakula, hebu fikiria sasa ni biashara gani ya laki tano ambayo unaweza ifanya kwa mtaji wa laki tano ukapata mil 3 kwa muda wa miezi 4 kwa kifupi haipo.

Mishahara mingi ya waajiriwa wenye shahada ni 450,000/=(kwa wale wenye mikopo) na 560,000/= kama huna mkopo, sasa tufanye hesabu fupi tuchukulie uhalisia kwamba vijana wengi wamesoma kwa mkopo, 450,000 ukilipia nyumba, umeme, maji na matumizi mengineyo unajikuta haifiki tarehe kumi tano unaanza kukopa tena, lakini ukichukua 450,000×12 =5,400,000/= kwa mwaka mzima, hii pesa kwa mkulima ni msimu mmoja tena huyo ni mkulima mdogo kabisa na kwa mwaka kuna misimu miwili.

Ushauri wangu kwa vijana tujaribu kuwekeza kwenye faida yake ni kubwa lakini pia kilimo ni mradi endelevu, idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo mahitaji ya chakula ni mengi kuliko idadi ya watu.
Bulaza Molembe nakuunga mkono 100%, najiandaa kukodi ekari 5 nilime mpunga mcmu huu.....nitarudi hapa mwakani kutoa mrejesho, Mungu Muweza wa yote akitujalia pumzi ya uhai!
 
Fanya utafit kwanza ndipo utoe ushaur, japo ushaur wako ni mzur sana
Lakin tuangalie risk katika kilimo tanzania tena kilimo endelevu.
Ni kweli mazao ya chakula soko lake ni lauwakika sana
Ila swali la kujiuliza shortage ya mahid iliyopo maeneo ya mikoa ya kaskazin wakulima wa kusuni ambao wanasuplus ya mahid wataweza faidika na hali hiyo
Je nyanya za dumila, mkulima anaweza faidika na shortage ya nyanya dar.
Kisha waza mtu alie chukua mkopo bank na anatakiwa kulipa na riba, kwa hali kama hiyo ataweza.
Maana utafit unasaidia kupunguza riski, ila kuingia ktk biashara bila utafik na kuangalia flan alipata nin tena kwa kipind kifup ni hatar sana.
Ni vema kujua taarifa za zao utakalo kulilima kama sehemu ya uwekezaji wako kuanzia mazingira ya uzalishaji (inputs) kama chanzo ya maji yako kwa hali ya sasa, usafirishaji, pembe jeo na mambo mengine.
Naunga mkono wazo lako
Ukitaka kufanikiwa lazma uwe risk taker, wengi wanashindwa kutoka wakiogopa risk tena hasa kw maneno ya watu wanaovunja moyo.Utamu wa ngoma ingia ucheze!
 
Kujifanya mnajua research sana ndo kunawafanya muwe maskini. Watu wanaongelea ushuhuda bado unataka afanye research tena theoretically??? Ili approve nini wakati tayari ameshafaya pratically??

Tatizo letu vijana tunakuwa sio risk takers! Na lazima tujue the mkre risk you take the more reward you are likely to get!

Sasa mkikutana na waoga kama jawa wanaoogopa kuthubutu na mkawasikiliza mtajikuta mnazeeka maskini na sio katika kulima tu, katika kila biashara watu wa namna hii wapo. Mtu anakwambia mimi nina boda boda yangu na napiga hela kiasi flan kwa mwezi, badalaya kumuuliza unafanye upate hela kama hiyo unaanza kumwambia pikipiki nikinunua itapata ajali! Hawa watu wa type hii ni wa kupuuzwa kabisa!

Mimi nawahakikishia hela ipo kwenye kilimo na ni uhakika sana. Ukichemka msimu wa kwanza msimu ujao unatusua. Cha msingi ni kuwauliza wanaofanikiwa wanapitia njia zipi na sio kuwaambia ukilima mazao yatakauka mvuahaitanyesha.

