Kilimo cha Mchaichai(Lemon Grass): Utaalamu, Masoko na changamoto zake

brazoo

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
707
508
Poleni na majukumu wakuu, nilikua nataka mnijuze ABC za kilimo cha mchaichai hapa Tanzania hasa nilitaka kujua sehem ambazo hili zao linapatikana kwa wingi au sehem ambazo linastawi vizuri

Nitashukuru sana kwa michango yenu

Unemployed graduate
 
Sehemu gani mchaichai unasindikwa au kuuzwa kibiashara, wapi ambapo unaweza kupita usione mchaichai umepandwa kwenye fensi na kwenye makopo!
Ha!ha! Bro unachekesha kweli na hujaijua tu fursa iliyopo kwenye mchaichai.Kifupi soko la mchaichai kwa Dar tu halitoshelez mchaichai unatafutwa sanabado hujapata chance ya kuupeleka nje ya nchi haswa Italy.Kifupi mafuta ya mchaichai ni dili sana.mafuta ya mchaichai yanatumika kutengenezea perfume,kiungo muhimu sana,pia unatibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kansa ya damu,pia kama kinywaji
Ni zao ambalo mtu akiwa siriaz linakupa pesa ya kutosha,kuupanda mpaka kuuvuna ni miez minne tu,baada ya hapo unakua unavuna mara kwa mara kwa mwaka unavuna mara nne.Kwa mwaka jana kilo 1 ya mchai chai ilikua inauzwa 3000 kwa ufupi ukiwa na ekari moja kwa kila mchumo au uvunaji utapata wastani wa milion saba kulingana na bei ya soko yaweza ikazidi ukiweka gharama za shamba na uvunaji na usafiri mara mwaka faida ipo kubwa sana.Kwa Bongo hakuna kiwanda hata hao utakaowauzia wanapeleka Zanzibar ndo kuna kiwanda.Kuna jamaa wanadeal na hiki kilimo wanajiita Mtandao wa kijani kibichi wapo KimaraTemboni waone watakupa ushauri,mbegu na kila kitu.
Kifupi Watanzania tukiamka na kuacha kupiga blabla hiki kilimo kina manufaa sana pia waweza kuona kuajiriwa ni utumwa masoko mengi sana .cheki hii link . Nime attach hii inahusu market research ya mchai mchai na masoko yake
 
Attachments

  • Lemon-Grass-Market-study-2009-_revised-Jan-2010_-_2_1(1).pdf
    413.1 KB · Views: 419

Shukrani sana mkuu nimeangalia hiyo video na kusoma hiyo PDF kwa kweli nimehamasika sana,kuna product ya mchaichai nataka nitengeneze kwa kweli umenisaidia sana,naamini morogoro ni sehem ambayo naweza kulima vizuri kabisa
 
frusa zipo nyingi shida ni uthubutu, ukidhubutu mtaji hauna! changamoto nyingi zinaturudisha nyuma sana.
 
Attachments

  • Screenshot_20170131-153152.png
    Screenshot_20170131-153152.png
    33.2 KB · Views: 303
Unemployed graduate unauliza mchaichai? Pumbavu kabisa!
Kama hujui kitu ni bora kunyamaza, sasa tumeshamtambua mpumbavu ni nani kati ya unemployed graduate na wewe.

[HASHTAG]#NoResearchNoRightToSpeak[/HASHTAG]
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimewahi hudhuria maonesho ya viwanda Desemba pale viwanja vya sabasaba Dar es salaam, wajasiriamali wengi walikuja Na bidhaa zilizosindikwa pamoja Na mchaichai,viungo ,madawa Na ladha mbalimbali walipata Wateja wengi Na bidhaa zilikuwa zinahitajika mno ni bidhaa nzuri mno.

Naamini kuna haja ya kushiriki fursa hii.

Asante kutushirikisha Jambo hili.
 
waulizeni kwanza walowafuata kijani kbichi pale morogoro wakafuga Sungura, mende na wakalima mchaichai waliishia waapi. Maisha hayako simple kama mnavyofikiria, ukisikia jambo usikurupuke kama digi digi mjini. inauma saana kuona watu ambao hawana utaalamu wowote wa kilimo wakiwahadaaa wakulima mchana kweupee.

Nilimshaur saana dadaangu kuhusu hizi fursa lakini alikuwa mbishi saana saana. mmatokeo yaake anataka kwenda mahakamani.

Wito wangu fanyia utafit fursa yeyote utafitii wa kutoshaa kabisaa kabisaa teena uufanye wewe mwenyewe na sio kuulizia kwa watu
 
Sister ako alishika fursa gani?.....maana kuna hawa jamaa wa sungura ukiwasikiliza utaona life is so simple!!!
 
hahahahahaha ni kweli mkuu alishika Sungura na Mchai chai na walikuwa wana mtembelea kwa sana tuu mpaka akaanza kunicheka. kimbembe ni sungura walipoanza kuzaa. jamaa hata simu hawakupokea. akawacheki na namaingo ikawa kimyaa wao wakamwambia boraa angenunulia kwao. mchai chai umefia shambani maskini hakuna cha kuja na machine wala nini
 
Maskini....pole yake.....alichukua wapi Sungura?.....nashangaa wanakuuzia Sungura 85,000 ila wakizaa wao wanamnunua 24,000 mabanda ununue kwao, emergency kit, vyakula etc. Wahuni tu hawa!!!.....
 
Yan huku kwet mchai chai ni kama mauwa tu hakuna wakyyatmia yakikus tunayafyeka kama majan mengine nipen hlo dill
 
Back
Top Bottom