SoC01 Kilimo chanzo kikubwa cha mabadiliko na maendeleo chanya kwa taifa letu

Stories of Change - 2021 Competition
Aug 21, 2021
1
2
ANDIKO: KILIMO CHANZO CHA MABADILIKO MAKUBWA KWA TAIFA NA KICHOCHEO KIKUBWA CHA MAENDELEO KWA SEKTA NYINGINE.

UTANGULIZI

Sekta ya kilimo,
ni moja kati ya sekta muhimu sana zenye kuchangia kwa kiasi kikubwa kupanda na kushuka kwa pato la taifa hasa kwa mataifa ya Afrika, shughuli za kilimo zimekua zikifanywa mara nyingi kwaku tegemea Zaidi majira ya mwaka ikiwemo vipindi vya mvua(masika) lakini mfumo huu umekuja kuathiriwa Zaidi na mabadiliko na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ikiwemo viwanda yaliyopelekea Zaidi kuathiri mifumo ya ikolojia na kupelekea athari kubwa ya upatikanaji sahii wa majira ya mwaka, hivyo kuathiri kwa kiwango kikubwa uzalishaji katika sekta ya kilimo; lakini pia njia zisizokuwa sahihi ambazo zimekuwa zikitumiwa na wakulima wengi zimepunguza Zaidi uzalishaji katika sekta hii ya kilimo ikiwemo utumiaji holela wa kemikali za kuua vijidudu pamoja na mbolea za viwandani, uzalishaji wa zao la aina moja katika eneo moja kwa muda mrefu pamoja na ukataji na uchomaji wa misitu ili kupata mshamba vimepelekea kupunguza rutuba pamoja na ardhi kukosa uimara na hivyo kupelekea kupata matokea/mavuno hafifu katika shughuli za kilimo. Sekta hii ya kilimo ni moja kati ya sekta zinazopaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kurahisisha njia za uzalishaji katika sekta hii pamoja na kusaidia ongezeko la uzalishaji,

Zifuatazo ni hoja zinazopelekea uchochezi wa mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo:-

Kuwekeza Zaidi katika Kilimo cha mazao ya biashara
, tunaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo kupitia uwekezaji Zaidi juu ya kilimo cha mazao ya biasha na inaweza kuleta maendeleo endelevu kwa taifa letu, tunaweza kuwekeza katika mikoa inayosadifu Zaidi mazao hayo ya biasha kama vile Mtwara(korosho) na Dodoma(zabibu) na hii itapelekea nchi yetu kuingia katika ushindani mkubwa wa uuzaji katika soko la dunia na kuweza kupata fedha nyingi za kigeni, lakini pia itaongeza fursa ya uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi na hii itasaidia kukua kwa miji na majiji.

Kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa uuzaji wa mazao katika soko la dunia,
serikali pamoja na wadau wengine wa masuala ya kilimo wanapaswa kutafuta na kutengeneza njia rahisi za upatikanaji wa maudho ya uhakika wa mazao mengi yanayozalishwa ndani ya nchi katika soko la dunia ili kuwezesha Zaidi uzalishaji wenye faida ndani ya sekta ya kilimo, kwani kwa miaka mingi imetokea kwa taifa letu kuzalisha mazao mengi na mazao hayo kukosa soko kimataifa na hivyo kupelekea hasara kwa wakulima, mfano:- mbaazi ni zao liliozalishwa kwa wingi nchi kwa mwaka 2020 hasa mikoa ya Dodoma na Singida na zao hili kukosa soko kutokana na nchi ya India kuacha kuingiza mbaazi kwa mwaka huo na soko la uhakika la mbaazi lilikuwa katika nchi ya India.

Kuanzishwe sera pamoja na kampeni mbalimbali zitakazo chochea mabadiliko chanya ndani ya sekta ya kilimo, kwani hii yaweza kuwa njia rahisi Zaidi ya ubalozi na utoaji wa elimukwa haraka kwa jamii za kitanzania, sera hizo pamoja na kampeni hizo zibebe maudhui ya kilimo cha kisasa pamoja na uchochezi wa watu kujihusisha Zaidi na kilimo ili kuenenda sambamba na mabadiliko pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia mfanu tunaweza kwenda na sera: ZINDUKA NA KILIMO SASA. Juu ya sera ya zinduka na kilimo sasa kuwe na mabalozi watakao simamia sera hii kwa kutoa elimu juu ya kilimo cha kisasa kisicho lete athari hasi kwa mazingira yetu na kitakacho pelekea Zaidi mabadiliko katika sekta hii ya kilimo na wakulima wote kwa pamoja.

Itolewe elimu kwa jamii nzima ili kuhakikisha kuhakikisha kila mkulima analima kilimo cha kisasa kilicho rafiki kwa mazingira yetu hata kwa wale wavijijini, lakini shughuli za kilimo hasa kwa maeneo ya vijijini imekuwa zikionekana ni shughuli za watu wa chini tu hivyo elimu itolewe kwa jamii ili watu waondokane na Imani hii potofu na hivyo kuona kuwa mtu yeyote anaweza kulima nah ii itaongeza motisha kwa vijana wengi kuliko kungoja na kuendelea kulalamika juu ya ukosefu wa ajira waone hii ni kama fursa kwao wajishughulishe na kilimo na uzuri kilimo hakimfungi mtu maadamu tu una ardhi hata kama umekodi na unaweza kulima basi wewe ni mkulima.

