Bakariforever
JF-Expert Member
- Aug 30, 2017
- 510
- 514
Nina taarifa zao zipo kwenye PDF kuhusu kilimo cha mahindi, kilimo cha alizeti, kilimo cha mpunga, kilimo cha maharage Kilindi, na kwasasa wanaelekea kwenye kilimo cha parachichi baada ya kufanya utafiti wao, huwa naliona ghala lao la mpunga na wakulima wao liko Mbingu njia ukielekea Mlimba, kuna jamaa mmoja ambaye ni mnufaika huwa namuona lkn mimi huwa nachukua taarifa zao kwenye kuandaa michanganuo ya makisio kama nikiwa naandika mchanganuo wa biashara kwenda kwenye zile 10% kutoka halmashauri. Binafsi sijawahi kujiunga ila huwa napenda kuwafuatilia hao na TAHA , huwa nalima mimi mwenyewe kama mimi. JATU ni PLC taasisi inayomilikiwa na wanachama wenyewe (ya umma) ina ukitaka kuingia kuna gharama unatoa na kuna gharama Saccos yao inatoa kukukopesha hivyo lazima ijiunge na Saccos kununua hisa. Sijawahi kusikia taarifa za utapeli kutoka kwa watu ila kuna kushuka kwa bei ya mazao na kuna kupanda. Wakianzishaga mradi huanza majaribio kwa wao wenyewe kwanza kujua changamoto kabla ya kuwaambia wanachama wao.Wakuu Wa Kilimo habari!
Naombeni kujuzwa habari za hawa jamaa wanajiita JATU KILIMO, wao wanajinadi kuwa ni kampuni kubwa lenye makao yake dsm, Kazi mojawapo wanayofanya ni kuwasadia wakulima kwa kuwaunganisha na kudanya kilimo kwa niaba yao. Yaani mkulima unatoa pesa 678,000 kwajili ya kilimo cha mahindi, wao watafanya kila kitu kuanzia kulima, kuhudumia mpaka kuvuna, na kukuwekea gharani, kwa eka moja mkulima anapewa magunia 30 ya mahindi hivyo hivyo kwenye mazao mengine kama maharage, mpungu na alizeti.
Maswali yangu.
1. Je, kuna mtu aliswhai kulima now? vile wanaahidi ni vya kweli??
2. Je, kuna harufu yeyote ya utapeli kwenye miradi yao hio?
3. Je, hakuna ubabaishaji wowote?
4. Je, wewe ulishawai kufanyanao biashara hio na ukapata kama wanavyoahidi?
Naombeni maoni yenu wadau, maana natamani nijilipue na eka 50 za mahindi huko kiteto
Hadi hapo nadhani utakuwa umepata mawili, matatu akili kumkichwa kutokana na malengo yako