Achamaneno andaa shamba alafu uvune tuone yakikosa soko sasa!
Haya ndo mawazo ya mcng, co vijana tunajifanya research research watu wanatusua....jiulize wakulima kule kijijini wamelima kuanzia enzi hizo tena bila njia bora za kilimo lkn wamemudu maisha na kuwasomesha watoto hadi vyuo vikuu, leo una-graduate unajifanya hulimi hadi ufanye research!
 
Okey,
Sikuzote uwekezaji unaanza na idea ambayo wewe umeitoa, baada ya hapo unaitaji finance usuport idea yako.
Kama huna huo mtaji, utawezaje kufanikisha hilo
Sehem ambayo unaweza uza idea yako ni bank kwa kuandika business plan yako na wao watakupa mkupo wakiwa na iman ya kurudisha pesa yao pamoja na riba.
Sio jambo lakusema degree itakupa mtaji ila kwa jinsi gan itakupa mtaji ndio jambo la msingi
Bro, em acha kuzidisha ugumu wa maisha....we umeandika b'nss plan ngapi na bank gani imekupa loan nami niandike!? Mabenki yamekuwa yanajinadi tu ila ktk uhalisia pesa ya bank kuipata kw style hyo ni ngumu sana!
 
Kitu chenye pesa na mafanikio hakifanywi na kila mtu mkuu! Ingekua hivyo kila mtu angekua tajiri
Na lazma uwe na moyo wa chuma km yule raia wa England aliyetabiri Leicester FC wangebeba kombe EPL mcmu ulopita lkn leo hii ni billionea, vingnevyo utasubiri sn!
 
Kuna watu wapo busy kuhangaika kutafuta ajira serikalini na mashirika binafsi, wengi hufikiri kuwa wanaweza kutoka kwa kuajiriwa, vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo aidha wanafikiri kuwa kilimo hakilipi na wajanja waliopo huko hawawambii wenzao kuwa kilimo kinalipa.

Nitoe ushuhuda kidogo mwezi wa 9 mwaka jana nimelima ekari mbili gharama haikuzidi laki 5 lakini nimeuza mahindi hayo zaidi ya milioni 3. Na bado mengine nikaacha kwa ajili ya chakula, hebu fikiria sasa ni biashara gani ya laki tano ambayo unaweza ifanya kwa mtaji wa laki tano ukapata mil 3 kwa muda wa miezi 4 kwa kifupi haipo.

Mishahara mingi ya waajiriwa wenye shahada ni 450,000/=(kwa wale wenye mikopo) na 560,000/= kama huna mkopo, sasa tufanye hesabu fupi tuchukulie uhalisia kwamba vijana wengi wamesoma kwa mkopo, 450,000 ukilipia nyumba, umeme, maji na matumizi mengineyo unajikuta haifiki tarehe kumi tano unaanza kukopa tena, lakini ukichukua 450,000×12 =5,400,000/= kwa mwaka mzima, hii pesa kwa mkulima ni msimu mmoja tena huyo ni mkulima mdogo kabisa na kwa mwaka kuna misimu miwili.

Ushauri wangu kwa vijana tujaribu kuwekeza kwenye faida yake ni kubwa lakini pia kilimo ni mradi endelevu, idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo mahitaji ya chakula ni mengi kuliko idadi ya watu.
Mkuu ninakupongeza kwa hatua uliyopiga. Lakini bado sijaridhika na gharama ulotaja, ninasema hivyo kwa kuwa mimi pia nimewekeza kwenye kilimo cha mahindi kwa miaka mitano sasa. Naomba utuoneshe mchanganuo wa gharama zifutatazo:

*Kukodi kila heka 50,000.
*Kulima kila heka sh. ngapi?
*Palizi kila heka sh. ngapi
*Mbegu sh. ngapi kila kilo?
*Kilo ngapi za mbegu kila heka?
*Kuvuna sh. ngapi kila heka?
*Kupanda sh. ngapi kila heka?
*Kupukuchua sh ngapi?
Then tuzidishe mara mbili, pia utuambie wastani wa mavuno kwa heka ni gunia ngapi na uliuza kwa bei gani?

Ni vizuri kuhamasisha watu lakini si kwa kuwadanganya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom