Kilimo na JATU: Je, kuna ukweli wowote?

Kilimo na JATU: Je, kuna ukweli wowote?

Ukiamua kuwekeza kwenye kilimo, jitahidi uwepo shambani kwa zaidi ya asilimia 70. Kama huwezi kuwepo huko shamba, acha kafanye kitu kingine. Kilimo cha simu na mtandao...UTAIBIWA, narudia tena, UTAIBIWA. Na mkishaibiwa msisahau kwenda kwenye medias kuomba serikali iwasaidie
 
Huu ndio ukweli.
 
Matapeli ni watu hatari sana. Wakulima wanaolima vizuri kabisa anajibunia kupata gunia 18-20 kwa Ekari, huyu hata sehemu husika wanajua kuwa shamba lake analihudumia Sana. Sasa Hawa wa gunia 30.

Kwenye masoko ya hisa kwetu huku janja ni nyingi, mpaka wameenda kule inamaanisha hawana mtaji. Na kuwa kule ni namna pia ya kuvutia wateja ili wapige zaidi.

Kama wengi wanavyozungumza, kilimo kinahitaji mwenyewe ulime siyo ukodi watu. UTAUMIA TU, utapigwa tu, maana hamna namna nyingine.
 
Hamna kitu huko mzee huwezi toboa and i stand to be corrected unalima kulipwa ni kama hawakua wanajua wanatakiwa kukulipa watakusumbua sanaaa narudia watakusumbua sanaaaa
 
Siwajui, lakini jitahidi kufanya uchunguzi sana kabla ya kutoa pesa yako. Gharama za jumla za kilimo cha mahindi kwa wastani kwa ekari moja inawezafika hiyo laki sita na point, ila sijaona wao faida ya kujiendesha itatoka wapi na pia nina wasiwasi wa kufikisha hayo mavuno ya gunia 30 kwa ekari.
gharama haiwezi fika laki sita katika heka hata ulime na tractor na upige alow haifiki
heka moja kulimiwa ni 70000 au tufanye laki +kupandiwa 5000+ mbegu mifuko mitatu tufanye 5000 + palizi 70000 =270000 haya tuongeze 30000 ya palizi ya kwanza inakuja laki tatu
 
Kuna mtu wangu wa karibu alilima na kupata faida na karudia tena kwa mtaji ule ule kapiga heka kadhaa mwaka huu, sasa nasubiri mrejesho wa faida ya sasa.
Wanaonekana wako smart.

Nawapongeza sana vijana walioanzisha JATU kwa kuweza kuja na aidia nzuri, kilimo kina hitaji rasilimali na muda, kwa mfumo wao kama watakuwa smart itakuwa msaada mkubwa sana kwa wakulima wasioweza kufika shamba.
Serikali inatakiwa iwawezeshe hao vijana kwani wamekuja na suluhu. Vijana nao wawasapoti vijana wenzao si kuwakatisha tamaa na kuwabeza bila sababu za msingi, tuwape muda.
JATU n kama suluhisho la ajira kwa vijana kwani wameajiri baadhi ya vijana.
 
Hao ni waongo mimi nalima mahindi sijawahi kuona mavuno zaidi ya gunia 20 au ikizidi sana 23,nalimia kiteto ....huku kuna wakulima wanalima mahindi mpka eka 3000 kilimo cha kisasa wameajiri mabwana shamba,nyenzo zote wanazo ila hawawezi kuvuna hiyo 30.
Jatu itakua analimia kwenye daftari kna mr kuku

Siwajui, lakini jitahidi kufanya uchunguzi sana kabla ya kutoa pesa yako. Gharama za jumla za kilimo cha mahindi kwa wastani kwa ekari moja inawezafika hiyo laki sita na point, ila sijaona wao faida ya kujiendesha itatoka wapi na pia nina wasiwasi wa kufikisha hayo mavuno ya gunia 30 kwa ekari.
 
