Nimeona wakulima wengi wa pamba hasa mkoa wa mwanza wakikipa kisogo kilimo cha pamba ambacho kinachangamoto lukuki.
Bei ya pamba ni kikwazo kiasi kwamba ni Bora kulima mahindi ambayo yana soko na pia yanaweza kutumiwa na familia husika kuliko pamba.
Wakulima wamekuwa wakipikwa( mara kadhaa) mbegu zisizoota na wakati Mwingine viuatilifu feki Hali inayoshusha uzalishaji na kuongeza umaskini.
Kumekuwa na makato mengi ktk kilo ya pamba ambayo yote humlemea mkulima huku wafanyabiashara wakipanga njama za kumuumiza mkulima.
Utashangaa makao mkuu ya bodi ya pamba yakiwa Dar es salaam ilihali zao hilo likizalishwa Kwa wingi kanda ya ziwa.
Kwa ushauri wangu ni vyema wakulima c wazalishe aina nyingine ya mazao kuliko pamba.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.