Kujihusisha Zaidi na kilimo cha umwagiliaji kuliko kutegemea mvua, shughuli nyingi za kilimo ndani ya taifa letu zimekuwa zikifanywa kwa kutegemea mvua Zaidi na hivyo mazao mengu yamekuwa yakizalishwa kwa misimu, hivyo basi tunaweza kuleta mabadiliko Zaidi katika sekta ya kilimo endapo watu wataanza kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji ambacho kitapelekea uzalishaji Zaidi katika kilimo bila kutegemea misimu na hii itaweza kuleta maendeleo kwa haraka Zaidi katika sekta ya kilimo lakini pia kwa sekta ya viwanda kwani inategemea Zaidi malighafi kutoka katika sekta ya kilimo.

Matumizi ya mbegu bora za muda mfupi zenye kuhimili ukame, kupitia matumizi ya mbegu bora hii itaweza kuleta mabadiliko Zaidi katika kilimo kwani uzalishaji utaongezeka Zaidi lakini pia tunaweza kupata mazao ndani ya muda mfupi, mbegu hizi pia zinasifa ya kuhimili ukame hivyo zaweza kuwa rafiki ata kwa mikoa yenye ukame kama vile mikoa ya kanda ya kati ambayo imekuwa ikipata mvua za wastani kipindi cha masika.

Kuenenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, itatusaidia Zaidi kuleta mabadiliko chanya ndani ya sekta ya kilimo hii ni pamoja na matumizi ya nyezo rahisi pamoja na pembejeo zinazozalishwa Zaidi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia zinazowezesha kilimo kufanyika katika njia rahisi, lakini pia kuzalisha sambamba na uhitaji wa soko kutokana na uhitaji wa malighafi viwandani.

Punguzo za shuru, kodi pamoja na tozo, ndani ya sekta ya kilimo zaweza kuleta mabadiliko Zaidi ndani ya sekta ya kilimo kwani inaweza kuwa njia rahisi ya kuongeza wigo wa uwekezaji ndani ya sekta ya kilimo lakini pia kuongeza uzalishaji Zaidi kwani wakulima watajikita Zaidi katika kuzalisha na sio kuwaza tena juu ya kodi pamoja na tozo mbalimbali kama zilivyokuwa zikitozwa hapo awali.

Kuwepo kwa njia rahisi za upatikanaji wa bima za mazao kwa wakulima, serikali pamoja na wadau wengine wa masuala ya kilimo wanapaswa kutengeneza njia rahisi kwa wakulima kujipatia bima za mazao zitakazo wasaidia kupata fidia ya mazao yao endapo kutatokea uharibifu wowote wa mazao utakaojitokea kutokana na majanga ya asili au hata yasiyokuwa ya asili, hii itapelekea kuinuka Zaidi kwa wakulima kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakizalisha kwa bahati nasibu na uharibifu wowote wa mazao uliokuwa ukijitokeza walipambana nao na hasara ilikuwa juu yao.

Kuendeleza kilimo cha mashamba makubwa ya miti, kwani hii huchangia Zaidi kulinda na kutunza mifumo ya ikolojia nah ii itapelekea kuapata vipindi sahii vya majira yam waka ikiwemo masika yenye mvua za kutosha, lakini pia kusaidia ulinzi wa ardhi yetu na kusaidia ongezeko la uzalishaji wa malighafi zitokanazo na miti ikiwemo mbao, nguzo lakini pia mkaa kutokana na misitu yetu ya kupanda na hii kupelekea ulinzi kwa misitu yetu ya asili.


FAIDA TUTAKAZO ZIPATA BAADA YA KUTEKELEZA HOJA ZILIZO ORODHESHWA HAPO JUU.

Kupitia yote hayo itatusaidia kujipatia fedha za kigeni kwa wingi kutokana na kuuza mazao yetu mengi kimataifa, tutaweza kuongeza wigo wa uwekezaji kwenye sekta ya kilimo, itawasaidia wakulima wetu kutokutegemea mvua tuu ili kulima bali wataweza kuzalisha Zaidi kwa kilimo cha umwagiliaji bila kutegemea misimu, kupitia bima za mazao wakulima wetu watakuwa na uhakika wa kile wanachokitarajia na itawasaidia kuepuka hasara walizokuwa wakizipata mwanzo walipokuwa hawana bima za mazao, itawasaidia wakulima wote hata wale walioko vijini kupata elimu na kufanya shughuli zao kitalaamu, itatusaidia kuwezesha kwa kiwango kikubwa juhudi za Serikali yetu za kupeleka nchi katika uchumi wa viwanda kwani kutakuwa na upatikanaji mkubwa wa malighafi zitakazo tumika katika viwanda hivyo hapahapa ndani ya nchi,ongeeko la upatikanaji wa ajira kwa vijana kwani itawawezesha wengi kujishughulishana shughuli za kilimo hata kama si kuingia shambani kulima bali hata kufanya biashara za mazao, itapelekea kukua kwa miji na majiji, ongezeko la pato la nchi, itasaidia kukua kwa sekta nyingine ikiwemo uchumi, viwanda na biashara.
 
Back
Top Bottom