Binafsi naomba niwaeleze watanzania na wengine wenye nia ya kujiunga na hii kampuni. Nimefanya nao kilimo kuanzia mwaka 2020/2021. Mavuno yalipaswa kuwa 2021. Nimeweka pesa nyingi kwao, nadhani kati ya wakulima 10 na mimi nimo.

Kwanza customer care yao sio nzuri. Yaani unasumbuka sana kufanya kitu cha kawaida. Wanapenda sana pesa ila unapohitaji huduma wanakusumbua sana. Kwa siku unaweza kuongea na watu kama 10 bila mafanikio.

Pili, kuna kila dalili za uongo kwenye kilimo chao. Mfano CEO wa hiyo kampuni anakaa anabadilisha simu. Yaani unaweza kuongea naye leo, kesho akawa na namba nyingine ya simu. Hii ni dalili ya kukwepa watu. Anaweza akawa anakwepa watu hili kuepuka usumbufu wa maswali ya ujinga lakini pia anaweza kuwa anakwepa watu sababu hana majibu.

Nimeongea na manager, CEO...hawa wote mtindo wao wa kukwepa watu ni mmoja tu. Hawawezi kukupa jibu lolote. Hii inaonesha kampuni yao ipo kupiga watu na si kilimo kama wanavyotangaza.

Mavuno ya mwaka huu 2021 yamefanyika ila hawakutangaza maharage wamepata nini...eti mpaka mwezi wa kumi. Sasa jipimie mwenyewe. Yaani unalima kitu kwa mwaka mmoja...pengine hutapata pesa yako mpaka baada ya miaka miwili. Ni nani huwa analima hivyo?

Sasa hivi wametangaza mazao yaliyopatikana kwenye mchele na mahindi. Cha ajabu sasa, wanakwepa simu za watu...yaani huwezi kupiga simu ukaulizia kwamba unataka kuuza mazao yako wakapokea au wakakwambia kitu chochote. Hi ni kuanzia kwa CEO (huyu huwezi kumpata), manager (huyu nadhani anadanganya tu) na wafanyakazi wa kawaida (hawa ndo basi)...yaani management ikiisha sasa wafanyakazi wafanye nini?

Kwa ufupi uhusiano wao na wewe ni pale unapopeleka pesa tu. Hakuna mahusiano zaidi ya hapo. Baada ya hapo huwapati tena. Manager huwa anadai yupo busy kwenye mikutano. Sasa swali ni kwamba, unafanya mikutano na kina nani kama unawakwepa wawekezaji wako?

Serikali ya Magufuli ilikuwa imeanza kuwachunguza. Ilidhani wanauzia watu mashamba ya maharage ambayo hawana. Kwa kuogopa walikuwa wamestisha kuwauzia watu. Baada ya Rais Magufuli kufariki, wakaaza kuwauzia tena watu. Nina wasi wasi kama kweli wana hekari za kutosha za maharage na inaonekana ndio maana hawakutangaza kiasi walichopata.

Kampuni ina kila adalili za ubabaishaji. Wewe hata usiende mbali. Mtafute manager wao..ongea naye kwa week 1. Utajua! Akishajua wamechukua pesa zako anakukwepa.

Nitaendelea kufatilia zaidi na kutoa update kadri ntakavyowasoma. Kwa sasa sitashauri watu wasiwekeze kwao. Ntasema tu watu wawe makini. Kama kuna kitu chochote ntakachojifunza zaidi chenye kunionesha mambo tofauti na haya niloandika ntakisema hapa. Ila kwa sasa, haya ndo nimeona. Hakuna kampuni duniani haithamini wawekezaji. Ukiona kampuni ya hivyo, ni dalili za uhuni.
 
Watanzania kwenye hizi scheme wengi ni wapigaji....Fuatilia mkuu ili uokoe wengine wasipigwe ,niliwaona hawa JATU wakifanya makongamano na Mjomba MPOTO wanauza hisa kwa elfu 5.
 
Na mimi kuna mtu kawekeza kwao namjua wanamzungusha yeye ashaandaa kabisa zigana yake ina risasi 12 ashanieleza iko siku JATU zitaokotwa maiti tu atafagia wote wasipompa chake mapema.
 
