Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Pilato2006

Senior Member
Aug 25, 2008
124
35

Wana JF, nataka kufanya kilimo cha mapapai ila nahitaji mbegu za muda mfupi kuzaa ili nianze kuvuna mapema. Naomba msaada wa yafuatayo

1 Wapi nitapata mbegu fupi za muda mfupi kuanza kuzaa?
2. Nikitaka kupanda spacing iwe kiasi gani toka mche hadi mche?

Asanteni sana hii ni katika kuhangaika kuongeza kipato maana hii nchi ukizubaa ukajikuta unanyong'onyea sana kwa wanayojili.


Ushauri kutoka kwa wadau




 
Nenda Chuo cha Kilimo SUA utapata ushauri wa kitaalam zaidi.



============

 
Wakuu natafuta miche ya Mapapai makubwa. Nataka kulima. Wapi nitapata ushauri wa kitaalam (Nipe contacts)
 
Very easy nunua mapapai size unayoitaka then toa mbegu upande naona umeamua kuingia kwenye kilimo kwanza.

anatafuta miche ya mipapai wewe unamwelekeza akatoe mbegu .... kuna tofauti sana kati ya mbegu na miche .... miche inakuwa tayari imeshakuwa-selected kupata mbegu bora na kutunzwa kwa ubora na muda muafakakwa ajili ya kuihamisha (transplantation)

mbegu huoteshwa .... na miche huhamishwa
 
Aiseee bora ufate ushauri wa shossi,mche m1 wa mpapai ni kama buku hivi mikubwa ila ukinunua unaweza ukakuta yote mipapai dume haizai inatoa maua tu na huku uswazi wanasema unafunga bunzi la muhindi zen unabadilika sijui kama it works!
 

Sawa mkuu lakini kumbuka mipapai sio mayai! ukinunua mayai makubwa unauhakika kifaranga kikitotolewa kitakuwa kikubwa unaweza kuuziwa miche ukaambiwa ni mapapai makubwa kumbe ni watoto wa papai! ndio maana njia sahihi ni kununua size uitakayo halafu ukapanda mwenyewe unless unataka kupanda uawani lakini kama ni kwa kilimo cha biashara hiyo ndio njia mwafaka.

Pilato:

Study zinaonyesha sisi wakulima tunapenda kulima tunavyopenda sisi na sio vinavyopendwa na soko sijui umefanya utafiti ukajua ni mapapai gani yanapendwa? na yapi ni economy to grow?
 
Naona upo kimya mkuu ila ningekushauri utafute mbegu ambayo inavumilia kupata ugongwa hasa wa virus wanaoitwa rig worms, kama ni kwa biashara tafuta mipapai inayozaa mapapai mengi ili ikupatie mapapai 3 kwa wiki kila mche mmoja i.e 3 papaya per tree assume you have 2000 trees you will have 6000 papaya uza bei ya chini shs 300 kwa papaya moja!
 

Attachments

  • mitoboto project.jpg
    63.3 KB · Views: 5,715

Mohammed Shossi

mkuu ... hii aina ya zao hili la papai inaitwaje kwa kitaaluma ya kilimo ...specie
 
Last edited by a moderator:
Mohammed Shossi

mkuu ... hii aina ya zao hili la papai inaitwaje kwa kitaaluma ya kilimo ...specie

Kuna mbegu nyingi zilizofanyiwa utafiti duniani kama F1 Hybrid Taiwan Princess mbegu hii sio genetic kwahiyo inaweza kulimwa nchini na ni nzuri kwasababu shelf time yake ni kubwa kulinganisha na papai zetu za kienyeji na zinaweza kuuuzika nje ya nchi (Ideal for export)
 

great ... je soko la papai unalionaje ... zaidi ya local fresh fruit market and vending ...je kuna soko zaidi ya hilo? .... au supermarkets kama shoprite au shoppers plaza pia wanaweza kununua once unakuwa na zao bora

share your opinion
 

Juzikati nilikuwa Nzega mjini, wakati nasubiri mhudumu wa ofisi ya M-pesa afike nikawa naangaza macho, nikamuona jamaa anashusha tenga la mapapai makubwa ajabu kutoka kwenye basikeli. Sikuvumilia, nikamsogelea na kumuuliza
mbegu alizipata wapi, akasema yeye alikula papai akamwaga mbegu zake na matokeo ndiyo hayo.

Kusema kweli papai zile zina ukubwa wa kufikia kilo 7 hivi kwa kukadilia, ulefu wake haupungui futi moja na nusu na unene wa chini kama inchi 8 hivi.(niko vizuri kwenye kukadilia)
Kwa namna lilivyo, nusu tu inatosha kuliwa na familia ya watu sita. Papai ninaloliona hapo kwenye miti yako Mohamed, kwa sasa hapa Dar ni kama Tshs.1000/=. Ninalozungumzia, changanya hayo matatu na nusu ndiyo unapata moja, pengine kuliuza inaweza kuwa tabu kidogo.
 
great ... je soko la papai unalionaje ... zaidi ya local fresh fruit market and vending ...je kuna soko zaidi ya hilo? .... au supermarkets kama shoprite au shoppers plaza pia wanaweza kununua once unakuwa na zao bora

share your opinion

Soko lipo lakini sio la mapapai ya kienyeji ambayo ni very perishable hiyo mbegu niliyokutajia ikiiva kabisa papai lake linakuwa na ugumu fulani ambao unaweza kulifanya limudu kukaa more than 7 days kwa maana hiyo ni papai ambayo inaweza kuuzwa nje ya nchi!

Serikali kama ina mipango madhubuti ingewaelimisha wananchi wakazane kwenye kilimo cha matunda na mboga mboga na kusafirisha kwenda nje! Ni aibu kushindwa kutumia mashirika ya ndege yanayotua na kuruka daily from Tanzania to 100 different destinations bila ya mazao kutoka Tanzania.

Ukifika nchi kama Saudia ndege nyingi hushusha matunda ya aina mbalimbali kutoka nchi tofauti duaniani na hata ukienda dubai hali ni hiyo hiyo hawalimi lakini tunda lolote ukilitaka unapata!
 
Kamuzu,
Mkuu kwenye kilimo cha biashara hatuangalii ukubwa wa tunda tunaangalia ubora wa tunda kwenye mambo makuu matatu:
1. Uvumilivu wa magonjwa
2. Kutoharibika haraka baada ya kuiva
3. Ladha nzuri

Mapapai makubwa hata mimi ninayo mbegu zake lakini hayana ladha nzuri yanawahi kuharibika yakiiva, uchukuzi wake ni very costly as ni mazito ukiweka juu papai jingine la chini halifiki salama! Na miche yake haivumilii ugunjwa wa ring spot.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…