Mtindo ule ule wa MR kuku, uliona wapi kilimo au ufugaji wa namna hiyo kwamba wewe utoe pesa ukalale nyumbani usubiri mavuno! Na wanaopigwa ni wazembe tu na lazima mwisho waishie kutapeliwa
 
Nilivyoona huu uzi umerudi nikataka kusema kimeumana tayari .....kumbe bado acha Jatu waendelee kuikusanyia serikali mapato...maana zikishataifishwa huwa hazirudi🤣
 
Mtindo ule ule wa MR kuku, uliona wapi kilimo au ufugaji wa namna hiyo kwamba wewe utoe pesa ukalale nyumbani usubiri mavuno! Na wanaopigwa ni wazembe tu na lazima mwisho waishie kutapeliwa

Inaonekana jamaa wamejisajili kabisa ila serikali wametulia kimya naona wanasubiri mfuko utune wamfilisi ile kwa wana hisa.
 
Kwa ufupi tu, mazao watakwambia wanalima ila ikifika mavuno sivyo kama wanavyokwambia. Wanadai lima na sisi bila stress na vitu kama hivyo. Yaani kwanza unalazimishwa kununua mazao yao. Lazima ununue kilo 50 kila mwezi (sasa jiulize kilo 50 utazinunua uzipeleke wapi).

Baada ya hayo yote, kampuni yao haina njia zinazoeleweka kwenye malipo. Yaani kuja kuuza mazao yako, kulipwa...ni kama vita. Lazima umjue mtu humo au watakuangsisha mpaka basi. Hawaeleweki!

Lazima kuna sababu zinazowafanya wasieleweke. Inawezekana hawana pesa ya kulipa watu. Ndio maana wanakusumbua vile.

Hii inakuwa ni haki yako lakini wao wanaifanya kama wanakusaidia.

Unampigia simu mtu mmoja anakupeleka kwa mwingine...huyo naye anakupeleka kwa mwingine na baadae unaweza kurudishwa kwa mtu yule yule wa kwanza au wote wakukwepe....wasipokee simu zako.

Haya yanafanywa kuanzia kwa CEO, Manager hadi wafanyakazi wa kawaida.

Usumbufu unaopitia unaweza kulima shamba hadi ukavuna. Sasa jipime mwenyewe kama hii ni sehemu ya kuwekeza. Yaani unalima maharage, unasubiri mavuno. Kukulipa au kuyanunua mazao yako mpaka mtu ndani ya kampuni akuonee huruma. Wote wanakuwa wanakukimbia/wanakukwepa ikifika mwisho wa mauzo. Sasa hivi wanasema unasubiri kupewa pesa miezi mitatu (yaani miezi mitatu umesubiri pesa). Uliona wapi kilimo cha namna hii??

Inaweza kuwa ilikuwa kampuni yenye nia ya kufanya biashara lakini management nadhani imewashinda. Kama mkulima analipia shamba, uandaaji na wanavuna mazao (kama wanavyosema), tatizo la kukwepa watu linatokea wapi??

Inawezekana pesa inapelekwa kwenye miradi mingine na mwisho wa siku wanalima vitu hewa. Structure ya kilimo chao ipo kama upatu. Kuna mfanyakazi humo amesema "....ni kama upatu".

Quote Reply
Report Edit
 
Na mimi kuna mtu kawekeza kwao namjua wanamzungusha yeye ashaandaa kabisa zigana yake ina risasi 12 ashanieleza iko siku JATU zitaokotwa maiti tu atafagia wote wasipompa chake mapema.

hawa jamaa ni wasumbufu kwenye malipo ase hakuna jibu unapata linaeleweka ata umtafute CEO wao lugha ni ile ile subiri mchakato
 
Mleta mada Bora hiyo pesa ukaitunza uje UNUNUE mazao kwa wakulima tu.Hutajuta
 
Back
Top Bottom